Kuna uwezekano Aubin Kramo hajui kuwa jina lake limeondolewa kwenye wachezaji wa Simba

Siku mkipata nafasi ya kumuuliza jaribu tena..uliza swali hili eti mwenyekiti yule wakala wa kutoka DRC ulimlipa hela zake ? Na yule wakala mwingine toka Anayeishi Morocco 🇲🇦 alilipwa ..akikujibu utaniambia
 
Ushauri wangu ukikutana na Mr Jaribu tena mwambie yule wakala wa drc na yule wa Morocco vipi kamalizana nao ?
 
Siku mkipata nafasi ya kumuuliza jaribu tena..uliza swali hili eti mwenyekiti yule wakala wa kutoka DRC ulimlipa hela zake ? Na yule wakala mwingine toka Anayeishi Morocco [emoji1173] alilipwa ..akikujibu utaniambia
Sitajisumbua kumuuliza maana najua nitafukuzwa kama Mbwa. Jaribu Tena ni kirusi kisicho na tiba Simba.
 
Muda wote mngekuwa mnajikita zaidi kwenye kujadili yale mazuri na pia mapungufu yote ya timu yenu, kama ulivyofanya hapa! Sidhani kama kuna mtu angewaita nyinyi ni mbumbumbu.
 
Binafsi niliacha kuzifuatilia hizi timu.

Nilifanya kazi simba NIKAKUTANA NA UOZO KILA KONA.

Simba na yanga ni virusi vya maendeleo ya mpira wa Tanzania.
 
Wenzake walishaanza kumwambia njoo huku kupo fresh zaidi.
Mikiani kwa roho mbaya wakasema isiwe tabu baki kwanza.
 
Simba inaonekana viongozi Wana wachezaji wao, hata Kakolanya alifanywa kipa wa tatu makusudi ili aondoke.
Wanachama wanaochagua hao viongozi hawana uchungu na timu kabisa.
Hao wanachama wanajulikana ili watajwe watu wawawjue? Ina mana wao ndio wanapanga timu sasa na kuamua nani acheze nani asicheze
 
Hao wanachama wanajulikana ili watajwe watu wawawjue? Ina mana wao ndio wanapanga timu sasa na kuamua nani acheze nani asicheze
Simba walipomleta.kipa mbrazil Kuna mwanachama wa Simba aliniambia yule mchezaji hatadumu mwaka nikambishia akaniambia wewe hujui zile biashara za watu na bado sikuamini mpaka niliposikia mikataba umesitishwa sababu ya majeraha kambini.
Huyo mchezo Simba upo muda mrefu, ndio maana Kuna makocha wazuri wanaonekana hawafai kumbe tunaeawekea wachezaji magumashi.
Hivi klabu ya Simba na ukubwa wake inaweza kusajili mchezaji bila kumpima afya, na lile benchi lote kazi yake ni nini?
 
Sasa mkuu, wakifanya hivyo au wanaofanya hivyo malengo yao ni nini? Maana ya kuleta wachezaji wabovu mana yake nini? Wapate tu hizo 10%? Hawataki SIMBA ipate mafanikio? Je hawaoni simba kuchukua ubingwa ligikuu na kuingia nusu fainali ni mafanikio hata kwao kupitia hao wachezaji wao wanaowachukulia 10% zao sio kwamba wangekua wanahakikisha simba inapata vikombe vya ubingwa kwanza mana wanapofeli hao wachezaji watakosa motisha na kuondoka
Au ndio hawana uchungu wao hawajali simba ishinde isishinde mtajua wenyewe, wao wachezaj wao akipata mshahara, anatoa 10% anampa mwanachama husika, maisha yanaendelea
 
Dooh ningum sana kuelewa kwa sasa.
Wacha tusubir pindi atakapo pewa thankU yataibuka mengi kumhusu kramo.
 
Hawana uchungu, wameweka maslahi mbele na hili halikuanza Leo lipo enzi na enzi.
Bakhresa alijiondoa Simba baada ya kushikiwa kisu na mwanachama kisa alitaka kuwajengea Simba hostel, Kuna kipindi Simba ilipata mwekezaji wa kuwajengea Msimbazi lakini aliondoka baada ya kumleta mpiga picha apige picha ya jengo akapigwa na watu waliokuwa wanashindea klabuni kisa wanadai uongozi ulitaka kuuza jengo.
Jengo la Simba lilijengwa mbavuni waliosema wameweka msingi wa ghorofa saba kumbe ni ghorofa tatu wahusika wapo.
Jengo la Simba lilimegwa kwa nyuma na kuuzwa lakini husikii lolote wahusika wapo.
Malkia wa nyuki alijiondoa. Baada ya kugundua viongozi walikuwa wanakula pesa za mishahara ya wachezaji mhusika yupo Tena akiongea watu watu .wanamsifia..
Wachezaji bomu wameanza kuletwa muda mrefu mfano pape ndiew aliyekuja na hirizi, mchezaji aliyesajuliwa kuziba nafasi ya Samatta akaishia kucheza mechi moja Tena walisema alikuwa akimweka Samatta benchi. Kuna yule Gyan yupo Singida walimsajili dola laki moja alikuja Kama forward wakambadilisha kuwa beki.
Bus la Simba limeuzwa kinyemela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…