Kuna ukweli wowote kwamba kazi za IT / Computer serikalini wana muda mwingi sana wa kupumzika bila kazi ?

Kuna ukweli wowote kwamba kazi za IT / Computer serikalini wana muda mwingi sana wa kupumzika bila kazi ?

Mfano niliwahi kusikia system administrator wa Chuo kazi yake kwa kiasi kikubwa ni kuangalia tu system haina matatizo (Monitoring), Anapata muda mwingi wa kupumzika, anawahi kuondoka na mshahara mzuri.

Yani wakishaseti Server, Database na Network kinachobaki huwa ni kutazama kila kitu kinaenda sawa, mfumo mzima umeshasetiwa unajiendesha.

Siku ambayo kazi inakuwa ngumu sana ni pale ambapo mtandao umeharibika, hakuna huduma kwa watumiaji, server zimekorofisha, wadukuaji wameingia kwenye mfumo, au kuna virusi. Hapo ni kazi ngumu sana, na inakuwa hakuna kupumzika kwa sababu kila kitu kinahitaji kutatuliwa haraka.
Ulivyo mpumbavu bila ht haya unafikiria kazi za uvivu, kwa huo uvivu hiyo IT hautaweza kuisoma
 
Sio kweli.
IT huwa wanashiriki vikao mbalimbali iwe ni administration, operations, n.k
Pia kuna seminars na training,
Pia wanasoma sana technology inabalibalika na siku hizi kila mahali Kuna technology iwe ni mfumo, network, n.k.
Kusema hawafanyi kazi na kila siku wewe unafanya kazi zako zote kupitia miundo mbinu ya IT.
Iwe ni malipo ya fedha, inventory, database, n.k.
Mfano mfumo ukizingua ofisi nzima inakuwa hamna cha kufanya zaidi ya IT yeye ndio ana-run ofisi nzima na kujua jinsi mfumo unafanya kazi, LAN ilivyo hiyo siyo kitu cha siku moja au mbili, kuleta tu mtu yoyote tu aguseguse,
Hivyo IT ni critical person kwenye ofisi anabeba past and future nzima ya ofisi..
Tafuta job description zao ?

jaribu kulipia mtu awe anacheki kukiwa na tatizo tu au uajiri IT ipi ghali?
IT wa wapi hao wanasoma sana, Bongo ? 😂

Maofisini kwenyewe hadi leo kuna windows 7, shangaa !

Mfumo ukizingua huwa hapalaliki lakini mfumo ukirudi huwa ni kuuangalia na maintanance kidogo
 
Upo sahihi Serikali kuna mambo yanachekesha sana mkuu Mimi nimewahi kumaliza miezi sita siendi kazini nilikuwa napiga simu tu
 
IT wa wapi hao wanasoma sana, Bongo ? 😂

Maofisini kwenyewe hadi leo kuna windows 7, shangaa !

Mfumo ukizingua huwa hapalaliki lakini mfumo ukirudi huwa ni kuuangalia na maintanance kidogo
Shida yako inaonekana una roho ya kwanini

Mbona wewe hukusoma IT?

By the way kwenye maisha siyo nguvu huwa zinalipa Bali akili
Unaweza fanya kazi asubuhi mpaka jioni kwa nguvu ila Kuna mtu anafanya kazi ya akili nusu saa kwa siku na akakupiga mbali mno
 
CONFIGURATION UNAITA CONSULTANT
Consultant analipwa na nani? Kama analipwa na serikali basi ujue huo ni utaratibu rasmi, maana serikali haiwezi kulipa hela zisizokuwa supported na maelezo rasmi
 
Mfano niliwahi kusikia system administrator wa Chuo kazi yake kwa kiasi kikubwa ni kuangalia tu system haina matatizo (Monitoring),
Huko ulikisikia ungeuliza pia, Je, system ikiwa na matatizo? Ukisikia uje uongezee nyama kwenye uzi wako
 
Mfano niliwahi kusikia system administrator wa Chuo kazi yake kwa kiasi kikubwa ni kuangalia tu system haina matatizo (Monitoring), Anapata muda mwingi wa kupumzika, anawahi kuondoka na mshahara mzuri.

Yani wakishaseti Server, Database na Network kinachobaki huwa ni kutazama kila kitu kinaenda sawa, mfumo mzima umeshasetiwa unajiendesha.

Siku ambayo kazi inakuwa ngumu sana ni pale ambapo mtandao umeharibika, hakuna huduma kwa watumiaji, server zimekorofisha, wadukuaji wameingia kwenye mfumo, au kuna virusi. Hapo ni kazi ngumu sana, na inakuwa hakuna kupumzika kwa sababu kila kitu kinahitaji kutatuliwa haraka.
Kwamba administrator wa GePG, Tanesco, TRA, etc huyo ndiyo anakula shushu!!
 
Back
Top Bottom