Kuna ugonjwa ukiumwa unakuwa unakiona kifo

Hizi dalili zilimpata pia dogo hapa home.
Natamani mods wazikusanye hizi dalili ili tupate dalili za ugonjwa huu hapa kwetu.
 
Una uhakika na ulisemalo. Nina twins hapa miezi 7 sasa nawalinda kama ulinzi wa jiwe akiwa kwenye ziara. Nina hofu ishu za kushindwa kupumua, watoto wakipatwa watastahimili kweli? Muda si mrefu nilikuwa nachimba biti Mana Mama yao alitoka nao nje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usilegeze kamba maana hata kama siyo hao watoto wewe mwenyewe unaweza kuwa muhanga. Mwanamke anauleta unashangaa yeye anapata mild symptoms ila kwako mwanaume zinakuwa severe. Kwa hiyo beat liendelee tu ndugu.
 
Wana wake akili zao wanazijuwa wenyewe!!!!
 
Ss Mungu alivyi waajabu..wanatoka aalama hawaumwi mimi kipindi najihis nna malaria kumbe sio..mwanangu anakuja ananibusu mara nilishe namlisha ..nalala nae etc..baadar nilivyoanza kuona sinusi nikasema hili goma jipya hili limenikumba..nikaanza mwazia mwanangu but suprisingly mwezi ss tangu nipone walaa hajaguswa....so pray for them wako salama hao malaika lkn walinde usirelax
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana Mdau, Mimi pia tarehe 27 march (kipindi hicho mdudu futa hakuwa ni habari kubwa huku kwetu), niliamka najihisi kuumwa mafua kadri muda ulivyozidi kwenda nilihisi yanazidi kuwa makali jioni baada ya kutoka kazi huwa nakawaida ya kufanya jogging na wenzangu sasa siku hiyo kiukweli tukiwa mazoezi kiukweli nilishindwa kumaliza na wenzangu nikaishia njiani, Nikiwa bado mwili umechemka unatoka jasho jingi lakini cha ajabu nahisi baridi kali na ngozi ikatoka vipele vya baridi na vinyweleo kusimama, Jamaa angu akaniambia hii itakuwa ni malaria nikupeleke hospital ukacheki nilimwambia hapana huwa nina mafua makali na yamenianza leo tu, labda unisaidie kunipeleka nyumbani, Kuna mdau mwingine pale alivyosikia nikisema hivyo akashauri nitumie dawa inaitwa "mara moja na piliton" hutibu haraka mafua. Nilipofika home nikaji isolate pia mwili ulikuwa mchovu sana kiasi kwamba hata kuzungumza na watu nilikuwa naona ni kazi kubwa mno, nilifikia kitandani nikajilaza na branket juu wala sikuoga kwani nilikuwa nikihisi baridi la ajabu nikajikunyata kushituka, hapo mafua ndio yamepamba moto pua zote zinaziba napumua kwa mdomo tu pia kifua, mbavu na kichwa kinauma balaa asee asikwambie mtu na ilikuwa kama saa nne hivi usiku, hapo sasa hofu ilinikamata nikasema au ni hii pandemic mdudu futa amenikamata au ni mafua tu ya kawaida? Nilisurrender sasa nikataka nijisalimishe hospitali kiukweli niliamka pale kitandani nilikuwa siwezi kusimama wima manake nilikuwa napata maumivu balaa, kwa ule uvivu ikanibidi niagize dawa zile nilizoshauriwa "nikaletewa dawa Fulani za chenga chenga hivi zina rangi nyingi nyingi pia na paracetamol nikajitahidi kula chakula nikanywa na hizo dawa then nikajilaza, nilikuja shtuka usiku kama saa tisa ama kumi usiku yale maumivu yamepungua kwa kiasi kikubwa na kichwa hakiumi kabisa pia pua moja imefunguka aiseee nilimshukuru sana Mwenyezi Mungu nikapata amani, Kwa ufupi nilivyoamka asubuhi sikuwa na maumivu tena na mafua yalikaa kama siku mbili tatu yakaisha kabisa, hadi leo huwa sipati picha ilikuwa ni mafua ya dizaini gani yale,
NOTE yangu ni kwamba tuchukue NA tuzingatie sana tahadhari wadau, pia ukipatwa na janga kama hili jaribu kuondoa hofu na uamini ni la muda litapita. Pia fanya uwezalo uwakinge wanaokuzunguka hasa wazee, wenye magonjwa sugu na mtu yeyote yule aliye karibu yako.
 
Kabisa nakwambia mwenyezi Mungu ni waajabu sana mimi pia yaani nilikuwa nawazia sana familia yangu lakini cha ajabu hadi sasa dogo yuko vizuri kabisa hata hajawahi kutetereka. Tunachoweza sema Our God is an Awesome God
 
pole sana ndugu yangu
 
Mi nahisi kilichonisaidia ni mazoezi maana mbavu hazikuuma ila koo, kifua na maumivu ya joint kama nimepigwa mawe ni hatari. Na jana usiku saa 7 ndo nimeanza kuisikia harufu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…