Kuna wageni ambao hawana ustaarabu mezani saa ya chakula

Tatizo si kupika kidogo, inawezekana wako wengine jikoni lakini ustaarabu ni kuhakikisha kilichotokea mezani kila mtu amepata na nyongeza ni ziada.
 
Mtoa mada punguza roho za njaa , wanawake vyakula vinawapaga stress.
Wewe unasema tu kwakuwa ni mwanaume, ila kuna wageni siyo wastaarabu kabisaa, na hapo ndo unaanza kuona mama mwenye nyumba mbaya kumbe mbaya wewe ambaye hujatumia ustaarabu kuto jali wengine vitu vinaenda kwa bajeti tena samaki walivyo bei halafu hawagawikagi unakuta watoto wanaambulia macho ya samaki kisa wewe mgeni

#kama mpo wengi nyumbani pika nyama ili kuepuka shari#[emoji16]
 
We ukija kwetu utaishi kwa tabu sana

Bi mkubwa wangu ukipakua paja moja la kuku anakuongezea yeye mawil..hahahah..hata muwe wangap kwenye meza.....sasa sis wengne tumeendeleza hyo tabia..


Hahah natania.......ila kwel bi mkubwa wangu sis watoto wa kiume alikua anatuoverload mda wa kula sana...
 
Absolutely right,
Kuacha Table manner viko vingi vya kuchunguza na kuwafunza wenetu.

Nimewahi kununiwa na staff mwenzangu baada ya kumrekebisha kuhusiana na uchakuaji(utafunaji) mbovu wa chakula.

Ni tabia mbaya kutafuna Kama mbuzi,hufungi mdomo pia unaongea.
 
Sky Eclat Kupakua chakula bila kujali wanao baki ni ujinga wa kukosa malezi Bora kutoka kwa wazazi, muhimu kwamba kitu kinapo kuwa kidogo mnagawana kidogo kidogo ili kila mtu apate.

Ila Tabia nyingine ambayo siipendi ni kubakiza chakula kwenye sahani, Kuna watu kubakiza chakula kwenye sahani wanaona fashion, wanachukia kingi cha nini Kama hawawezi kumaliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengi wanatafuna Kama nguruwe sio mbuzi, mtu anatafuna mpaka nyumba ya nne wanasikia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona umeamua kutusema sisi akina mabula na maduhu
 
Sahihi kabisa mkuu
 
Ndio maana sisi nyumbani tunapakua kwenye sinia kubwa kila kitu ni spidi yako tu na efficiency, na bahati yako kukaa upande mzuri utaweza kufaidi vinono. Shika smartphone uone kama utapata kitoweo
 
Ndiyo maana leo huli bali unafukia, kumbe ulishazoeshwa na bi mkubwa wako kufukia, wewe hufai kukaribishwa na Sky Eclat, unafaa uje nyumbani kwangu ili uwe overloaded.[emoji1787]
Kabisa mkuu....na unawekaje samaki 8 exactly na idad ya wageni buana....weka misamaki yakutosha kama una wagen usibanie

Mi bi mkubwa wangu akiandaa meza aisee..mnaweza kula had mkatambaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…