Wewe si unajua takwimu zilipo mzeiya, lete hapa ili tuthibitishe na wewe utakuwa sahihi zaidi ya wengine ambao tunaamini hakuna Corona kwa sasa. Data ziko external kama unavyosema, maana tayari una access ya huko ziliko, please zilete hapa tuone, mbona ni rahisi tu.
All in all, kuongea bila facts ni kusaidia kuleta panic na kupotosha umma, taarifa na tahadhari uliyotoa ilitakiwa kutolewa na mamlaka as wao ndio walikuwa na takwimu sahihi. Hivi unajua kuwaambia watu wanunue vyakula na maji ya kutosha, huenda wachukue fedha za kutosha na kuziweka nyumbani tayari ungeleta taharuki katika jamii? Unajua ungesababisha panic na uhaba wa bidhaa muhimu pamoja na vyakula? Kwa nini wewe ambaye huna mamlaka ulitoa tahadhari ambayo huenda ilitakiwa kutolewa na either waziri mkuu au waziri wa afya?
Unajua watu wanakuandama kwa sababu uliandika kitu usichokijua na bahati mbaya hujui kama hukujua, to-date bado hujui kama ulichoandika hukukijua. Mstaarabu akivuliwa huchutama.