Kuna ugonjwa ukiumwa unakuwa unakiona kifo

Kuna ugonjwa ukiumwa unakuwa unakiona kifo

Kama huamini Mungu yupo basi anza kusali leo kuna majanga ukipitia unatamani usali kwa lugha zote za ulimwengu huu, unamuona kabisa Israel mtoa roho anakukaribia Ule ugonjwa ulifanya niombe kila aina ya sala wakati kanisani nina miaka sijawahi kugusa, mafua makali, kizunguzungu na kuishiwa nguvu mara chache nikawa napumua kwa kuhema na kwa tabu sana haikuwa homa wala mafua ya kawaida niliyoyazoea

Siamini mpaka sasa niko hai japo sikupima lakini naamini ile ni hii new cases, zile wiki karibia 4 kasoro zilikuwa za mtihani mkubwa sana kwangu.

Naanza kwenda kanisani rasmi naamini ni mungu tu aliyeniponya
Mungu apewe sifa na kila mwenye pumzi aseme Amen
 
hii kitu ilinipiga ..nikawa kila nikikaa nasikia ule wimbo wa niagieni ..niagieni...pua zote zikaziba...koo linakereketa...tumbo linasokota...ngozi inacharara...akili ikarudi kwenye 2G...nikawa nakula mlo kama nakula makapi...kusema kweli niliumwa mnoo..nauhakika asilimia 199.95% ilikuwa ni ile kitu...nilkuwa nikilala naota majeneza tu..
 
😀😀😀mkuu umesema kweli kabisa ni hivyo aisee😀😀😀😀 Eti niageni
 
hii kitu ilinipiga ..nikawa kila nikikaa nasikia ule wimbo wa niagieni ..niagieni...pua zote zikaziba...koo linakereketa...tumbo linasokota...ngozi inacharara...akili ikarudi kwenye 2G...nikawa nakula mlo kama nakula makapi...kusema kweli niliumwa mnoo..nauhakika asilimia 199.95% ilikuwa ni ile kitu...nilkuwa nikilala naota majeneza tu..
Hiyo ya tumbo acha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simulia sana ila omba yasikukute...Hapa nilipo sina uwezo wa kusikia harufu yoyote wala kuhisi radha ya chakula chochote

Viungo vya mwili ndio usiseme vinavouma...Pua zimeziba hii inaelekea siku ya 7 au 8 na hamna dawa ya mafua iliyonipa nafuu

Covid ni hatarii naamin nitapona tu inshaallah...
Pole sana jamani
Utapona, Mungu ni mwaminifu sana
 
Unahisi dudu ulikutana nalo maeneo ya wapi?
Taja mtaa, na mji kama inawezekana ili tujue maeneo hatarishi zaidi.
 
Daaa huwa nawaza sana kwa tulio na watoto wadogo na wachanga. Mana inashauriwa mtoto asifukizwe hata kidogo, itakuwaje!? Mungu upo simama nasi viumbe wako tutapona!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ajabu ya Mungu ni kuwa watoto wengi hawaathiriwi na huu ugonjwa. Dawa za kawaida za homa na mafua zinawatibu.
Ngoma iko kwa vijana wa kiume waliokwenye rika la balehe, na wanaume watu wazima ambao wameshashusha libido. Hapo ndo akiwa na magonjwa nyemelezi basi covi anafanya yake.
 
Back
Top Bottom