Katika fuatilia zangu, nimegundua kuwa kuna upigaji mkubwa sana kwenye miradi ya ujenzi hasa majengo mbalimbali na barabara nchini Tanzania.
Kiukweli barabara nyingi nchini zinajengwa chini ya kiwango, kuanzia upana , hadi ubora wa barabara husika na kamwe huoni wakandarasi wakichukuliwa hatua jambo linaloashiria kandarasi husika kupatikana kwa njia ya rushwa.
Nimejaribu kufuatilia namna barabara za wenzetu kwenye mataifa ya hapa hapa Afrika zinavyojengwa mfano Afrika Kusini, Algeria, Ivory Coast, Kenya na hata Morocco na kusema kweli nimekuja kugundua barabara zetu zinajengwa kwa viwango duni sana na kwa gharama kubwa sana tofauti na wenzetu.
Ukitazama barabara nyingi zinazojengwa na Tarura hazina hata sehemu za Watembea kwa miguu (Pedestrians) na nyingi hazifungwi hata taa za kuona usiku kwa watembea kwa miguu na inasemekana fedha hizo huwa zinatengwa kwenye bajeti za ujenzi wa barabara husika.
Tanzania tuna kazi kubwa sana kwa kweli hasa katika uadilifu wa watu wetu na uzalendo wa wstu wetu katika kufanya mambo wakiangalia maslahi ya Taifa badala ya maslahi yao binafsi.
View attachment 3097223View attachment 3097224View attachment 3097225