Hujamjibu swali lake, bali umetoa fikra zako.JKT kupoteza muda tu na kutesa vijana wetu wameshachoka na mitihani hata hawajapumzika waend tena kulima huko na kukimbiakimbia, hao wa kujitolea tu hawawaajiri wanazeekea makambini na kurejea mitaani.
Binafsi sioni faida ya kwenda huko, labda kama una ndoto na jeshi unaweza kwenda ukapata connection otherwise piga chini, chuo utaenda tu.
Wameshaanza kuomba pesa za kununulia simu, acha waende wakajifunze maisha sio kunenepeana na kujaza mashavu bila sababu, ngoja waende wakajifunze hata kutumia mabumu yao watakapoanza vyuoMkuu, Sio dharau ila sababu, faida na madhara ya kujiunga au kukataa kujiunga na Taasisi, yao hao vijana wataenda kuyajua huko mbele kwa mbele.
Aidha kijana anatakiwa kujiandaa kwa hali zote za Heri na Shari sio anakaa tu kulemaa-lemaa hapo mtaani kazi ni kulalamika kila siku na kujishaua eti amesoma hadi form six. Akienda jeshini atashangaa anawakuta wenzake maafande wamesoma hadi form seveni na ndo watakaomhenyesha.
Wewe ndiye umempa jibuHakuna madhara yeyote mkuu, mimi nilihitimu form VI 2020 na sikwenda jkt. Chuo nilijiunga [UDSM) na mkopo niliapply pasipo kuombwa cheti cha jkt
Mkuu tuache siasa tuseme ukweli, Kama hhna ndoto za kujiunga jeshi kwenda Jkt ni kupoteza muda.Aisee! We unaweza kuwa ni mtu hatari sana unataka kulea vijana kama mayai. Kumbuka wahenga walisema "Kijana ni maji ya moto lakini hayachomi nyumba" tena wakasema "samaki mkunje akingali mbichi"
Umeona kijana wako eti anaenda kuteswa?? amechoka na mitihani??? wanaenda kulima na kukimbiakimbia?? Yaani Hutaki kijana wako achangamke, ajue kujipambania maisha na uhai wake, akutane na vijana wenzake wamkaramshe(Wamwondoe ulofaulofa) ajifunze kutii amri na pia kufanya maamuzi binafsi n.k. Sasa wewe umeamua kijana wako unamrembaremba na kumpetipeti hapo nyumbani? Majuto ni mjukuu. Nimemaliza.
Kijana, nenda JKT.Habari zenu Wana JF,
Naomba msaada kufahamu madhara ya kuacha kuripoti wito wa kujiunga na JKT kwa wale waliomaliza A level.
Je, cheti cha kumaliza mafunzo ya JKT huwa kinahitajika kwa ambaye anataka kufanya maombi vyuo vikuu vya Serikali kama UDSM, Tanzania Institute of Accountancy na IFM, kwa mfano?
Lakini la ziada: kama mhusika hatafanya maombi ya mkopo kupitia HESLB ataathirika namna gani?
Asanteni kwa msaada.
Laki moja kwa hiyo miezi 3 wewe utafanyia nini?Kuna posho pia watapewa huko jeshini mkuu. Unatoka na mtaji wa biashara kabisa
Ulonyolonyo mmeuanzisha nyie wazazi wa sasa wa dotcom....hakuna wazazi vilaza kama nyie yaani ni jukumu la mwingine....halafu eti ndio muwapeleke JKT, kwa nini upeleke nyolo JKT kaa nalo mwenyewe...maanza enzi zetu hakukua na nyolo kama hawa wenu ambao mnawalea kama mayai mkiamini ndio mapenzi....mtoto sio kuku kusema utakuja umle ....huyu ni binadam ambaye tunategema kesho aweze kujitegema na kuyatawala mazingira yake.Watoto wa sasa hivi ni lonyolonyo sana, nashauri mbunge litunge sheria iwe ni lazima kwenda JKT.
Kiukweli mnatusikitisha sana Toto lipo high school bado linasimamiwa na wazazi hawezi hata kujisimamia.
Kizazi hiki bila kukipitisha jeshini tunaandaa msiba mkubwa kwa Taifa.
Habari zenu Wana JF,
Naomba msaada kufahamu madhara ya kuacha kuripoti wito wa kujiunga na JKT kwa wale waliomaliza A level.
Je, cheti cha kumaliza mafunzo ya JKT huwa kinahitajika kwa ambaye anataka kufanya maombi vyuo vikuu vya Serikali kama UDSM, Tanzania Institute of Accountancy na IFM, kwa mfano?
Lakini la ziada: kama mhusika hatafanya maombi ya mkopo kupitia HESLB ataathirika namna gani?
Asanteni kwa msaada.
Nakazia hoja 100%.
Ewe kijana, kama utabahatika kupitia uzi huu nakushauri NENDA Karipoti JKT.
Manufaa ya kupitia Jeshini hayako wazi kivile na ndo maana wapo wachangiaji hapa wanasema(wanadai) ni kupoteza muda. Sio kupoteza muda hata kidogo.
Hebu fikiria ww kama kijana unatakiwa uwe jasiri, mvumilivu, ngangari, mbunifu, mwenye kuthubutu na mwenye kujisimamia - Kule JKT hayo utayapata na utakuja kugundua hilo baadaye utakapokuwa tayari umeshamaliza Jeshi na uko mitaani au kwenye ajira binafsi au kwenye Mashirika yasiyo ya kiserikali au hata Serikalini.
Usikubali ushauri wa hao ambao hawakupita huko na ndo hao Laini-laini(Nyoronyoro) anashindwa hata kutembea kwa miguu Km 3 eti ni mpaka apande boda.
Hahaha daah asee, noma kweli,
Ndo mnavyo danganyanaaa? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna posho pia watapewa huko jeshini mkuu. Unatoka na mtaji wa biashara kabisa
Nenda JKT kijana, hicho cheti kina umuhimu wake hata kama sio kwa kufanya application ya chuoJe, cheti cha kumaliza mafunzo ya JKT huwa kinahitajika kwa ambaye anataka kufanya maombi vyuo vikuu vya Serikali kama UDSM, Tanzania Institute of Accountancy na IFM, kwa mfano?
Kwa nini mkuuHata ingekua na madhara gani kweny ajira, mtoto au ndugu yangu wa kike hawezi kwenda JKT, wakiume kama ana afya na ye mwenyewe karidhia anaweza akaenda
Huko JKT watoto wanakwenda kupotezea muda na kutumikishwa bila sababu za msingi. Mimi mdogo wangu au mwanangu hawezi kwenda huko na hakuna mtu atakayemzuia kuingia Chuo Kikuu. Waache ujinga wa kuwatesa watoto wa watu makusudi.Habari zenu Wana JF,
Naomba msaada kufahamu madhara ya kuacha kuripoti wito wa kujiunga na JKT kwa wale waliomaliza A level.
Je, cheti cha kumaliza mafunzo ya JKT huwa kinahitajika kwa ambaye anataka kufanya maombi vyuo vikuu vya Serikali kama UDSM, Tanzania Institute of Accountancy na IFM, kwa mfano?
Lakini la ziada: kama mhusika hatafanya maombi ya mkopo kupitia HESLB ataathirika namna gani?
Asanteni kwa msaada.