Tetesi: Kuna uwezekano mkubwa wa LOCKDOWN nchi nzima. Kama hujajiandaa fanya sasa

Status
Not open for further replies.
70% ya watanzania tunaishi maisha ya ndege yaani tukishakwisha amka asubuhi hatujui leo rizki inatoka wapi .Sasa watupige hiyo LOCK DOWN si ndo watasababisha vifo vingi vya njaa kuliko ambavyo vingesababishwa na huyo covid19
Kuna kitu watu wengi mnajidanganya. Mnasema ni bora kufa kwa corona kuliko kufa kwa njaa.

Wewe na wenzako wenye mindset kama yako mkae mkijua kwamba moja ya masharti ya mtu anayeumwa Covid 19 ni kurest.

Ukishaumwa hiyo corona kuendelea kufanya kazi zako itakuwa ni kukitafuta kifo chako kwa kasi.

Hapo ndipo tutakapopukutika kama kuku wenye kideli.
 
Do you think wenye hayo maduka ambayo ww unataka yafungwe watakuelewa?
 
Serikali ikiona umuhimu wa kuboresha mwenendo wake wa awali ni sawa.

Ila tufanye taratibu ambazo shughuli za uzalishaji zitafanyika na pia ugonjwa nao utapunguzwa kuenea.

Kwani kwa inavyoonekana tunaletewa badala ya ugonjwa wenyewe kuanzia hapa.
Ukiachana na Quarrantine, Taja njia nyingine ambayo imewahi kutumika na kupelekea kupungua kwa cases mpya za Covid-19. Na hiyo njia ilitumiwa na nchi gani?
 
Labda kama serekali kuna kitu inaficha maana toka ugonjwa umeingia ni wagonjwa 20 tu tumewapata na kifo kimoja na waliopona wa 2 sasa ya nn kutufungia ndani wakati hakina maambukizi mapya
 
Ndoto za Alnacha! Usitutishe.. in Maalim's voice!
Ukiona mtu anawaza kufungiwa ujue hana nia njema na taifa hili. Ukiwa na akili timamu lazima uwafikirie na wengine. Watanzania wengi lazima watoke nyumbani ili waweze kula. HATA RAIS MWENYEWE ALILIONA HILO. HAKUSHINDWA KUTANGAZA HIYO LOCKDOWN YENU ILA KWAKIWA WATU WAKE ANAWAJUA NA KUWAJALI HAKUFANYA HIVYO. Anasisitiza hatua za tahadhari tu. Na matokeo ya hatua hizo tunayaona ni mazuri sana. TUAITISHANE NA KORONA JAMANI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watz hawana uwezo wa kukaa ndani muda wote. Tafadhali msiwagombanishe na serikali yao
 
Pohamba kwa usiku mi mwenyewe sioni mantik kwa sababu mikusanyiko inakua michache tofaut na mchana, tukifanya haya mambo kisiasa wananchi wataumia, maisha ya watanzania wengi bila kutoka nje hawaingizi siku unadhani itakuaje, serikal itaweza kuwagharamia?
 
tzkwanza ni kweli kwa hilo la nguvu wataweza ila kiuhalisia tuangalie maisha ya watanzania wengi kukaa ndani bila kutoka wataishi kwa kipato kipi na wengi bila kutoka basi siku haijaingia ukizngatia wanaomtegemea.
 
Kama Mkulu mwenyewe anazurula kwenye vijiwe vya kahawa,mwanae naye kila kukicha anakusanya watu na kuwahutubia hiyo lockdown itatokea wapi?
 
Kwanini umefikiria hivyo mkuu?

Je umeona ni njia sahihi au nji ya gharama ndogo katika kudhibiti maambukizi?

Kwa mtazamo wangu naona hiyo njia sio sahihi kwa sababu itapelekea mikusanyiko mara dufu na mikusanyiko hiyo itatokana na waandamanaji walio kosa chakula

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…