Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Haaaaaaa [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] duu ulipataje aibu, sasa nawewe kwanini ulikuwa unaenda karibu na nyumbani haaa haa mtoto huyo noma , pole sana!
 
Sasa mgahawani na pesa uwe nayo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kuna watu hadi ukitoka nae hapo unajiapiza huyu mbwa sitakwenda nae popote siku nyingine. Mtu anakula as if amekuja duniani kula tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mgeni wa hivyo shida jamani kuishi naye, ni jamaa mmoja uwii akija halafu kanizoea ni muda wote kula kama nzige, Baba mwenye nyumba huwa ananitizama tu ninavyohaika naye kumpikia haaa haaa hata sijui na kwa wengine akienda haa haa haa!
 
Watu wa hivyo very selfish.
Sana...
Nina wifi yangu ndiyo zake hizo, yeye hajali wenzake anapakuwa mboga nyingi wengine mtajua wenyewe. Siku hiyo nikamwambia wakati wa kula uwe unafikiria na wenzio.
Kakasirika kasema kwao na rafiki zake mimi nimemwambia anakula sana, basi saivi anakula chai nusu kikombe, km ni mkate slice1,chakula vijiko km 5 kashiba mpk kapungua.
Imeniuma sana najuta ht kumwambia vile ijapokuwa inakera sana
 
Mara nyingi wakosaji wakikosolewa wanaumia mno na kuona wameonewa. Sasa huyo si anajitesa tu bora angekubali kubadilika kuliko kufanya hasira kisa kaambiwa ukweli
 
Usitilie shaka wala kujiskia vibaya kumkanya mtu anapokuwa na tabia mbaya. Tabia mbaya kukemewa ni lazima na mtu mwenye tabia mbaya hatakiwi kukasirika hata iweje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara nyingi wakosaji wakikosolewa wanaumia mno na kuona wameonewa. Sasa huyo si anajitesa tu bora angekubali kubadilika kuliko kufanya hasira kisa kaambiwa ukweli
Ukiambiwa ukweli unapofanya makosa, yale maumivu, hasira, ghubu na kisirani ndio tabia mbaya inatoka pale so inabidi ujifunze tabia mbadala ili uwe mtu safi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara nyingi wakosaji wakikosolewa wanaumia mno na kuona wameonewa. Sasa huyo si anajitesa tu bora angekubali kubadilika kuliko kufanya hasira kisa kaambiwa ukweli
Kwa kweli tumeumia wote. Ila tunamtizama tu
 
kwa hyo mtu kula huku anatumia simu nalo ni tatzo duuuh,,, mbona maisha simple ila nyie mnataka kuyafanya yawe complicated sana
 
Kuna baadhi ya watu bado haiwasaidii.
Bado wanaulimbukeni wa chakula.
Yaani akitoka akala au akapika kitu kizuri anaona siifa hadi anatangaza.
Mimi hii kitu alinifundisha bro wangu. Nilikuwa na shobo saba na nyama. Na vyakula fast food kama soda, biscuits keki, etc, nilipoanza kazi, na kuanza kujitegemea nikawa navila hivi vyakula kwa uroho.

Nikaanza kuvizoea na kuviona vya kawaida sana. Ikafika moments naweza kwenda kwa mtu akapika nyama ya kuku mimi nisipate hata hamu ya kula hata kipande maana naona ni kitu nimezoea na kimenikifu.

Soda ndio kabisa.... Nikawa nikienda sehemu yoyote tumetoka mimi nitaagiza maji ya kilimanjaro chupa kubwa sababu sina tena hamu na vinywaji vingine vya kiwandani.

Plus mwili nilianza kuongezeka na kutanuka so ikawa kwangu ni shida kiafya.

So taratibu nikaanza diet. Nikienda kwa mtu nikikuta kapika maboga.... Dah nayachangamkia maana ni chakula cha afya.

Ila mayai, maziwa fresh, mtindi, Sausages, nyama ya kuku, chipsi, nyama kawaida, kitimoto, aaaah speed ilikuwa ndogo sana nilikuwa naona mzigo kuvitumia.....

So sometimes watu ni kukosa enough amount ya hivi vitu inawafanya kuwa na uroho navyo na kuleta tabia za Ulafi wanapo viona.

Mimi hiyo tabia imenisaidia sana hadi imefika hatua nimeanza kujua kujicontrol. Naweza kwenda sehemu nina njaa ya kula sana na nikaweza kula kidogo maana najua nikitoka hapa nitaweza kutafuta hivi vitu nikavila....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli nakumbuka wakati wetu sinia lina wekwa hapo limejaa wali harage lime mwagwa juu watu tuna lifinyaaa likiisha tunaulizana jamani mmeona?tunajibu bado ngoma linapigwa la pili tuna kulaa hapo anaanza mmoja mmoja kuinuka ujue watu wameona sasa!!
 
Huyo mama wa kula haraka nadhani atakua kakulia nakuolewa uswahilini aisee
 
Sio watu wote walifundishwa nidhamu ya mezani (table manners) wasamehe tu malezi pia yanachangia
 
Hivyo nibkuharibu watoto...
Tabia hiyo inaendelea mpk ukubwani. Sasa ukiwa kwa watu unatia aibu
Ndio maana sisi nyumbani tunapakua kwenye sinia kubwa kila kitu ni spidi yako tu na efficiency, na bahati yako kukaa upande mzuri utaweza kufaidi vinono. Shika smartphone uone kama utapata kitoweo
 
Kaka hapo kwenye shemeji umenipatia nilishapata kumuona kima mmoja mwenye tabia hizo.
Kama hatokei Kigoma Basi Ni Kanda ya ziwa.
Atakua aliongea na chakula mdomoni.
Hajui matumizi ya Uma, kiwiko Cha mkono wa kushoto kukitwa mezani.

There is a manual for table manners
"Complete table etiquette" download and read for free.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…