Mfano....Wangefanya JKT iwe mandatory kwa wanaume tu kama nchi nyingi za Ulaya. Kwa wanawake iwe hiyari. Sababu huko kuna changamoto nyingi ambazo siyo rafiki kwa wasichana.
daah, yaniHata wiki haijaisha tokea Wanafunzi wa A- level wamalize mitihani, JKT washakuja na orodha yao. Haya ni maumivu na stress tupu kwa vijana hata muda wa ku relax baada ya kumaliza masomo hakuna?
Hujui kama hujuiJKT kupoteza muda tu na kutesa vijana wetu wameshachoka na mitihani hata hawajapumzika waend tena kulima huko na kukimbiakimbia, hao wa kujitolea tu hawawaajiri wanazeekea makambini na kurejea mitaani.
Binafsi sioni faida ya kwenda huko, labda kama una ndoto na jeshi unaweza kwenda ukapata connection otherwise piga chini, chuo utaenda tu.
Nakazia hoja 100%.Watoto wa sasa hivi ni lonyolonyo sana, nashauri mbunge litunge sheria iwe ni lazima kwenda JKT.
Kiukweli mnatusikitisha sana Toto lipo high school bado linasimamiwa na wazazi hawezi hata kujisimamia.
Kizazi hiki bila kukipitisha jeshini tunaandaa msiba mkubwa kwa Taifa.
Mkuu, Wewe alipitia mafunzo hayo? Unataka vijana wa-relax kweli kwa hali tunayokwenda nayo sasa?Hata wiki haijaisha tokea Wanafunzi wa A- level wamalize mitihani, JKT washakuja na orodha yao. Haya ni maumivu na stress tupu kwa vijana hata muda wa ku relax baada ya kumaliza masomo hakuna?
Aisee! We unaweza kuwa ni mtu hatari sana unataka kulea vijana kama mayai. Kumbuka wahenga walisema "Kijana ni maji ya moto lakini hayachomi nyumba" tena wakasema "samaki mkunje akingali mbichi"JKT kupoteza muda tu na kutesa vijana wetu wameshachoka na mitihani hata hawajapumzika waend tena kulima huko na kukimbiakimbia, hao wa kujitolea tu hawawaajiri wanazeekea makambini na kurejea mitaani.
Binafsi sioni faida ya kwenda huko, labda kama una ndoto na jeshi unaweza kwenda ukapata connection otherwise piga chini, chuo utaenda tu.
Wanafunzi ni wengi kuliko idadi ya kambi zilizopo ndo maana hawaangaiki kabisa.JKT wangekuwa hawachoki kila mara kuwaelimisha Vijana sababu, faida na madhara ya kujiiunga au kukataa kujiunga na taasisi yao. Lakini naona kipaumbele chao ni kutangaza orodha tu kila mwaka kwa wanafunzi wanaotakiwa kuripoti kambini bila ya kufafanua kwanini, kwa sheria zipi, manufaa yapi na madhara yapi wakiripoti au wasiporipoti kambini. Kuweka tu orodha ya Wanafunzi na vitu wanavyotakiwa kuwa navyo wakati wana ripoti kambini bila ya kuwafahamisha kwa nini waripoti ni dharau.
Utambue wanaohitajika kuripoti JKT ni kutoka bara tu, huko kungine wanakula bata kusubiri ajira zaoHabari zenu Wana JF,
Naomba msaada kufahamu madhara ya kuacha kuripoti wito wa kujiunga na JKT kwa wale waliomaliza A level.
Je, cheti cha kumaliza mafunzo ya JKT huwa kinahitajika kwa ambaye anataka kufanya maombi vyuo vikuu vya Serikali kama UDSM, Tanzania Institute of Accountancy na IFM, kwa mfano?
Lakini la ziada: kama mhusika hatafanya maombi ya mkopo kupitia HESLB ataathirika namna gani?
Asanteni kwa msaada.
Mkuu, Sio dharau ila sababu, faida na madhara ya kujiunga au kukataa kujiunga na Taasisi, yao hao vijana wataenda kuyajua huko mbele kwa mbele.JKT wangekuwa hawachoki kila mara kuwaelimisha Vijana sababu, faida na madhara ya kujiiunga au kukataa kujiunga na taasisi yao. Lakini naona kipaumbele chao ni kutangaza orodha tu kila mwaka kwa wanafunzi wanaotakiwa kuripoti kambini bila ya kufafanua kwanini, kwa sheria zipi, manufaa yapi na madhara yapi wakiripoti au wasiporipoti kambini. Kuweka tu orodha ya Wanafunzi na vitu wanavyotakiwa kuwa navyo wakati wana ripoti kambini bila ya kuwafahamisha kwa nini waripoti ni dharau.
Huko Visiwani vipiMkuu, Sio dharau ila sababu, faida na madhara ya kujiunga au kukataa kujiunga na Taasisi, yao hao vijana wataenda kuyajua huko mbele kwa mbele.
Aidha kijana anatakiwa kujiandaa kwa hali zote za Heri na Shari sio anakaa tu kulemaa-lemaa hapo mtaani kazi ni kulalamika kila siku na kujishaua eti amesoma hadi form six. Akienda jeshini atashangaa anawakuta wenzake maafande wamesoma hadi form seveni na ndo watakaomhenyesha.
Exactly. Safi sana hii comment yako. Mimi nimepitia JKT ile ya mwaka mmoja na hayo ulioyasema ni mubashara kabisa. Ukitaka kuhakikisha we jisahau halafu uweke SMG hapo au RPG au handgrenade 56 -Kitaeleweka.Kama mwanao hana kazi ya muhimu anayofanya hapo nyumbani ni heri aende jkt, usiweke matarajio kua akienda jkt ndio atapata ajira, hapana.
Sema itamsaidia kuona maisha kwa namna tofauti, mimi nilivomaliza kidato cha sita wazazi wangu walinikomalia niende jkt, Na kweli nilienda na nimejifunza mengi nimekutana na watu wengi, tumelima sana, kufyatua matofali,kuchoma mkaa kupanda miche ya maparachichi,kwata,kua mkakamavu na mvumilivu, imenifundisha kidogo kuhusu silaha leo nina abc zake,kubwa kabisa imetengenezea mtandao mkubwa sana nimepata marafiki wengi,
Haya mambo yote nisingeyajua kama nisingeenda ningeishia kucheza magame kwenye ps nyumbani na kufukuzia mahousegirl.Kwa sababu sikua na kazi yoyote ya kufanya mda huo zaidi ya kula ugali wa baba.
Kila mmoja anatakiwa ashinde mechi zake. Huko kuna JKU.Huko Visiwani vipi
Yaani eti hiyo hapo ndiyo tovuti ya jeshi letu na pengine ina wasomi kabisa wa IT. Mtu akitaka kujua kambi aliyopangiwa mtoto li website lao halifunguki kabisa au linafunguka kwa kuonyesha majina ya baadhi tu ya vijana toka juzi walipodai wameweka majina yote kwenye website. Bure kabisa.Hebu mwenye kufahamu tovuti ya JKT yenye kuonyesha majina ya waloitwa Jeshini,maana hii ya www.jkt.go.tz haipatikani,au siyo ya jeshi la kujenga taifa ?