Nakazia hoja 100%.
Ewe kijana, kama utabahatika kupitia uzi huu nakushauri NENDA Karipoti JKT.
Manufaa ya kupitia Jeshini hayako wazi kivile na ndo maana wapo wachangiaji hapa wanasema(wanadai) ni kupoteza muda. Sio kupoteza muda hata kidogo.
Hebu fikiria ww kama kijana unatakiwa uwe jasiri, mvumilivu, ngangari, mbunifu, mwenye kuthubutu na mwenye kujisimamia - Kule JKT hayo utayapata na utakuja kugundua hilo baadaye utakapokuwa tayari umeshamaliza Jeshi na uko mitaani au kwenye ajira binafsi au kwenye Mashirika yasiyo ya kiserikali au hata Serikalini.
Usikubali ushauri wa hao ambao hawakupita huko na ndo hao Laini-laini(Nyoronyoro) anashindwa hata kutembea kwa miguu Km 3 eti ni mpaka apande boda.