Kuna umuhimu wa kuripoti JKT kwa wahitimu wa Form 6?

Kuna umuhimu wa kuripoti JKT kwa wahitimu wa Form 6?

Huko wapelekwe watoto wa masikini
Watoto wa maskini wanashindwa kwenda kwa sababu mara nyingi kambi zinakua mbali na mahitaji ya kununua ni gharama pia familia nyingi huko vijijini hazimudu.
 
Hakina mchango wowote mambo ya kutesa watoto Bure tuu, jkt waende wa kujitolea wanaotaka na wenye uhakika wa kuajiriwa jeshini, vinginevyo ni porojoo tuu havisaidii lolote
Mafunzo ya kijeshi unaita kutesa watoto, ingekua mteremko isingekua mafunzo.
 
Kwa mtoto wa kike kazi anayo kwakweli..mimi nikiwa mmoja wa waliopita huko nilikuwa nawahurumia sana .
 
Kama unataka kwenda kwenye majeshi siku za usoni,nenda,ila kama huna hilo tarajio,unaweza usiende.Nakwambia hivyo kwasababu nakutana sana na majamaa waliopitia JKT na wapo mtaani,hawana maajabu zaidi ya kuombana pesa za winston wavute,huku wengine wakiwa wamepigwa na maisha,pasipo kutumia mazingira yanayowazunguka kujinufaisha.
 
Habari zenu Wana JF,

Naomba msaada kufahamu madhara ya kuacha kuripoti wito wa kujiunga na JKT kwa wale waliomaliza A level.

Je, cheti cha kumaliza mafunzo ya JKT huwa kinahitajika kwa ambaye anataka kufanya maombi vyuo vikuu vya Serikali kama UDSM, Tanzania Institute of Accountancy na IFM, kwa mfano?

Lakini la ziada: kama mhusika hatafanya maombi ya mkopo kupitia HESLB ataathirika namna gani?

Asanteni kwa msaada.
**kinachonitesa mimi ni hizo gharama walizotupa yani juzi tu NAULI watoto wamerudi....Leo tena mara viatu.. truck makaptura.. jacket NAULI tena ya kwenda SONGWE kutoka DODOMA....hata usingizi sipati.
 
Mkuu tuache siasa tuseme ukweli, Kama hhna ndoto za kujiunga jeshi kwenda Jkt ni kupoteza muda.

Hivi kijana wa miaka 19 aliyemaliza kidato cha 6 nini atakwenda kujifunza ambacho hajajifunza nyumbanibjwao kwa miaka yote tangu anazaliwa.

Hivi hujaona watoto wa darasa la pili wanahudumia wateja madukani na magengeni au hata barabarani wakizungusha mboga? Utajifunza kilicho kwenye familia yako automatically.

Hata hivyo enzi hizi siyo za kujivunia kwenda kujifunza eti kuchoma mkaa, kufyatua matofali, n.k... na ukifuatlia siyo kwamba elimu hutolewa labda ya kilimo bali wanatumika tu km mashine za uzalishaji.

Mazoezi yenyewe ukirudi mtaani wiki mbili tu yashapotea.

Tuache uzamani, mambo ya miaka ya 70 yamekwishapitwa na wakati.
Sidhani kama ndivyo ilivo. Huo "ukisasa" ndo unaowaponza vijana wengi. Kijana anadhani kumaliza kidato cha sita ndo amemaliza elimu au ndo amejua mengi. Huo ni ufinyu wa kimawazo. Kijana ameshasahau kwamba pale jeshini anakula na kulala. Sasa nani alipie hiyo gharama? Akumbuke hapo sio nyumbani kwa babake. Umeme, maji, akiugua anapelekwa Hospitali Kuna ulinzi (+ kaposho kidogo)n.k. n.k. Yote hayo ni gharama. Nani anagharamia? Lazima afanye kazi. Na hilo ndo Elimu.
Wewe mzazi/Mlezi usijisahau kwamba iko siku (tena ni lazma)hutakuwepo naye i.e. utakuwa umeRIP. Hapo ndipo kijana ataanza kuona "marinjerinje" kwani hakuandaliwa au hakujiandaa.
 
Una fikra za kimasikini sana.
Huo muda unaopoteza kulima bustani bora ukawe machinga
Umachinga sio kitu rahisi kivile. Machinga hapandi bodaboda- ni mguu asubuhi hadi jioni -jua lake na mvua yake,saa nyingine wanadhulumiwa. Je, hawa vijana wa dotcom.mayai watamudu kazi hiyo ya suluba?
Machinga hizo bidhaa anachukuwa kwa kauli-mali dukani. Jioni anarudisha mahesabu. Je, hawa vijana legelege eti ni F6 atamudu? Kumbuka sio wote F6 wanatoka familia zenye ahueni au zilizojitosheleza. Vijana waache tabia mbaya ya kudanganyana eti nitafungua fremu yangu, ntanunua kinglion napiga boda n.k.
Mimi nashauri Waende JKT wakakomae huko kifikra na kimtizamo kwani "Ukisasa" wanaoshobokea(wanajaribu kuukumbatia) unadai mtu kuwa na salio-anzia.(Capital inputs). Muda anaotumia kulima, kukimbiakimbia n.k. tungeweza kuita ni Field practicals. Akitoka jeshini ni nadra sana maisha ya Uraiani kumshinda - labda iwe na huko jeshini alikua ni selule.
 
Sidhani kama ndivyo ilivo. Huo "ukisasa" ndo unaowaponza vijana wengi. Kijana anadhani kumaliza kidato cha sita ndo amemaliza elimu au ndo amejua mengi. Huo ni ufinyu wa kimawazo. Kijana ameshasahau kwamba pale jeshini anakula na kulala. Sasa nani alipie hiyo gharama? Akumbuke hapo sio nyumbani kwa babake. Umeme, maji, akiugua anapelekwa Hospitali Kuna ulinzi (+ kaposho kidogo)n.k. n.k. Yote hayo ni gharama. Nani anagharamia? Lazima afanye kazi. Na hilo ndo Elimu.
Wewe mzazi/Mlezi usijisahau kwamba iko siku (tena ni lazma)hutakuwepo naye i.e. utakuwa umeRIP. Hapo ndipo kijana ataanza kuona "marinjerinje" kwani hakuandaliwa au hakujiandaa.
Ukisasa nliomaanisha ni kuwekeza kwenye matumizi ya teknolojia mkuu.

Hivi kwa miaka hii, watu mnaondoka kambini na ndoo mnaenda kumwagilia bustani/shamba kilomita 10, mnasomba mchanga kwa ndoo kilomita 5 n.k, unafundishwa kujificha porini, Enzi hizi kweli.

Sijakataa hayo ila yafanyike kwa wahusika wenyewe, kwa kijana wangu hiyo miezi mitatu bora asome driving na hata compute kidogo.
 
Yana ukweli hayo usemayo????
Huyo ndugu unaweza kumwelewa fikra zake na mtizamo wake kutokana na maneno au sentensi alizotumia. Always his thoughts are focused on the Inguinal area. Anadhani afikirivyo yeye au kuamini ndivyo hali halisi ilivyo. Pengine hajapita JKT na kuhakikisha kwamba unaweza kulala na Ke kwenye handaki moja uck kucha na usikumbuke wala kutamani kufanya chochote.
 
Ukisasa nliomaanisha ni kuwekeza kwenye matumizi ya teknolojia mkuu.

Hivi kwa miaka hii, watu mnaondoka kambini na ndoo mnaenda kumwagilia bustani/shamba kilomita 10, mnasomba mchanga kwa ndoo kilomita 5 n.k, unafundishwa kujificha porini, Enzi hizi kweli.

Sijakataa hayo ila yafanyike kwa wahusika wenyewe, kwa kijana wangu hiyo miezi mitatu bora asome driving na hata compute kidogo.
Mkuu, Kijana Amemaliza F6 juzi tu, ana nini cha kuwekeza na kutoka wapi? Kijana F6 anateknolojia gani? masomo (combination ) ya masomo ya sekondari kuanzia F1 -F6 ni Nadharia(Theory) tu sio Applied. Hana ujuzi unaotambulika rasmi labda kama ni mtundu-mtundu anaweza kujua vichache sana kwa matendo.
Kama ni wewe mzazi/mlezi umemwandalia basi ujue 100% atasquander huo mtaji halafu atainua macho na kukutizama akimaanisha "Leta tena".
Lakini kama ni yeye mwenyewe kwa juhudi zake hiyo iko poa. Je, ni vijana wangapi watakuwa na mwelekeo huo? Je, kweli katika hizi wiki tatu -nne alizokaa hapo nyumbani ameweza kujitafutia cha kuwekeza? Hebu tuwe wa kweli. Kumpeleka kujifunza computer au Udereva ni added advantage kwa maana kwamba hiyo ni taaluma/ufundi/ujuzi utakaomrahisishia kiutendaji kwa kile atakachokuja kufanya hapo baadaye.
Kule shuleni alikuwa anatumia ubongo zaidi(Mental work) Sasa mwache atumie misuli (Physical work) kwa kubeba ndoo, kulima, kusomba mchanga n.k. ili ajifunze maisha sio lelemama na sio kila mahali mzazi/mlezi atakuwepo kukusapoti - iko siku mzazi /mlezi hatakuwepo kabisa-anawezakuwa ameRIP. Kijana ajifunze kusimama kwa miguu yake mwenyewe tena ajitafutie vitu/mali/chakula kihalali au kwa jasho lake mwenyewe sio vya kupewa.
 
Wameshaanza kuomba pesa za kununulia simu, acha waende wakajifunze maisha sio kunenepeana na kujaza mashavu bila sababu, ngoja waende wakajifunze hata kutumia mabumu yao watakapoanza vyuo
Ndiyo kabisa.Wanaweka (wengi wao)kipaumbele kwenye kuchakata mbususu wanadhani ni ushujaa. Stupid sana.
 
Mkuu, Kijana Amemaliza F6 juzi tu, ana nini cha kuwekeza na kutoka wapi? Kijana F6 anateknolojia gani? masomo (combination ) ya masomo ya sekondari kuanzia F1 -F6 ni Nadharia(Theory) tu sio Applied. Hana ujuzi unaotambulika rasmi labda kama ni mtundu-mtundu anaweza kujua vichache sana kwa matendo.
Kama ni wewe mzazi/mlezi umemwandalia basi ujue 100% atasquander huo mtaji halafu atainua macho na kukutizama akimaanisha "Leta tena".
Lakini kama ni yeye mwenyewe kwa juhudi zake hiyo iko poa. Je, ni vijana wangapi watakuwa na mwelekeo huo? Je, kweli katika hizi wiki tatu -nne alizokaa hapo nyumbani ameweza kujitafutia cha kuwekeza? Hebu tuwe wa kweli. Kumpeleka kujifunza computer au Udereva ni added advantage kwa maana kwamba hiyo ni taaluma/ufundi/ujuzi utakaomrahisishia kiutendaji kwa kile atakachokuja kufanya hapo baadaye.
Kule shuleni alikuwa anatumia ubongo zaidi(Mental work) Sasa mwache atumie misuli (Physical work) kwa kubeba ndoo, kulima, kusomba mchanga n.k. ili ajifunze maisha sio lelemama na sio kila mahali mzazi/mlezi atakuwepo kukusapoti - iko siku mzazi /mlezi hatakuwepo kabisa-anawezakuwa ameRIP. Kijana ajifunze kusimama kwa miguu yake mwenyewe tena ajitafutie vitu/mali/chakula kihalali au kwa jasho lake mwenyewe sio vya kupewa.
Nayaongea haya nkiwa na cheti cha jkt mujibu 2014, basi kila mtu ana maoni yake, kwangu mimi sioni asvantage kwa kweli, nilipotezewa tu muda bora ningewasaidia wazazi wangu kuvuna.

Afu uzalendo ni tabia tu wala haufundishwi, Hawa wanaoiba na kufuja fedha za umma wote walipita jkt tena mwaka mzima.
 
Watoto wa sasa hivi ni lonyolonyo sana, nashauri mbunge litunge sheria iwe ni lazima kwenda JKT.

Kiukweli mnatusikitisha sana Toto lipo high school bado linasimamiwa na wazazi hawezi hata kujisimamia.

Kizazi hiki bila kukipitisha jeshini tunaandaa msiba mkubwa kwa Taifa.
Kuna mmoja aliletwa na mama yake kuripoti shule form five tulimcheka mpaka Basi.
 
Back
Top Bottom