Kuna vitu huwa vinakera sana na kushangaza kwa baadhi ya wafanyabiashara wanavyofanya biashara zao

Kuna vitu huwa vinakera sana na kushangaza kwa baadhi ya wafanyabiashara wanavyofanya biashara zao

aisee aisee kuna huyu mama nlikua nanunua mihogo kwake, nikaja kuacha kidogo, siku moja nikakutana nae akaniambia 'unadhani bila hela yako nashindwa kuishi??' nilikwazika sana 😂

Nawasilisha.....
😀😀😀Ungemwambia mm pia sili mihogoyako michungu🤣🤣
 
Kuna wafanyabiashara hasa wale wamama wa masokoni ..huwa wanajisifia kabisa kumshushua mteja...
Utasikia Leo nimempa makavu ...
huko sokoni ndio kumeoza kabisa wanakunyooshea kidole kabisa. Niliwahi kula kwa mamantilie mmoja baada ya mda nkaacha, siku kaniona akaniambia utahangaika sana kula kwingine mwishowe utiliwe sumu ufe, nikabaki nashangaa maneno yote hayo ya ninini
 
Kuna duka niliwah enda muuzaji kanunaaaa. Sikumfatilia sana nikajua labda kavurugwa tu hiyo siku. Wakati mwingne tena nikaenda kanuna vile vile hee nikabaki najiuliza kwani hapa naomba msaada ama natoa pesa? Nikatoka bila kununua kilichonipeleka.
 
kabisa maana wateja wanakera ila unachopaswa kujali ni maslahi ya biashara yako.
Kweli mm nilipata changamoto ya msaidiz wa ovyo yaani wateja nisipokuwepo wakija wanaondoka had niwepo niwahudumie au tukiwa wote wateja wanakuambia hatumtaki huyo km ukobusy nisubir au Nije wakat mwingine lkn nikagundua wengi hawana kauli nzuri Kwa wateja ni changamoto
Niliposafiri nikakuta wateja wote wamehama😀😀
 
Kuna duka niliwah enda muuzaji kanunaaaa. Sikumfatilia sana nikajua labda kavurugwa tu hiyo siku. Wakati mwingne tena nikaenda kanuna vile vile hee nikabaki najiuliza kwani hapa naomba msaada ama natoa pesa? Nikatoka bila kununua kilichonipeleka.
Inasikitisha sana
 
Mie KUNUNA tu yaan unaenda DUKANI unamkuta mtu KANUNA kila ukimuongelesha anakujibu kama vile mna UGOMVI au anakupa msaada yaan MTEJA unaonekana msumbufu

Sasa ulilazimishwa kufungua DUKA si ufunge
Mm huwa nawatukana tu na Bidhaa kuniuzia utaniuzia tu kilazima lbda iwe sehemu amabayo siwezi kuifikia
watu wana stress na wengine ndio vile "maskini akipata matako hulia mbwata" wanamajivuno sana
 
Kuna wafanyabiashara hasa wale wamama wa masokoni ..huwa wanajisifia kabisa kumshushua mteja...
Utasikia Leo nimempa makavu ...
Halafu utakuta nauza matembele na mchicha
au NYANYA katandaza Chini dah !!
Tuna SAFARI ndefu y kustaarabika

Mbaya zaidi ukute ndo katoka KUVUNJA KIKOBA au ndo kapokea MCHEZO(upatu) yaan MAKAVU live na kisha anashushia cheko fulani hivi amazing la kukela ile unainua mguu tu unataka kuondok
anamalizia na kwendraaaaaaaa
 
Kuna duka niliwah enda muuzaji kanunaaaa. Sikumfatilia sana nikajua labda kavurugwa tu hiyo siku. Wakati mwingne tena nikaenda kanuna vile vile hee nikabaki najiuliza kwani hapa naomba msaada ama natoa pesa? Nikatoka bila kununua kilichonipeleka.
huyo itakuwa ndivyo alivyo mimi mwenyewe sipendelei kupata huduma mahali ambapo mtu anajinunisha kama ana mimba changa
 
Kuna duka niliwah enda muuzaji kanunaaaa. Sikumfatilia sana nikajua labda kavurugwa tu hiyo siku. Wakati mwingne tena nikaenda kanuna vile vile hee nikabaki najiuliza kwani hapa naomba msaada ama natoa pesa? Nikatoka bila kununua kilichonipeleka.
sasa unaeza kuta hicho kitu unatafuta, kinapatikana duka hilo tu hapo mtaani 😂
 
huko sokoni ndio kumeoza kabisa wanakunyooshea kidole kabisa. Niliwahi kula kwa mamantilie mmoja baada ya mda nkaacha, siku kaniona akaniambia utahangaika sana kula kwingine mwishowe utiliwe sumu, nikabaki nashangaa maneno yote hayo ya ninini

Kuna restaurant nilikuwa napenda Kula ..siku moja nafika na kuna jamaa kamaliza Kula anaondoka...nikashangaa mama WA hapo anamuanzishia story jamaa ...kwamba hajabadili suruali siku ya pili ..sikurudi tena pale
 
Back
Top Bottom