Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kuna watu wamemlaumu raisi Samia moja kwa moja kwamba anahusika na utekaji na uuaji unaofanyika nchini kwa sababu kuna viashiria vikubwa sana vyombo vya dola vinahusika katika uhalifu huu.
Lakini je, ni kweli kwamba raisi Samia anahusika moja kwa moja na utekaji na uuaji unaofanyika nchini hivi sasa? Binafsi sidhani kama raisi Samia anahusikika moja kwa moja kama ilivyokuwa kwa raisi Magufuli. Hata hivyo, raisi Samia hawezi kukwepa lawama, na hili anapaswa alitambue.
Raisi Samia anajua wazi kwamba huu mchezo wa kuteka na kuua, wakati wa Magufuli, uliingizwa katika vyombo vya dola vya usalama, kwa namna ya kuwa "kajimfumo" (informal institutionalization in the government security organs), na watu walipewa hii kazi maalum. Na sasa kuna dalili kwamba kale "kajimfumo" alikokaanzisha Magufuli bado kanaendelea, labda bila Samia "kuhusika" kwa namna ya yeye kuchagua kutohusika moja kwa moja, au kutojua.
Na tena, inawezekana kabisa raisi Samia hahusiki kwa kuwa kuna watu ambao walihusika na "kajimfumo" ka Magufuli ka kuteka na kuua, ambao wanaendelea kufanya haya wakiona kwamba, kama walifanya haya kwa faida ya Magufuli na serikali/CCM wakati ule, basi wanapaswa kufanya haya sasa kwa faida ya raisi Samia na serikali/CCM, hata kama Samia hatakubaliana na hili.
Lakini pia, inawezekana kabisa wanaofanya haya wanafanya haya wakiwa wamemshawishi Raisi Samia kuwaacha wafanye kile ambacho wanaona ni kwa faida yake na serikali/CCM bila yeye kuhusika moja kwa moja kama ilivyokuwa kwa Raisi Magufuli, kwamba wewe tuachie sisi, tunajua la kufanya, wewe kaa kando.
Na pia, inawezekana wanaoteka na kuua wanafanya haya kwa faida yao wenyewe, kwamba ni ka "sindiketi" fulani ka viongozi mafisadi ambao wanaelewa uwepo wa raisi Samia madarakani unawapa fursa kubwa za kujitajirisha na hivyo wanakaendeleza kale "kajimfumo" ka Magufuli kwa kutumia fedha zao wenyewe kugharamia "kajimfumo" ka utekaji na uuaji bila raisi Samia kuhusishwa wala fedha za serikali kutumiwa!
Lakini sasa, ni vigumu sana kuwazia kwamba watu walio katika mfumo wa vyombo vya dola vya usalama, au viongozi mafisadi serikalini, wanaweza kufanya haya bila raisi Samia kujua. Haiwezekani kabisa kwamba "intelijensia" ya raisi Samia ndani ya serikali na vyombo vya dola vya usalama haina habari juu ya hili jambo ambalo linafanya raisi Samia asiwe na habari juu yake. Siwezi kuamini kwamba raisi Samia hajui juu ya hili kwa sababu tu ya udhaifu wa intelijensia yake binafsi (the president's people) au intelijensia rasmi ndani ya serikali au vyombo vya dola vya usalama, ambayo ingempa habari kamili juu ya jambo hili. Huwezi ukawa raisi wa nchi halafu usiwe na intelijensia ndani ya vyombo vya usalama ya kukuwezesha kujua jambo kama hili - utapinduliwa au kuuawa kirahisi sana!
Kwa maelezo haya, inafanya raisi Samia astahili lawama zote za utekaji na uuaji unaoendelea, hata kama hahusiki moja kwa moja. Kumbuka, ilikuwa ni intelijensia binafsi ya Magufuli iliyomwambia kwenye mkutano huu nenda na kiti chako usikalie kiti walichokuandalia, au ukienda kwenye ile ziara, jifanye unaenda kula kwa mama ntilie usile chakula walichokuandalia! Sasa, ndio tuseme raisi Samia hana intelijensia ya namna hii? Siamini!