Kuna Upigaji mkubwa sana kwenye Miradi ya Ujenzi hasa Barabara

Kuna Upigaji mkubwa sana kwenye Miradi ya Ujenzi hasa Barabara

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Katika fuatilia zangu, nimegundua kuwa kuna upigaji mkubwa sana kwenye miradi ya ujenzi hasa majengo mbalimbali na barabara nchini Tanzania.

Kiukweli barabara nyingi nchini zinajengwa chini ya kiwango, kuanzia upana , hadi ubora wa barabara husika na kamwe huoni wakandarasi wakichukuliwa hatua jambo linaloashiria kandarasi husika kupatikana kwa njia ya rushwa.

Nimejaribu kufuatilia namna barabara za wenzetu kwenye mataifa ya hapa hapa Afrika zinavyojengwa mfano Afrika Kusini, Algeria, Ivory Coast, Kenya na hata Morocco na kusema kweli nimekuja kugundua barabara zetu zinajengwa kwa viwango duni sana na kwa gharama kubwa sana tofauti na wenzetu.

Ukitazama barabara nyingi zinazojengwa na Tarura hazina hata sehemu za Watembea kwa miguu (Pedestrians) au waendesha baiskeli na nyingi hazifungwi hata taa za kuona usiku kwa watembea kwa miguu na inasemekana fedha hizo huwa zinatengwa kwenye bajeti za ujenzi wa barabara husika.

Pia ubora wa barabara zetu kwenye uimara ni duni sana. Nyingi ya barabara zinazojengwa kwetu huaribika kabla hata ya kufika miaka 10 baada ya kujengwa tofauti na mataifa mengine.

Tanzania tuna kazi kubwa sana kwa kweli hasa katika uadilifu wa watu wetu na uzalendo wa wstu wetu katika kufanya mambo wakiangalia maslahi ya Taifa badala ya maslahi yao binafsi.

Angalia jinsi barabara za wenzetu zinavyojengwa👇

FB_IMG_1726470257483.jpg
FB_IMG_1726470234100.jpg
FB_IMG_1726470127169.jpg
 
Kimara-kibaha highway watu wanavuka kwenye zebra!!maengineer kweli walishindwa kuweka vivuko vya underground!vitu vingine hadi aibu aisee!
Ile ni aibu ya karne. Barabara ya mwendokasi mbagala saivi wanajaza mitaa ya kuongoza magari barabarani kama uchafu vile. Unajiuliza hawakuwaza kuweka vivuko vya underground au vya juu kweli?

Alafu kila siku kutaka kujiita sijui ma engeener. Hadi kwenye majina yao saivi wanaanzia na Eng. Edwin sijui Eng Agnes
 
Katika fuatilia zangu, nimegundua kuwa kuna upigaji mkubwa sana kwenye miradi ya ujenzi hasa majengo mbalimbali na barabara nchini Tanzania.

Kiukweli barabara nyingi nchini zinajengwa chini ya kiwango, kuanzia upana , hadi ubora wa barabara husika na kamwe huoni wakandarasi wakichukuliwa hatua jambo linaloashiria kandarasi husika kupatikana kwa njia ya rushwa.

Nimejaribu kufuatilia namna barabara za wenzetu kwenye mataifa ya hapa hapa Afrika zinavyojengwa mfano Afrika Kusini, Algeria, Ivory Coast, Kenya na hata Morocco na kusema kweli nimekuja kugundua barabara zetu zinajengwa kwa viwango duni sana na kwa gharama kubwa sana tofauti na wenzetu.

Ukitazama barabara nyingi zinazojengwa na Tarura hazina hata sehemu za Watembea kwa miguu (Pedestrians) na nyingi hazifungwi hata taa za kuona usiku kwa watembea kwa miguu na inasemekana fedha hizo huwa zinatengwa kwenye bajeti za ujenzi wa barabara husika.

Tanzania tuna kazi kubwa sana kwa kweli hasa katika uadilifu wa watu wetu na uzalendo wa wstu wetu katika kufanya mambo wakiangalia maslahi ya Taifa badala ya maslahi yao binafsi.View attachment 3097223View attachment 3097224View attachment 3097225
Sasa picha ulizoonesha na mifano ya Barabara kukosa sehemu ya watembea Kwa miguu vinahusianaje na ujenzi chini ya kiwango?

Wewe ni mjinga mmja tuu,design ndio inaamua Barabara ijengwe vipi na mwisho sio kweli kwamba Barabara zetu Hazina watembea Kwa miguu.
 
Ile ni aibu ya karne. Barabara ya mwendokasi mbagala saivi wanajaza mitaa ya barabarani kama uchafu vile. Unajiuliza hawakuwaza kuweka vivuko vya underground au vya juu kweli?

Alafu kila siku kutaka kujiita sijui ma engeener. Hadi kwenye majina yao saivi wanaanzia na Eng. Edwin sijui Eng Agnes
Sometimes najiuliza hawa wasomi wetu tutawategemea kwenye kipi? Duniani kuna barabara yenye taa nyingi kama kilwa road?
 
Sometimes najiuliza hawa wasomi wetu tutawategemea kwenye kipi? Duniani kuna barabara yenye taa nyingi kama kilwa road?
Makosa ya design(usanifu) sio swala la kujengwa chini ya kiwango.

Kwenye usanifu Tunafeli sana na pia tumekariri sana maisha.

Mfano hakuna sababu za msingi za kujenga Barabara za Tarura kwenye Miji yetu kidogo Kwa gharama kubwa bila kuzingatia matumizi ya Sasa na yajayo.
Barabara za TACTIC ni mfano mmjawapo tuu.
 
Back
Top Bottom