Kuna Ukweli gani juu ya mafuta na maji ya upako?

Umenena yoote..... unakuta unauamwa unafanya mavipimo hospital tofauti tofauti unaambiwa hauna ugonjwa au unachoumwa hakiendani na unachojisikia...... hapo ndio utajua dunia ina pande mbili
Madaktari wanakosea, hospitali nyingi za bongo hazina vifaa vya kisasa, kukiwa hakuna vifaa vya kisasa vyenye uwezo wa ku detect ugonjwa sio sababu ya wewe kusema ni uchawi

Mama yangu mzazi alipimwa hospitalini akaambiwa anauvimbe tumboni, akapanic nikamuambia nenda hospitali binafsi, huko akakutwa yuko fresh hana tatizo ni tumbo tu lakawaida linamsumbua.

Kuna mwingine aliandikiwa kufanya upasuaji baada ya vipimo vya xray kuonesha kuna kitu kipo ndani ya mwili wake, lakini mwisho wa siku ilikuja kufahamika kua mende aliingia kwenye mashine iliyotumika kupima, so kile kitu kilichokua kinatafsirika kipo tumboni kwa mtu ilikua ni mende ambaye yupo kwenye hicho kifaa
 
Ishu ya sadaka makanisani nowdays inafanywa kama kiingilio

Afu nilichokuja kubaini kanisani ndio kumesheheni watu wenye roho mbaya sana

Nakupa kisa kimoja

Kuna siku nilikua nimeenda church, kama kawaida ibada iliendelea na mwisho pastor akaitisha sadaka, watu tukatoa

Mwishoni kila mtu katoa sadaka tunasubiri afunge ibada, nikaskia pastor anasema "leo tumetembelewa na mtoto mdogo wa miaka 7 anaumwa moyo na anahitaji msaada wa kifedha kwa ajili ya matibabu, yeyote mwenye kiasi chocjote tunaomba mchango wake"

Mimi nikawa najiuliza, tumekua tukiambiwa kua sadaka zinatumika kusaidia mayatima na watu wasio jiweza, leo hii tumetembelewa na huyu mtoto, kwanini isitumike pesa ya sadaka tuliyotoa muda huu?

Ina maana mchungaji ana amini kila muumini anayekuja kanisani lazima abebe pesa ya sadaka na nyingine ya ziada?

Huwezi amini yule mtoto baada ya mchango kwenye kanisa lenye misa mbili na idadi ya watu zaidi ya 200 alipokea 30,000 tu
 
upumbavu huooo
wajinga ndyo waliwao, kwanini hao watoa mafuta ya upako wasijikusanye waende kuwamwagia wagonjwa mahospitalin ili tushuhudie izo nguvu za Mungu wao akiwatibu wagonjwa sirius[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

waafrika ban, sjui nan alie waloga kuamin maupumbav kama hayo, hao watumish na manabii ni aina za waganga wa kishirikina, tofauti yao na wale waganga wa vilingeni ni aina ya ofisi, mavazi na ushawishi wa masterplan wao yaan anaetoa nguvu za kuponya,

mponyaji anaetumiwa na waganga ni yule yule anaetumiaa na hao wachungaji wote haijarish anaomba kwa damu ya yesu na majina ya ajabu ajabu, nguvu ni zile zile tu, yaan shetani.


Hakuna anaemuabudu Muumba wakwel makanisani nyakati hizi, hayupoo na wachungaji woote waongo.

acheni kutapeliwa jmn mtadanganywa mpka ln?
 
Mkuu umeongea kwa ukali saana, kulikoni! Fahamu ya kua wapo watumishi wa Mungu walio wa kweli na wasio wa kweli na hili limeandikwa hata katika biblia na jambo la zana za upako kama mafuta na maji lina mjadala mpana saana kama wewe ni msomaji wa Biblia. Hata RC yenyewe wanatumia maji na wanatumia mafuta pia, kwenye Biblia mfalme Daudi alipakwa mafuta na pia Yohane mbatizaji aliwabatiza watu kwa maji. Sijui pana siri gani katila utumizi wa maji na mafuta ktk imani yetu ya Kikristo na japokua ninaliamini zaidi jina la Yesu kuliko zana hizo lakini bado nahitaji kujifunza zaidi. Kuhusu suala la kwenda mahospitalini na kushusha uponyaji for free, unapaswa uelewe ya kua uponyaji na miujiza katika Ukristo siyo suala la kufananishwa na mazingaombwe kabiisaaa, uponyaji na miujiza hutendeka kadiri Mungu atakavyo yeye kwa wasiomuamini ili waone nguvu zake wamuamini. Kwa hiyo unapewa kwanza habari za Yesu na ukiwa huamini au ili kukuza imani yako ndipo sasa unapata miujiza au uponyaji ili uamini kua uambiayo yana nguvu za Mungu. Kwa hiyo suala la mtumishi wa Mungu kwenda tuu hospitali na kuanza kuombea watu randomly wapone wote hiyo itakua ni mazingaombwe sasa maana suala la uponyaji na miujiza lina process za kupewa habari za Yesu kwanza. Hata kipindi kile Yesu angeweza kusema tuu, nchi hii watu wote wapone lakini haikua hivyo bali ilimpasa kila mtu achukue hatua kivyake ili apate uponyaji na muujiza..kumbuka yule mwanamke alievuja damu alivodhamiria na pia yule jamaa kipofu Batimayo aliemuita Yesu akihitaji kuona. Japo pia muujiza waweza kukufuata umekaa maana Mungu hutenda atakavyo.
 
Hii ya Sasa ni biashara
 
Nenda Aga khan kawaambie wagonjwa wote hiko kitu. Unadhani wao hawamjui Mungu?
Mungu hataki wazembe wasiotaka kumtafuta, hao wagonjwa wa Aga Khan wengine washasikia habari za Yesu lakini wengi wao hawajamtafuta na wanaumwa. Mungu anatoa muujiza na uponyaji akiona bidii yako na kinyume na hapo ni neema yake tuu ndiyo inatulinda. Mungu siyo wa kuchezesha mazingaombwe kama kwa watoto wa shule kubadili mchanga kua sukari, bali anataka wewe mwenyewe uchukue hatua vinginevyo ni neema yake tuu hutuponya maana atupenda kupita maelezo.
 
Naomba Picha ya majani ya kivumbasi Mkuu
 
Mkuu mbona hata katika biblia yote haya yameandikwa ya kua kutakua na watumishi wa uongo unastaajabu nini? Hii haimaanishi kua hawapo watumishi wa kweli wa Mungu, wapo! Kwa hiyo kuna wa uongo na wa kweli.
Na mara zote watumishi wa kweli hawafuatwagi na watu/waumini wengi maana wao hawahubiri hizi miujiza mafanikio pesa kujazwa so hayo watu hawataki siku hz.
 
Haiwezekani baada ya miaka 60 ya Uhuru Leo ndio unamletea mwananchi mlipa kodi Huduma ya maji, daraja na elimu tena kwa mbwembwe. Inapaswa mpigwe makofi na sio kupigiwa makofi.
Halafu 2025 unaombwa kura kwa ubwabwa na tishet
Unazungumzia nn
 
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wote matapeli tu

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Nachojua Mimi dunia ilivyo nzuri na yakutisha haiwezi tu kua imetokea from no where.

Aliyeumba dunia na vyote vilivyomo nitamtambua ndiye MUNGU.

Anisaidie tu kushinda dhambi nije nimuone mbinguni

Hizo habari za maji ya upako Sina uhakika nazo , hivyo siwezi coment
 
Kama huyi Mwamposa ni mponyaji kwa nini haendi mahospitalini wagonjwa wapo kibao wa kuponywa.
Unafikiri hata kipindi kile Yesu alikua anaenda vijiji na kutamka tuu hayaa kijiji hiki wagonjwa wote wapone!? Hapana mkuu kanuni ya imani yetu ya Kikristo haiko hivyo, ilibidi watu wamtafute Yesu ama wale alowafuata yeye mwenyewe wamkiri mioyoni mwao. Mungu anapenda kila mtu akate shauri kivyake na adhamirie kutoka moyoni kumtafuta ndipo ataweza kuona hiyo miujiza na uponyaji. Alieko hospitalini amtafute Mungu moyoni mwake kwa maana huko siyo eneo la mikutano ya injili kwamba wahubiriwe wapate miujiza. Kwa maana miujiza pasipo kuhubiriwa na kukata shauri ni mazingaombwe au neema. There is a thin line between mazingaombwe na ishara na miujiza, maajabu yasipomuhusisha Mungu wa ukweli popote hua ni mazingaombwe. Siyasemi haya kumtetea Mwamposa kwa maana Mungu ndiye atahukumu siku ya mwisho na pia zana za upako kama maji na chumvi bado sijazielewa lakini nitajifunza zaidi.
 
Sasa baada ya kuhubiriwa watu wanaingiwa na pepo na kukanyagana wakigombea mafuta, hadi watu 20 kufa!!!!
Hujanipata hapo bro!
 
Yy
 
Huyu jamaa miujiza kweli inatendeka Ila sijui inatoka wapi ,nilimpinga sana dingi kwenda huko Ila alinikalisha akanieleza yaliyojiri baada ya kwenda huko,Ila Bado sijajua source ya nguvu zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…