Kuna uwezekano Watanzania tuna tatizo la uelewa? Nikimsikiliza Polepole, namuona Mwl. Nyerere. Nyie msiomuelewa Polepole, je Nyerere mngemuelewa?


Mengine yoote wafananishe lakini, fahamu kuanzia leo kuwa misimamo ya Mwalimu Nyerere haikuwa SEASONALLY.
Maana yake, wakati anacho au ana uwezo wowote na wakati hana au hana uwezo wowote.

Kwa fikra na matendo yake:
1: Polepole wa bunge la katiba alikuwa tofauti na 👇
2: Polepole wa utawala wa Mh. Magufuli, nae Polepole huyo yuko tofauti katika misingi hiyo na 👇
3: Polepole wakati wa utawala wa Mh. Samia 👇
4: Tutarajia Polepole mwingine ajaye??

Tafakari kwa kina.
 
Kama ulivyokwisha kusema kua watanzania tuna matatizo yakutoelewa.. naam ni imani yangu kubwa kua na wewe ni Mtanzania ndio maana unathubutu kumtukana Mwl. Nyerere kwa kumfananisha na mwanasiasa wa hovyo kama Polepole.

Mwl alieichukua nchi ikiwa kwenye mfumo wa chama kimoja ila alivumilia kuona ikiwa ya vyama vingi leo hii hawa wahuni wachache wanaotamani kuangamiza mifumo ya ki demokrasia na hata kuua upinzani na kunyamazisha wanaohoji ndio unadhubutu kuwafananisha na waasisi wa hili taifa?

Tuongeeni kwenye uhalisia mnadhani hiki kizazi cha nne na cha tano cha siasa za tanzania kama nchi ingrkua iko bado kwenye mfumo wa chama kimoja hawa wenaosema wanashuhulikia wahuni unadhani wangeachia nchi? Na ikulu ingejengwa kanda ya ziwa walah
 
@paskali mayala
 
ndo maana nikasema watanzania wana ugonjwa wa kusahau. wameshasahau yote, kumbe ni mwaka jana tu hapa kulikuwa na uchaguzi.
 
Polepole sio mjamaa wala hajui ujamaa, ni msaka tonge kwa kutumia kalamu yake.

Nyerere aliwafananisha na mercenaries yaani mamluki. Yeye anafuata dau tu ndio unakuwa msimamo wake"He who pays the piper calls the tune".

Anachofanya sasa hivi ni sampuli ya kinyonga, ila anasahau kubadirisha misamamo hakubarishi genetical make up yake.
 
Hakuna shetani mwema kwa binadamu, hao wote uliowataja ni mashetani tu.
 
Huyu mtoa mada ndiye aliyesema Makonda anafaa kua rais wa nchi hii,. Kweli huyu mayala mayala yanamsumbua mpaka kwenye ubongo
Mkuu Robidinyo , hili bandiko linakuhusu, mkiitwa vilaza mnalalamika!.
Nenda kalisome tena bandiko hili huku ukishirikisha ubongo wako, only if kwenye kichwa chako kuna ubongo
Lakini kama unajijua kichwani ni an empty shell, please just save your time, don't!.
P
 
Dikteta alituambia mayala maana yake ni njaa
 
...alituambia mayala maana yake ni njaa
Ni kweli, ila sio njaa za tumbo inayohitaji shibe ya chakula ni baa la njaa, drought, famine, iliyosababishwa na ukame, inayohitaji mvua!. Alhamdidulahi, sasa mvua zimeanza kuonyesha!, maana...
P
 
Ukiwa mwanasiasa muda mwingine unalazimika tu kujifanya huna akili kumbe unazo, hii hoja ya Pasco ni mojawapo ya hoja za hovyo, zenye upofu na upogo, na utovu mwingi wa nidhamu!
 
imagine, haujawahi kua mbunge tangu uzaliwe, Rais Samia anakuteua ubunge wa bure ambao hata sio wa kupigiwa kura, unakula mshahara na marupurupu, usafiri everything, afu siku moja from nowhere unasikika ukiutangazia umma kwamba, wakitaka kukupora ubunge wachukue tu hauwaogopi. hivi kuna wangapi wangepewa nafasi yako hiyo ambao wangekuwa hata na adabu? wakati huo yule aliyekuteua hajakujibu wala nini na ni mtu mwenye mamlaka makubwa. vijana ndio maana wanashindwa kuaminiwa. vigeugeu sana.
 
Pascal mayala anaona mbali...one dei the team will rise and the dead will arise again
 
Vip mkuu kampeni za kumfanya homeboy kolomije boy awe prezidaa wa sita wa wadanganyika zimefikia wap??!!
Ahaa... kumbe na wewe uko kundi la vila...?!. Kanisome tena huku ukishirikisha ubongo wako!.
P
 
Nimesoma mkuu; kwamba homeboy kolomije ni mdhubutu kuliko hata dikteta hivyo ndo mwenye sifa ya kuwa lais wa 6; kama hiyo haitoshi kiloboto ana akili kama nyelele (au pengine kumzidi?!!); vip unapendekeza kiloboto awe lais wetu wa 7 baada ya homeboy kolomije?!! Kwa sababu wachunga ngombe ndo wengi basi ndo wenye haki ya kutawara mpaka hapo maeneo mengine nako watakapokuwa wengi... Duh! Ila ma homu boizi mna loho ngumuuuu!!!!
 
Sijui kwa nini Pasco, kila mara, watu waovu, yeye anaona ndio wanaofaa kuwa viongozi.

Habari za ndani kabisa ni kwamba Polepole ndiye aliyekuwa akiandaa majina ya watu wanaotakiwa kushughulikiwa na watu wasiojulikana. Walitekwa na kurundikwa chumba kimoja cha mateso, ghorofa ya 5, ofisi ndogo Lumumba. Baada ya mateso makali ama walikabidhiwa polisi au wasiojulikana waliwachukua, na baada ya hapo, kuonekana kwao ilikuwa ni maajaliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…