Kuna vitu huwa vinakera sana na kushangaza kwa baadhi ya wafanyabiashara wanavyofanya biashara zao

huyo itakuwa ndivyo alivyo mimi mwenyewe sipendelei kupata huduma mahali ambapo mtu anajinunisha kama ana mimba changa
Ndio alivyo nilipata kusikia malalamiko kumuhusu toka kwa watu wengne anajinusha hivyo hivyo. Nikishajua mahala wana huduma mbovu huwa sirudii kwenda. Yaan unaenda sehemu utadhan unaomba msaada wanavyoringa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa nilikuwa na bimkubwa Kariakoo akanunua kibao cha kukatia nyama tusikatie kwenye vibao vya plastiki, kumbe muuzaji huu anaodai ni mninga kaupaka varnish. Unapakaje varnish kwenye vyombo vya chakula, mtu anakwepa plastiki anakutana na varnish. Unakwepa nyama unakutana na mbogamboga zenye madawa, hapo umekimbia obesity ukakutana na toxins
 
lazima wahame, kauli ni muhimu sana kwa wateja wengi wanadhani kutoa huduma tu inatosha kumteka mteja.
 
Kuna duka la mtumba lilikua kahama .Aisee jamaa lilikuwa jivuni lile .Ukija linakucheki kama umepauka pauka hata haliinuki .Utaambiwa chagua unachotaka ukiuliza hii sendo bei gani? Linajiropokea mabei ya kujua lenyewe tu .Utasikia hiyo laki tatu na ishirini.Jivuni kweli lile fanyabiashara kama limelazimishwa.
 
Ndio alivyo nilipata kusikia malalamiko kumuhusu toka kwa watu wengne anajinusha hivyo hivyo. Nikishajua mahala wana huduma mbovu huwa sirudii kwenda. Yaan unaenda sehemu utadhan unaomba msaada wanavyoringa.

Sent using Jamii Forums mobile app
mtu from january to december ni kujinunisha tu alafu akipoteza wateja aseme kalogwa
 
Kuna restaurant nilikuwa napenda Kula ..siku moja nafika na kuna jamaa kamaliza Kula anaondoka...nikashangaa mama WA hapo anamuanzishia story jamaa ...kwamba hajabadili suruali siku ya pili ..sikurudi tena pale
tatizo la wamama wengi wa mtaani wanapenda sana umbea na kujua maisha ya watu. Ukishaona mtu kaondoka akasemwa tafsiri yake hata wewe ukunyanyuka ukaondoka watakusema vile vile.
 
hiyo ina madhara gani mkuu?
 
kuna watu kwa majivuno wameshindikana plus dharau. mtu hana uwezo au wa hali ya chini ni yeye mhudumie aende na maisha yake kikubwa kamudu kulipia huduma.
 
Katika miaka yangu 7 ya kubank na CRDB nimewahi hudumiwa mara 1 vizuri na mdada mmoja mzuri mweupe kama mimi, wa CRDB Chamwino-Dodoma. Yule dada alinihudumia nikaridhika nikatoka bank roho nyeupe. Wengine bwana! Kwanza mtu anaongelea tumboni, wako moody muda wote khaa!

Bank yangu ya sasa sijawahi pata expirience ya huduma mbaya.
 
kumbe wewe ni mweupe, hongera. Huko benki wadada wengi mashauzi sana hasa hiyo benki uliyoitaja.

wapi huko umehamia tukimbilie kutafuta ahueni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…