100 others
JF-Expert Member
- Aug 5, 2017
- 10,825
- 38,702
Chivayo alinunua ndege hio ya gharama kubwa, kumsaidia kuepuka traffic katika jiji la Harare na pia kumsaidia kufika kwenye vikao muhimu katika masuala yake ya kibiashara. Kwa mujibu wa maelezo yake.
Inaitwa Leonardo AW139, ina engines mbili, na inaendeshwa na marubani wawili.
Hio Helicopter kainunua mwaka huu huu 2026 nadhani mwezi May, katika kufuatilia mitandaoni sikupata model ya ndege au ni ndege ya aina gani ambayo amepata nayo ajali, katika kupita huku na kule ndipo nimegundua alinunua hio ndege ya kifahari aina ya Leonardo AW139.
Ni ndege ya gharama ,luxury na inatumiwa na watu maarufu, gharama aliyonunulia ni USD 9.8 million ni sawa na bilioni 26 na pointi kwa pesa za Kitanzania.
Kwanini nasema inawezekana ndio ndege aliyoanguka nayo? Kwa sababu vyanzo vya kuaminika vinasema kwenye ndege kulikuwa na marubani wawili, helicopter nyingi inaendeshwa na rubani mmoja, hio AW139 ni helicopter kubwa na luxury na inabeba hadi watu 15 na inaendeshwa na marubani wawili.
Kwenye mtandao wa linkedin kwenye account yake mwenyewe Chivayo, miezi mitatu iliyopita alipost hii video hapa chini. aliandika "LEONARDO AW139 coming home...9.8 million USD well spent...💪💰🇿🇼🇿🇼🇿🇼" aka ambatanisha na video.
AW139 inasifika kwa kwa kutengenezwa na advanced safety features, ina engines mbili, engine moja ikipata tatizo nyingine inaweza kuendelea na safari na hatimae helicopter ikatua mahala salama.
Hio ndege inatumika hadi kwenye missions za SAR, Search And Rescue, helicopter ambayo imepitishwa kufanya SAR missions ujue tu ina uwezo mkubwa wa kuvumilia mazingira magumu ya hali ya hewa.
Kiukweli siku ikifika imefika tu..