Aiseee biashara inachosha inafikia mahali kuna kauchovu fulani huwa kanajitokeza
inachosha zaidi kila siku uko pale pale haikui na gharama za uendeshaji zinazidi kupanda. Biashara sio kwa kila mtu zinahitaji uwe mvumilivu na mwenye nidhamu ya fedha kweli kweli.
Biashara ni sanaa, taaluma na sayansi kwa pamoja. Ni fani inayojitegemea yenyewe. Ni sehemu ya maisha yetu isiyokwepeka.
Mtu asiyeweza kufanya biashara, kimsingi hapo maisha yamemshinda tayari.
Ukichushwa (kuwa bored, kupoteza real, enthusiastic business energy ama stamina) kwenye biashara yako, it means huna malengo bora ya maisha, kwa sababu malengo makini humfanya mtu awe lively, winsome, na optimistic wakati wote.
NB: 1. Hapa sizungumzii
kuchoka bali
kuchushwa (kupoteza interest, hamasa, shauku ya kuendelea kufanya biashara yako).
Mtu anayeipenda biashara yake aliyoi-plan vilivyo, hata akichoka, asubuhi yake ataamka akiwa na nguvu mpya huku akijisikia yuko fresh tayari kuruka, afike ofisini kwake kwa wakati na kuifanya biashara yake kwa ubora kuliko jana.
2. Hata kama biashara inaweza kuyumba fulani (and it happens to all business people), bado mfanyabiashara anaweza kuwa na hamasa halisi ya kujitathmini, kufanya mabadiliko husika na kusonga mbele kwa ufanisi zaidi.
3. Mfanyabiashara wa namna hii anawapenda wateja wake, nao pia wanampenda yeye. Kwa nini, kwa mantiki hiyo, usifanikiwe sasa, hata kama biashara yako imepakana kabisa na ngome kuu ya
Iblis Bin Shetan ?