Kuna ukweli kuwa mwanaume na mwanamke wenye damu zenye chaji tofauti +ve na -ve hawawezi kupata mtoto?

Kuna ukweli kuwa mwanaume na mwanamke wenye damu zenye chaji tofauti +ve na -ve hawawezi kupata mtoto?

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Leo nimemsikia Mkuu wa kitengo cha damu salama wa hospitali moja ya serikali Dar es Salaam akisema ikiwa mwanaume ana damu +ve na mwanamke ana damu -ve (au vinginevyo) hawawezi kupata mtoto na kama wakipata mtoto atazaliwa akiwa na matatizo makubwa ya kiafya.

Hivyo ameshauri kabla ya kuoana ni vema kupima damu ili kuepusha tatizo la kutopata watoto.

Je, kuna ukweli wo wote kuhusu hoja hii? Binafsi nimeona watu wakipata watoto kutoka kwa wenza tofauti tofauti bila matatizo, je huu ni ugunduzi mpya?

====
Pia soma: Ijue Rhesus factor na ujauzito
 
Ndio mkuu, Rhesus incompatibility. Nitakuja kueleza kwa mapana zaidi
Kwa kuwa hizi complications siyo nyingi kihivyo ina maana wengi wanapata right partners, je kuna natural power ambayo inaepusha watu wengi kutopata matatizo haya?

Please ongezea na hoja hii kama una idea
 
Mwanamme akiwa na + na mwanamke ana - kupata mtoto wa kwanza uwezekano upo ila baada ya hapo wasahau aidha mimba kuharibika ikifika miezi mitatu au mtoto kuzaliwa tu na kufariki.
Mimi nina positive na wife ana negative kila mimba ikifika miezi saba mke anachoma chanjo inayoitwa ANT-D INJECTION. Gharama yake ni kuanzia laki moja na nusu hadi laki mbili kutegemeana na eneo lako lakin hizi injection kuna ambazo zinauzwa hadi laki tatu na anachoma mbili.
Ya kwanza ni mimba ikifikisha miezi saba na ya pili ni masaa 72 baada ya kujifungua.
Kwani bila kufanya hivyo sahau kuhusu kuwa na familia.
 
Hii kitu ipo kweli kabisa na kama ikiwakuta na hamuelewi kwa mapana yake,mnaweza hisi mmelogwa kutokana na series ya miscarriage.
Na mara nyingine husababisha wakina mama kuchepuka na kuzaa nje ya ndoa ,baada ya kuchoka kusemwa sana hususani na ndugu wa kiumeni kuhusu tatizo la mimba kutoka au kutozaa Kwa muda mrefu.
 
Wanapata isipokuwa kwa mama akiwa ni negative ndiyo italeta shida au kukosa kabisa mtoto.

Kwanza rhesus ni protein iliyo kwenye damu.
Wote wenye hiyo protein ndio hao wanaitwa rhesus positive.
Wasiyonayo wanaitwa rhesus negative.

Shida ni pale ambapo mama atakuwa na damu yenye rhesus negative( hana rhesus protein) halafu Baba awe ni rhesus positive(ana rhesus protein)

Maanake mtoto akitengezwa tumboni halafu akarithi rhesus positive ya baba.( akawa nae ana rhesus protein)

Mwili wa mama utarecognize kama kitu kigeni hivyo utatengeneza ulinzi wa kushambulia damu ya mtoto atakaefuata mwenye rhesus positive.
 
DR Mambo Jambo shule ya rhesus incompatibility utupatie tafadhali, haha
Ni shule ndefu sana..!
Kifupi Kabla hujaoa Unatakiwa Kupima Damu na Bila kusahau Group la Damu na Rh kwa nyote wewe na mwenza wako ili mpange jinsi mtakavyopata watoto maana Watoto/Mama wajawazito wengi wanapata Matatizo kwa kutokujua au Negligence ya Vipimo hivi muhimu..

Na kwa Ushauri wengi nimeona Wanaogopa Rh Incompatibility ila Siku hizi naona zimwi linaitwa ABO incompitibility Ndo linatake over sana, Kila wagonjwa (Watoto wadogo) 60 kati ya 100 wenye HDN (Haemolytic disease of the newborn) Wanakuwa wana ABO incompa...na 40 ambao Ni severe cases wana Rh inco..

Hii kitu ni hatari sana ukiikuta kwenye severe cese
 
Mkuu shukrani, acha nipitie kwenye ABO incompatibility.
 
Back
Top Bottom