Kuna ukweli wowote kwamba kazi za IT / Computer serikalini wana muda mwingi sana wa kupumzika bila kazi ?

nguvu ya buku

Senior Member
Joined
Jul 15, 2025
Posts
168
Reaction score
549
Mfano niliwahi kusikia system administrator wa Chuo kazi yake kwa kiasi kikubwa ni kuangalia tu system haina matatizo (Monitoring), Anapata muda mwingi wa kupumzika, anawahi kuondoka na mshahara mzuri.

Yani wakishaseti Server, Database na Network kinachobaki huwa ni kutazama kila kitu kinaenda sawa, mfumo mzima umeshasetiwa unajiendesha.

Siku ambayo kazi inakuwa ngumu sana ni pale ambapo mtandao umeharibika, hakuna huduma kwa watumiaji, server zimekorofisha, wadukuaji wameingia kwenye mfumo, au kuna virusi. Hapo ni kazi ngumu sana, na inakuwa hakuna kupumzika kwa sababu kila kitu kinahitaji kutatuliwa haraka.
 
Mfano niliwahi kusikia system administrator wa Chuo kazi yake kwa kiasi kikubwa ni kuangalia tu system haina matatizo (Monitoring), Anapata muda mwingi wa kupumzika, anawahi kuondoka na mshahara mzuri.
Serikalini hua tunaingia saa mbili kamili, tunasubiri wafanye usafi mpaka saa tatu. Wakimaliza usafi tunaingia ofisini, tunaweka koti kwenye kiti na begi, then tunaenda kwenye chai. Tunarudi saa tano na nusu kucheki kama kuna lolote then tunatoka saa sita kamili kwenda lunch mpaka saa nane. Nane na nusu tunarudi ofisini kufunga funga, tisa kamili tunatoka.
 
Weeee! Jidanganye na ujichanganye mdogo wangu.
Ni kwa moto naweza kukupa na mifano
Ndio uweke ushahidi, kuna jamaa kaniambia wakishaseti Mitambo kitu wanachofanya huwa ni kuangalia tu (Monitoring) na kufanya maintance mara chache

Achana na wale IT ambao huwa tunawaita kila mara watusetie mausi, watuwashie printer, n.k.
 
Mfano niliwahi kusikia system administrator wa Chuo kazi yake kwa kiasi kikubwa ni kuangalia tu system haina matatizo (Monitoring), Anapata muda mwingi wa kupumzika, anawahi kuondoka na mshahara mzuri.
Wewe kazi ya monitoring na maintanance unaiona ndogo?
 
Inategemeana na huduma ambazo Ofisi husika inatoa.kuna baadhi ya Ofisi hazina majukumu mengi na shughuli zao sio automated kihivyo.
 
Mfano niliwahi kusikia system administrator wa Chuo kazi yake kwa kiasi kikubwa ni kuangalia tu system haina matatizo (Monitoring), Anapata muda mwingi wa kupumzika, anawahi kuondoka na mshahara mzuri.
Systems ni term ya ujumla. Ukubwa wa kazi ya za systems administrator hutegemea na system mahususi anayoisimamia, maana inaweza ikawa inatoa huduma kwa watu wengi au wachache.

Mfano, unasimamia network system ya chuo yenye watumiaji wengi, ofisi/vyumba kama 100 hivi plus computer labs. Possibility ya kuwa busy ni kubwa ukilinganisha na anayesimamia web based system ya kufundishia, tena iliyopo kwenye server mliyoiweka kwa Service provider fulani nje ya taasisi yenu.
 
Serikalini hua tunaingia saa mbili kamili, tunasubiri wafanye usafi mpaka saa tatu. Wakimaliza usafi tunaingia ofisini, tunaweka koti kwenye kiti na begi, then tunaenda kwenye chai. Tunarudi saa tano na nusu kucheki kama kuna lolote then tunatoka saa sita kamili kwenda lunch mpaka saa nane. Nane na nusu tunarudi ofisini kufunga funga, tisa kamili tunatoka.
Ila cku mfumo ukikorofisha nasikia mnashindwa kurekebisha hadi wakorea waingilie kati
 
Serikalini hua tunaingia saa mbili kamili, tunasubiri wafanye usafi mpaka saa tatu. Wakimaliza usafi tunaingia ofisini, tunaweka koti kwenye kiti na begi, then tunaenda kwenye chai. Tunarudi saa tano na nusu kucheki kama kuna lolote then tunatoka saa sita kamili kwenda lunch mpaka saa nane. Nane na nusu tunarudi ofisini kufunga funga, tisa kamili tunatoka.
Halafu huwa mnajipimia speed kubwa sana ya internet 😂

Kuna kijana yupo idara ya IT niliwahi kutumia laptop yake, speed ni kubwa kuliko watumiaji wengine
 
Ndio uweke ushahidi, kuna jamaa kaniambia wakishaseti Mitambo kitu wanachofanya huwa ni kuangalia tu (Monitoring) na kufanya maintance mara chache

Achana na wale IT ambao huwa tunawaita kila mara watusetie mausi, watuwashie printer, n.k.
Inategemea na serikal branch gani, shirika gani.

Kunashirika sito litaja, wale jamaa ni kama private sector, IT mle hawapumziki ni kazi kazi. Ila sababu ya demand ya kazi yao
 
Serikalini hua tunaingia saa mbili kamili, tunasubiri wafanye usafi mpaka saa tatu. Wakimaliza usafi tunaingia ofisini, tunaweka koti kwenye kiti na begi, then tunaenda kwenye chai. Tunarudi saa tano na nusu kucheki kama kuna lolote then tunatoka saa sita kamili kwenda lunch mpaka saa nane. Nane na nusu tunarudi ofisini kufunga funga, tisa kamili tunatoka.
😄😄😄
Kuna ukweli fulani hapa. Niliwahi kufanya kazi kwenye programme moja iliokuwa na ushirika wa serikali na donor agency ya nchi fulani,nikiwa mtu wa IT.

Yule mwenzangu wa upande wa serikalini kwakweli alikuwa anakula shushu la kutosha maana kati ya mara kumi alizohitajika kuwa ofisini basi ni mara mbili utampata.

Na mara nane iliyobaki alikuwa nje ya ofisi kwa masuala binafsi.
 
Binafsi naingia kazini moja kamili, natest upatikanaji wa mawasiliano (server room), km Kuna changamoto nafix chap, then nasubiri staffs wengine waingie Kwa ofisi zao nazunguka kuona km printer/scanner na internet/network Iko okay. Mpaka kufikia saa nne au tano nakuwa nishamaliza kazi nasepa naenda hospital au kituo Cha afya Cha karibu nazuga kuchek connections za mifumo yao then by saa sita nasepa kitaa kuendelea na utawala binafsi.
 
CONFIGURATION UNAITA CONSULTANT
 
Sio kweli.
IT huwa wanashiriki vikao mbalimbali iwe ni administration, operations, n.k
Pia kuna seminars na training,
Pia wanasoma sana technology inabalibalika na siku hizi kila mahali Kuna technology iwe ni mfumo, network, n.k.
Kusema hawafanyi kazi na kila siku wewe unafanya kazi zako zote kupitia miundo mbinu ya IT.
Iwe ni malipo ya fedha, inventory, database, n.k.
Mfano mfumo ukizingua ofisi nzima inakuwa hamna cha kufanya zaidi ya IT yeye ndio ana-run ofisi nzima na kujua jinsi mfumo unafanya kazi, LAN ilivyo hiyo siyo kitu cha siku moja au mbili, kuleta tu mtu yoyote tu aguseguse,
Hivyo IT ni critical person kwenye ofisi anabeba past and future nzima ya ofisi..
Tafuta job description zao ?

jaribu kulipia mtu awe anacheki kukiwa na tatizo tu au uajiri IT ipi ghali?
 
Serikalini hua tunaingia saa mbili kamili, tunasubiri wafanye usafi mpaka saa tatu. Wakimaliza usafi tunaingia ofisini, tunaweka koti kwenye kiti na begi, then tunaenda kwenye chai. Tunarudi saa tano na nusu kucheki kama kuna lolote then tunatoka saa sita kamili kwenda lunch mpaka saa nane.
Nimecheka kifala sana
Nane na nusu tunarudi ofisini kufunga funga, tisa kamili tunatoka.
Baada ya kundoka ofisini tunapita Bup tuanapiga moja moto moja baridi na kiti moto.. saa tatu, nne usiku tunarudi nyumbani kulala.......kesho tena kama jana..
 
Back
Top Bottom