Kuna umuhimu wa kuripoti JKT kwa wahitimu wa Form 6?

Kuna umuhimu wa kuripoti JKT kwa wahitimu wa Form 6?

Cheti cha JKT kitakusadia kama utataka kazi ya Ulinzi na wako vijana wengi wameishia JKT tu hawajasoma na wamepata ajiri za ulinzi na wanaendesha maisha yao.

Ila kama unapitia JKT baada ya Form 6 kabla ya kwenda Chuo Kikuu, sioni kabisa maana yake, haina msaada wowote.
 
Hata wiki haijaisha tokea Wanafunzi wa A- level wamalize mitihani, JKT washakuja na orodha yao. Haya ni maumivu na stress tupu kwa vijana hata muda wa ku relax baada ya kumaliza masomo hakuna?
daah, yani
 
JKT kupoteza muda tu na kutesa vijana wetu wameshachoka na mitihani hata hawajapumzika waend tena kulima huko na kukimbiakimbia, hao wa kujitolea tu hawawaajiri wanazeekea makambini na kurejea mitaani.
Binafsi sioni faida ya kwenda huko, labda kama una ndoto na jeshi unaweza kwenda ukapata connection otherwise piga chini, chuo utaenda tu.
Hujui kama hujui
 
Watoto wa sasa hivi ni lonyolonyo sana, nashauri mbunge litunge sheria iwe ni lazima kwenda JKT.

Kiukweli mnatusikitisha sana Toto lipo high school bado linasimamiwa na wazazi hawezi hata kujisimamia.

Kizazi hiki bila kukipitisha jeshini tunaandaa msiba mkubwa kwa Taifa.
Nakazia hoja 100%.
Ewe kijana, kama utabahatika kupitia uzi huu nakushauri NENDA Karipoti JKT.
Manufaa ya kupitia Jeshini hayako wazi kivile na ndo maana wapo wachangiaji hapa wanasema(wanadai) ni kupoteza muda. Sio kupoteza muda hata kidogo.
Hebu fikiria ww kama kijana unatakiwa uwe jasiri, mvumilivu, ngangari, mbunifu, mwenye kuthubutu na mwenye kujisimamia - Kule JKT hayo utayapata na utakuja kugundua hilo baadaye utakapokuwa tayari umeshamaliza Jeshi na uko mitaani au kwenye ajira binafsi au kwenye Mashirika yasiyo ya kiserikali au hata Serikalini.
Usikubali ushauri wa hao ambao hawakupita huko na ndo hao Laini-laini(Nyoronyoro) anashindwa hata kutembea kwa miguu Km 3 eti ni mpaka apande boda.
 
Hata wiki haijaisha tokea Wanafunzi wa A- level wamalize mitihani, JKT washakuja na orodha yao. Haya ni maumivu na stress tupu kwa vijana hata muda wa ku relax baada ya kumaliza masomo hakuna?
Mkuu, Wewe alipitia mafunzo hayo? Unataka vijana wa-relax kweli kwa hali tunayokwenda nayo sasa?
 
Acha waende wakajifunze uzalendo, wakajifunze na jinsi yakutumia pesa
 
JKT kupoteza muda tu na kutesa vijana wetu wameshachoka na mitihani hata hawajapumzika waend tena kulima huko na kukimbiakimbia, hao wa kujitolea tu hawawaajiri wanazeekea makambini na kurejea mitaani.
Binafsi sioni faida ya kwenda huko, labda kama una ndoto na jeshi unaweza kwenda ukapata connection otherwise piga chini, chuo utaenda tu.
Aisee! We unaweza kuwa ni mtu hatari sana unataka kulea vijana kama mayai. Kumbuka wahenga walisema "Kijana ni maji ya moto lakini hayachomi nyumba" tena wakasema "samaki mkunje akingali mbichi"
Umeona kijana wako eti anaenda kuteswa?? amechoka na mitihani??? wanaenda kulima na kukimbiakimbia?? Yaani Hutaki kijana wako achangamke, ajue kujipambania maisha na uhai wake, akutane na vijana wenzake wamkaramshe(Wamwondoe ulofaulofa) ajifunze kutii amri na pia kufanya maamuzi binafsi n.k. Sasa wewe umeamua kijana wako unamrembaremba na kumpetipeti hapo nyumbani? Majuto ni mjukuu. Nimemaliza.
 
JKT wangekuwa hawachoki kila mara kuwaelimisha Vijana sababu, faida na madhara ya kujiiunga au kukataa kujiunga na taasisi yao. Lakini naona kipaumbele chao ni kutangaza orodha tu kila mwaka kwa wanafunzi wanaotakiwa kuripoti kambini bila ya kufafanua kwanini, kwa sheria zipi, manufaa yapi na madhara yapi wakiripoti au wasiporipoti kambini. Kuweka tu orodha ya Wanafunzi na vitu wanavyotakiwa kuwa navyo wakati wana ripoti kambini bila ya kuwafahamisha kwa nini waripoti ni dharau.
Wanafunzi ni wengi kuliko idadi ya kambi zilizopo ndo maana hawaangaiki kabisa.
 
Kama mwanao hana kazi ya muhimu anayofanya hapo nyumbani ni heri aende jkt, usiweke matarajio kua akienda jkt ndio atapata ajira, hapana.
Sema itamsaidia kuona maisha kwa namna tofauti, mimi nilivomaliza kidato cha sita wazazi wangu walinikomalia niende jkt, Na kweli nilienda na nimejifunza mengi nimekutana na watu wengi, tumelima sana, kufyatua matofali,kuchoma mkaa kupanda miche ya maparachichi,kwata,kua mkakamavu na mvumilivu, imenifundisha kidogo kuhusu silaha leo nina abc zake,kubwa kabisa imetengenezea mtandao mkubwa sana nimepata marafiki wengi,
Haya mambo yote nisingeyajua kama nisingeenda ningeishia kucheza magame kwenye ps nyumbani na kufukuzia mahousegirl.Kwa sababu sikua na kazi yoyote ya kufanya mda huo zaidi ya kula ugali wa baba.
 
Habari zenu Wana JF,

Naomba msaada kufahamu madhara ya kuacha kuripoti wito wa kujiunga na JKT kwa wale waliomaliza A level.

Je, cheti cha kumaliza mafunzo ya JKT huwa kinahitajika kwa ambaye anataka kufanya maombi vyuo vikuu vya Serikali kama UDSM, Tanzania Institute of Accountancy na IFM, kwa mfano?

Lakini la ziada: kama mhusika hatafanya maombi ya mkopo kupitia HESLB ataathirika namna gani?

Asanteni kwa msaada.
Utambue wanaohitajika kuripoti JKT ni kutoka bara tu, huko kungine wanakula bata kusubiri ajira zao
 
JKT wangekuwa hawachoki kila mara kuwaelimisha Vijana sababu, faida na madhara ya kujiiunga au kukataa kujiunga na taasisi yao. Lakini naona kipaumbele chao ni kutangaza orodha tu kila mwaka kwa wanafunzi wanaotakiwa kuripoti kambini bila ya kufafanua kwanini, kwa sheria zipi, manufaa yapi na madhara yapi wakiripoti au wasiporipoti kambini. Kuweka tu orodha ya Wanafunzi na vitu wanavyotakiwa kuwa navyo wakati wana ripoti kambini bila ya kuwafahamisha kwa nini waripoti ni dharau.
Mkuu, Sio dharau ila sababu, faida na madhara ya kujiunga au kukataa kujiunga na Taasisi, yao hao vijana wataenda kuyajua huko mbele kwa mbele.
Aidha kijana anatakiwa kujiandaa kwa hali zote za Heri na Shari sio anakaa tu kulemaa-lemaa hapo mtaani kazi ni kulalamika kila siku na kujishaua eti amesoma hadi form six. Akienda jeshini atashangaa anawakuta wenzake maafande wamesoma hadi form seveni na ndo watakaomhenyesha.
 
Hebu mwenye kufahamu tovuti ya JKT yenye kuonyesha majina ya waloitwa Jeshini,maana hii ya www.jkt.go.tz haipatikani,au siyo ya jeshi la kujenga taifa ?
 
Huko Visiwani vipi
 
Kama mwanao hana kazi ya muhimu anayofanya hapo nyumbani ni heri aende jkt, usiweke matarajio kua akienda jkt ndio atapata ajira, hapana.
Sema itamsaidia kuona maisha kwa namna tofauti, mimi nilivomaliza kidato cha sita wazazi wangu walinikomalia niende jkt, Na kweli nilienda na nimejifunza mengi nimekutana na watu wengi, tumelima sana, kufyatua matofali,kuchoma mkaa kupanda miche ya maparachichi,kwata,kua mkakamavu na mvumilivu, imenifundisha kidogo kuhusu silaha leo nina abc zake,kubwa kabisa imetengenezea mtandao mkubwa sana nimepata marafiki wengi,
Haya mambo yote nisingeyajua kama nisingeenda ningeishia kucheza magame kwenye ps nyumbani na kufukuzia mahousegirl.Kwa sababu sikua na kazi yoyote ya kufanya mda huo zaidi ya kula ugali wa baba.
Exactly. Safi sana hii comment yako. Mimi nimepitia JKT ile ya mwaka mmoja na hayo ulioyasema ni mubashara kabisa. Ukitaka kuhakikisha we jisahau halafu uweke SMG hapo au RPG au handgrenade 56 -Kitaeleweka.
 
Hebu mwenye kufahamu tovuti ya JKT yenye kuonyesha majina ya waloitwa Jeshini,maana hii ya www.jkt.go.tz haipatikani,au siyo ya jeshi la kujenga taifa ?
Yaani eti hiyo hapo ndiyo tovuti ya jeshi letu na pengine ina wasomi kabisa wa IT. Mtu akitaka kujua kambi aliyopangiwa mtoto li website lao halifunguki kabisa au linafunguka kwa kuonyesha majina ya baadhi tu ya vijana toka juzi walipodai wameweka majina yote kwenye website. Bure kabisa.
 
Hilo swali lako ni kama la saba anakuuliza kuna umuhimu gani kwenda sekondari? Au wewe form 6 ungemjibu nini form 4 akikuuliza umuhimu wa kufika form 6?
Hizi ni hatua muhimu za maisha..usipoenda utapoteza kitu na kuna mahali hutavuka. Ni wahindi na wachina tu hawatakuuliza kama hukupita jeshini. Kipimo cha uzalendo na ukakamavu ni mafunzo ya JKT.
WENGI MNAFELI INTERVIEW NA HAMJUI NINI KIMEWAANGUSHA. UNAPOONA HAKUNA AJIRA KWENYE MAJESHI YOTE KAMA HUJAPATA MAFUNZO YA AWALI JKT.
Utamaliza degree, utapatamani mahali na ukiingia chumba cha interview unakumbana na hilo swali......

Nendeni, ndo maana mnachapwa makofi na wasichana wenu.
 
Back
Top Bottom