Imenibidi niulize tena swali hili, ambalo watu wengi wameamini tu kwa kusikia/kuambiwa kwamba ni "vyombo vya dola" vinahusika na mauaji hayo.
Hivi vyombo vinavyojulikana ni polisi, Jeshi, au hata TISS?
Kuna ushahidi wowote unaoonyesha uhusika wa polisi au jeshi katika mauaji hayo?
Picha zote zinazoonyeshwa za watu walioshikilia silaha na kuwawinda waTanzania mitaani hazionyeshi polisi au jeshi, kwa utambulisho wa mavazi yao kuwa ndio wahusika wa mauaji.
Je, haiwezekani hawa watu wakawa ni makundi maalum yaliyoandaliwa kufanya kazi hii nje ya taratibu za kidola?
Hata Tume ya mchongo ya Chande haisemi kuwa ni polisi waliohusika na mauaji hayo; wala jeshi la ulinzi.
Kwa nini basi iaminiwe tu kijumlajumla kuwa mauaji yalitekelezwa na vyombo vya dola.
Hii dola imewekwa tu kuwa kisingizio cha mauaji yaliyopangwa nje ya utaratibu wa kiutawala.
Ndiyo maana kuna haja ya kuwepo na uchunguzi huru kutambua wahusika hasa ni akina nani, na walipewa kazi hiyo na nani.
Pamoja na ubovu wa polisi ulivyo, bado siyo sahihi kuwatwisha tu mzigo ambao pengine hauwahusu, zaidi ya akina Camilius na Jamanne Muliro. kufanya mipango nje ya taratibu za jeshi hilo.
Sijaona picha yoyote ya polisi aliyekuwa mitaani siku hiyo, akiwa ndani ya unifomu; jambo ambalo linashangaza sana!