Kuna umuhimu wa kuripoti JKT kwa wahitimu wa Form 6?

Think wisely, Miezi mi3 ni michache sana. Kama hauna cha msingi cha kufanya nyumbani na una afya yako njema, nenda huko. Ni kuzuri kuna faida utajua siku ya mwisho. pia kuna advantage ya cheti utakachopata kitakusaidia kwenye mbele huko.
 
Nakubaliana na wewe kabisa mkuu, pia kama utaratibu huu ni kuwajengea vijana uwezo wa kizalendo pamoja na utambuzi wa skills mbalimbali za maisha basi nashauri usiwe na mazingira ya kiubaguzi kwani sio wote wanaomaliza huenda bali wengi wao huwa ni school candidates na sio PC. Unawezaje kuona SC anafaa kujiunga na JKT halafu PC asifae ilihali wote ni vijana wa kitanzania. Pili napata tabu kujua ni utaratibu upi ulitumika kutambua kuwa wanaostahili kwenda jkt kwa mujibu wa sheria ni hawa waliomaliza six pekee? Kwa nini kama lengo ni jema serikali isiweke utaratibu unaogusa kundi kubwa la vijana na iwe ni lazima labda mtu mwenye matatizo? Naomba nimalizie kwa kusema kwamba binafsi naliona kundi linalofaa kujiunga jkt kwa mujibu wa sheria ni hawa wanaomaliza kidato cha nne na iwe hivyo kwa wote kabisa kabisa.
Sababu ni kama zifuatazo:-

1/. Utagusa kundi kubwa sana la vijana.

2/. Kutokana na mazingira ya sasa, utakuwa umeokoa vijana wengi kwa kuwafanya wakakamavu na kuwaondolea hali ya urojourojo ikumbukwe kwamba siku hizi mfumo wa maisha umebadilika vijana wengi wamezoeshwa maisha mwendokasi kwa hiyo kusubiria wamalize kidato cha sita wanakuwa wameshakubuhu.

3/. Ni kundi ambalo lina muda mrefu wa kukaa jkt bila kuwaza mambo mengine kwani huwa kuna gap kubwa kutoka kumaliza shule, matokeo kutoka, selection na kujiunga na ngazi nyingine za elimu. Na hapa utakuwa umeokoa au umenusuru watoto wengi dhidi ya mambo kurupushi ya mtaani mfano kuolewa kabla ya kufikia malengo, na mengine yenye kufanana na hayo.

4/. Kundi hili kubwa mara baada ya kumaliza mafunzo hayo, nina imani vijana wetu hawatabaki kama walivyoingia na hatimae nchi itakuwa ina vijana wengi wanaojitambua.

NB. SERIKALI ISIOGOPE GHARAMA.
 
Hebu mwenye kufahamu tovuti ya JKT yenye kuonyesha majina ya waloitwa Jeshini,maana hii ya www.jkt.go.tz haipatikani,au siyo ya jeshi la kujenga taifa ?
 
Unauliza haya maswali Ili usiende JKT dogo??
 

Njoo na cheti chako cha JKT na mimi na hiki kitambi changu lakini ntakuponda vbya mno.

Hakuna faida yyte kwend JKT,Usimtishe dogo
 
Yajayo yanafurahisha
 
Yana ukweli hayo usemayo????
 
Mimi nilichaguliwa lakini sikwenda, madhara niliyoyapata Ni kushindwa kuapply kazi Kama za ujamiaji nk. Ila Mimi pia Ni mkakamavu sikuona sababu ya kwenda JKT
 
jkt kwa mujibu ( kupitia form six miezi3) haina faida yoyote maana hata magereza, polisi wanakataa wele wenye cheti cha jkt kwa mujibu wanataka wale waliojitolea kwa miaka kazaa juzi tu hapa ajira za vyombo vya ulinzi zimetoka wale wote wenye vyeti vya kwa mujibu wamepigwa chini
 
Una fikra za kimasikini sana.
Huo muda unaopoteza kulima bustani bora ukawe machinga
 
KUNA UMUHIMU SANA KUNA KUSAIDIA KUPATA MARAFIKI WAPYA AMBAO BADAE NDO WAMBANGA WA WANAO ....UMEELEWAA JICHANGANYE NA WATU
 
Ndio maana mnaitwa wajinga na wapumbavu.
Hayo yote ulitakiwa fundishwa na waliokuzaa
 
Achana na hao wapumbavu, jeshi kwa Tz halina maana. Hakuna uzalendo unafundishwa kwa miezi 3
 
Kijana, nenda JKT.
Siku zitakuja mbeleni, very soon, kuna fursa zitatokea na kwa makusudi kabisa, watasema aliyepita JKT ana "added advantage"
Hakuna madhara ya kupitia JKT, bali kuna faida.
Siku za mbeleni zipi wakati kuna kundi kubwa la wasio na ajira na wamepita huko?
Watu wasipoteze muda wao kwenda jiahangaisha
 
Mbona kuna kundi kubwa la wasiojua kusoma na kuandika wa zama hizo kuliko zama hizi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…