Kuna ugonjwa ukiumwa unakuwa unakiona kifo

Mungu apewe sifa na kila mwenye pumzi aseme Amen
 
hii kitu ilinipiga ..nikawa kila nikikaa nasikia ule wimbo wa niagieni ..niagieni...pua zote zikaziba...koo linakereketa...tumbo linasokota...ngozi inacharara...akili ikarudi kwenye 2G...nikawa nakula mlo kama nakula makapi...kusema kweli niliumwa mnoo..nauhakika asilimia 199.95% ilikuwa ni ile kitu...nilkuwa nikilala naota majeneza tu..
 
😀😀😀mkuu umesema kweli kabisa ni hivyo aisee😀😀😀😀 Eti niageni
 
Hiyo ya tumbo acha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana jamani
Utapona, Mungu ni mwaminifu sana
 
Unahisi dudu ulikutana nalo maeneo ya wapi?
Taja mtaa, na mji kama inawezekana ili tujue maeneo hatarishi zaidi.
 
Daaa huwa nawaza sana kwa tulio na watoto wadogo na wachanga. Mana inashauriwa mtoto asifukizwe hata kidogo, itakuwaje!? Mungu upo simama nasi viumbe wako tutapona!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ajabu ya Mungu ni kuwa watoto wengi hawaathiriwi na huu ugonjwa. Dawa za kawaida za homa na mafua zinawatibu.
Ngoma iko kwa vijana wa kiume waliokwenye rika la balehe, na wanaume watu wazima ambao wameshashusha libido. Hapo ndo akiwa na magonjwa nyemelezi basi covi anafanya yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…