Kuna uhusiano gani wa CC za gari na ulaji mafuta?

Gari ya diesel in return pipe ambayo hurudisha mafuta ya ziada ambayo hayakuingia kwenye combustion chamber lkn hili wataalam wanaweza wakaliweka vizuri zaidi
 
Labda gari ikiwa na cc kubwa kiwango cha mafuta kinachoingia kwenye cylinder ili kunguzwa ni kikubwa kuliko ya kile cha gari yeye cc ndogo. MF cc kubwa inachukua kijiko cha chakula cha mafuta kwa muunguzo mmoja kwa cylinder lkn cc ndogo inachukua nusu kijiko cha chai kwa muunguzo mmoja kwa cylinder, huo ni muono wangu wa kawaida tu.
 
huwez sema exactly engine ya cc 1000 itakuwa mafuta kiac gan kwa km flan ni mpaka injin iwekwe kwa gar ndo wafany test then watoe majib . mfano injin za toyota unakuta moja imetumika kwa magar kadhaa tofaut ambayo ni kimaumbo uzito pia application ya gar husika hvy utakuta fuel consumption ni tofaut wakat injin ni lile lile imetumika kwa magar mawil tofauti.
 
na co kwel kuwa gar ya cc 2000 ikifungwa turbo inafikia ya 2500 icyo na turbo inategemea na hyo turbo inaongeza asilimia ngap ya orijino power magar ya kawaida huwa turbo inaongeza 30_40% kwa injin some high perfomanc car zna turbo boosting up to 100% au zaid
 
Nimesoma maelezo yako vizuri sana. Asante kwa ufafanuzi.

Naomba nijuze.. ivi mafuta ya Petrol yanayouzwa kwenye vituo vya kuuzia mafuta zinatofautiana??..

Mfano: baadhi ya vituo unakuta petrol hii ni "unleaded"

Kwenye kituo kingine utakuta Petrol ni "super"

Wengine utakuta ni " Premium"

Tofauti na Diesel huwa naona ni diesel tu.

Je hizi ni brand name tu au huwa zinatofautiana ubora.

Kama kuna utofauti wa ubora. Ipi ipo recomended, kwa uzoefu wako.

Thank you in advance.
 
Mkuu inawezekana mengine uliyoyasema ni sahihi lakini ili la kusema gari ikiwa na Cc kubwa ni ya diesel sio kweli. Kuna magari ya diesel yana cc 2,700 na wakati huo kuna magari ya petrol yana cc 4,700, mfano VX V8. Hapo sijui unasemaje.

Tiba
Yeah na kuna brevis pia 2500/3000cc ni petrol
 
Kama ni sensors za Fuel system na au ignition system kuna uhusiano mkubwa sana mkuu.
Mkuu kama sensors za fuel au ignition system zina tatizo utajuaje? Je mafundi wa mtaani wanaweza jua hili?kwasababu gari yangu imeongeza matumizi ya mafuta na fundi wangu naona kama imeshamshinda.
 
Mkuu @prondo njoo utoe jibu hapa
 
Ni sawa na kulinganisha miili hasa vitambi, mwenye kubwa lazima ale sana kuliko mwembamba
 
CC ni cubic centimeters
Yaani total volume ambayo piston inasweep wakati inanyonya na kucompress mafuta
Kutoka BOTTOM DEAD CENTRE(BDC) Mpaka TOP DEAD CENTRE (TDC)
Yaani jumla ya ujazo (eneo la wazi) ya cylinder zote, ujazo ukiwa mkubwa inamaana volume ya mafuta pia yanayonyonywa SUNCTION itakuwa kubwa,
Nguvu ya engine inategemea UWINGI WA MAFUTA YANAYOKUWA COMPRESSED na CALORIFIC VALUE YA MAFUTA HUSIKA
kumbe
Power= total volume(fuel)*calorific value ya fuel
Hitimisho CC ikiwa kubwa engine inakula mafuta mengi,ila power ya engine haitegemei uwingi wa mafuta tu ,inategemea ni mafuta aina gani na yana calorific value ngap(ENERGY CONTENT)
 
Maelezo yako ni mazuri sana,sasa hebu fafanua pale unapokuta gari kama Ipsum new model cc2400 engine vvti inakuaje inakwenda almost sawa na gari ya cc 1500 yaani 1liter inagonga mpaka 13km.
Jibu ni rahisi
Kuna uwezekano mkubwa gari yenye Engine ndogo kula mafuta mengi ukilinganisha na yenye Engine kubwa na sababu ni hizi
1. Gari inakula mafuta mengi unapotembelea gia kubwa yaani Nr .1
2. Kwahiyo gari ndogo pahala unapotembelea gia Nr 1 au Nr 2 kwa gari yenye Engine kubwa unatembelea gia Nr 4 au tano.
3. Ngari yenye Engine ndogo inabidi wakati mwingi ukanyage mafuta mpaka mwisho wakati Engine kubwa ukikanyaga kidogo unapata mwendo unaouhitaji
4. Mambo mengine yanayochangia ulaji wa Mafuta Aina ya Matairi, Upepo katika matairi, Barabara (mzuri au mbovu)
Kasi ya Upepo, Kufungua kioo pia kunachagia ulaji wa Mafuta, Mkato wa gari (yaani gari yenye kioo cha Flat kama Defender itakula mafuta mengi kulikoni yenge round Glasses
Ziko Fakto nyingi
 
Ufafanuzi mzuri.
 
ni ukweli petrol ikichomwa inakuwa imechomwa ila diesel ikichomwa inarud tena
 
ni ukweli petrol ikichomwa inakuwa imechomwa ila diesel ikichomwa inarud tena
Petrol na diesel yote ni mafuta ila wakati wa uchomwaji baadhi hurudishwa kwenye tank na kwani sio mafuta yote uchomwa kwa wakati mmoja mengine hubakia na kurudishwa kwenye tank, mfano mzuri ni toyota spacio ambapo gari hii utumia petrol, ukifungua mfuniko wa tank wakati iko sailensa utaona baadhi ya mafuta yanachuruzika kutoka kwa ndani kidogo ambapo kuna pipe yakurudisha mafuta na kuelekea kwenye tank
 
hapo kwenye red, inakuwaje?
 
hapo kwenye red, inakuwaje?
Aina ya Matairi nilikusudia Profile ya Pira wenyewe (Umekakwa na Kashata kubwa kama mpira wa Offroad au ya kwaida tu)
Hio inaongeza au Kupunguza Friction kwenye Barabara
Mipira vile vile iana Klass zake na Speed zake Kwa Mfano:
F-Index 80 km/h
G-Index 90 km/h
J-Index 100 km/h
K-Index 110 km/h
L-Index 120km/h
M-Index 130km/h
N-Index 140 km/h
P-Index 150 km/h
Q-Index 160km/h
R-Index 170 km/h
S-Index 180 km/h
T-Index
T- 190 km/h
U-Index 200 km/h
 
power to weight ratio ..engine doesnt have to work harder


yu may find a car like IST with five psg kuna saa inakula mafuta mengi kuliko rav4 ya cc 2000 ni kwa sababu ya hcho kitu power to weight ratio mliman injin ndogo inafanya kazi kubwa ku maintain spid flan hivo rpm inakuwa juu mafuta yanaeza kwenda mengi sana
 
VVTI ni ya zaman kidogo mpya.ni hizi D4 au D4D kwa upande wa toyota GDI kwa mitsubishi na TDI kwa audi na bmw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…