Kuna wanaume wanaishi kwenye ndoa ngumu nyie

Kuna wanaume wanaishi kwenye ndoa ngumu nyie

Mimi najitegemea in fact, lakini hakuna maisha mazuri kama mke na mume kuwa marafiki, mume kumhudumia mke, na mke kumheshimu mume, naenjoy mume wangu akiniwekea vocha nikienda saluni lazima atauliza unataka sh ngapi kama nywele ni elfu 20 na ninajua siku hiyo hana kitu ntamwambia nahitaji 10 ingine nilimuachiaga dada wa saluni chenj yangu, au nyingine ntaongezea utanilipa. Mwanamke unaesoma hapa elewa hata upate vipi hela please usimnyang'anye mwanaume uanaume wake,(manhood) aidha kwa maneno au matendo yako au kwa kujigamba , maintain his man hood please.Huyo Mercy Mchechu alieongea hivyo amewapa sababu wanawake wandagaji kumtafuta mumewe.Tuna maisha ya kawaida lakini mgeni akija kwangu kwa anachokikuta lazima atajifunza kitu, utashangaa sasa limama lizima likija linaniita pembeni eti unanyenyekeaje mwanaume atakuja kukusaliti, wanadam wote wanasaliti, ishi ndoa yako Leo sasa hivi, kwamba ulisalitiwa ilishapita utasalitiwa haijatokea bado, kwa hiyo tunaweza kusema mengi kutaka umaarufu lakini UKWELI upo pale pale, Mwanamke anaeaga ana nafasi kubwa ya kuaminimka kuliko asiyeaga, anayepewa hela kulingana na kipato cha mumewe anapendwa zaidi kuliko asiyepewa.
You deserve motherhood compliment! I grant it to you. You know better how to cherish marriage. Congrats! Mrs. Executivesister
 
Mimi najitegemea in fact, lakini hakuna maisha mazuri kama mke na mume kuwa marafiki, mume kumhudumia mke, na mke kumheshimu mume, naenjoy mume wangu akiniwekea vocha nikienda saluni lazima atauliza unataka sh ngapi kama nywele ni elfu 20 na ninajua siku hiyo hana kitu ntamwambia nahitaji 10 ingine nilimuachiaga dada wa saluni chenj yangu, au nyingine ntaongezea utanilipa. Mwanamke unaesoma hapa elewa hata upate vipi hela please usimnyang'anye mwanaume uanaume wake,(manhood) aidha kwa maneno au matendo yako au kwa kujigamba , maintain his man hood please.Huyo Mercy Mchechu alieongea hivyo amewapa sababu wanawake wandagaji kumtafuta mumewe.Tuna maisha ya kawaida lakini mgeni akija kwangu kwa anachokikuta lazima atajifunza kitu, utashangaa sasa limama lizima likija linaniita pembeni eti unanyenyekeaje mwanaume atakuja kukusaliti, wanadam wote wanasaliti, ishi ndoa yako Leo sasa hivi, kwamba ulisalitiwa ilishapita utasalitiwa haijatokea bado, kwa hiyo tunaweza kusema mengi kutaka umaarufu lakini UKWELI upo pale pale, Mwanamke anaeaga ana nafasi kubwa ya kuaminimka kuliko asiyeaga, anayepewa hela kulingana na kipato cha mumewe anapendwa zaidi kuliko asiyepewa.
Unadhani nin ni wajibu wa mwanaume kweny mahusiano?
 
Huyo mwanamke sidhani kama ana mume, hii ni dharau kubwa sana kwa mwanaume, mawifi mpaka kwa wakwe zake. Kama ana akili timamu na ana mume bhasi atakuwa amekengeushwa kuongea hayo mbele ya hadhara ya wanawake wenzake. Au alijua labda itaishia hapohapo ukumbini?!
 
Sasa hapo huyo ndio kaonekana wa maana wa kuwafundisha wenzie kwenye huo mkutano mpaka mc akampa mic. Yani sijui kasahau au hakumsikiliza raisi samia aliesema yeye pamoja na uraisi wake ila mbele ya mume wake anapiga goti.

Nafikiri kutokana na wanawake wengi kuishi single wakishafanikiwa kifedha sasa wanawadanganya wenzao walio kwenye ndoa ili nao wawaletee kiburi waume zao watimuliwe ili nao wabaki pia single.
Ni Kweli wanawake wanaoshi Single wanapenda sana Kuona ndoa zinavunjika Kwa wingi sana Ili wapate MAHALI pa kudanga na kupata huduma ya kupigwa shoo. Kwa Maana kwamba pakiwa na Ndoa zilizotulia na vijana wakioa na Kutulia na wake zao ni Wazo wawake wenye KAZI zao na pesa zao wangewehuka mana wangekuwa hawapati huduma ya ngono kirahisi . Kwa Sasa wanawake wengi wanajeuri mana wanajua kwamba wamevuruga ndoa nyingi sana na wanawatumia vijana wasio na Ajira kingono na watu maarufu Ili kujipa uhakika Wa kuendeleza jeuri Yao.

Huyo mdada ni Mjinga. Ndoa ni taasisi kwenye jamii ambayo Ina watoto wanaohitaji malezi ya baba na mama . Sasa ukiona MTU anachochea kuvuruga taasisi huyo MTU ni Wa kumwogopa sana . Angekua na biashara nadhani Hata wanaume na wanawake wenye Ndoa zao wanatakiwa kususia biashara yake.

MTU kama huyo Hata ukimwajiri ni shida sana . Wengi wanaajiriwa na mahawara wao au wanatembea na mabosi au wamiliki Wa kampuni. Hii ni Ili wawe na jeuri mpaka KAZINI. Mfanyakazi mtiifu Kwa Bosi wake hua Hata mumewe anamtii lakini Mwanamke akishaanza Kutembea na mabosi wakubwa Kama Wakurugenzi,mawaziri n.k. anakua jeuri mpaka Ofisini anaweza akaondoka tu na kuwaacha wateja au Hata kujibu Kwa nyodo mana anajua hawezi kufukuzwa KAZI .

Hivyo huyo dada ni Mfano Wa wanawake wapumbavu wasio na busara wanaowaza ubosi tuu. Bila kujau kuwa Bado ana safari ndefu ya maisha. Na asitegemee kuwa ikatokea anapata tatizo la,kensa ya kizazi (ambayo huko tuendako itakua kubwa sana kutokana na wanawake kubadili wanaume Wa aina Tofauti Tofauti kama fasheni na wengine kuhiingizia mpaka midoli kwenye Uke) au tatizo la Figo kuna MTU Wa vikoba na vikao vya harakati atamsaidia zaidi ya Mume wake na Wazazi wake kama wapo.
Ndoa kama Taasisi inahitaji kuwa na Kiongozi anaseheshimika na kuwa dirá na kichwa Cha taasisi hiyo.

Tukiwa na taifa lisilo na watu wenye Ndoa imara basi Hata uadilifu utapungua sana . Ndio Maana Leo watu wanaiba mabilion ya pesa kwenda kula Bata na mahawara zao. Watu wanapeana Ajira Kwa rushwa za ngono. Digrii zinatolewa Kwa rushwa ya ngono mana hakuna anayeheshimu mahusiano zaidi ya kukidhi matamanio yake ya kingono.
Nchi imevamiwa na Pepo wabaya sana . Hata upagani Ulikua na miiko kwenye suala la mahusiano ndio MAANA watu waliweza kutambika na mvua zikanyesha mana Mungu yupo sirias sana kwenye suala la mahusiano hasa wanawake kutii na kutunza familia . Mungu anawajali sana wanawake watiifu na waaminifu mana Mwanamke ndio Kiwanda cha uumbaji Wa Mungu. Sasa Kiwanda kikiwa kibovu basi kimakua hakina thamani na faida Kwa mmiliki .
 
Yule mwanamke mpumbavu ni mke wa Nehemiah Mchechu, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nyumba (NHC) sasa Msajili wa Hazina

Sijui Mchechu anaishije na mwanamke asiye na heshima kwa mume kama yule. Kwa kauli ile kamdhalilisha sana mumewe
Duuh, ni Noma sana . Lakini ndio janga la Dunia Kwa Sasa . Sidhani kama ana pesa kama Hata theluthi ya pesa aliyonayo huyo mumewe. Ni ulimbukeni tu na ujinga. Akiachwa halafu mumewe akaoa Mwanamke mwingine Wa Kitanga au Kiarabu Fulani amazing,mwenye kukulia kwenye Dini hasa na kujua Maana ya ndoa kidini Hapo atatia akili. Kama ni Mkristo basi Hapo ni janga Kwa kweli mana Wakristo wengi wameamua kumtumikia Shetani Ili wapewe milki na fahari yooote ya Dunia. Walianzia Edeni kutaka kuwa Sawa na Mungu Ili wasiombe ruhusa Kwa MUNGU Wala Kwa mumewe Adam. Ikashindikana kuwa kama Mungu.
 
Huyu dada Mercy Luhanga. Mke wa Nehemia Mchechu. Ngonja nikamnyakie Mchechu nimpe heshima zote na mapenzi kama yote. Hahahhaha.Mbona Mercy atatia akili.Jamani ninatania tu,nimeokoka siwezi iba mme wa mtu.
Bandika bandua. Mwanamke Gabi huyo Ana mume mwenye mijihela na umaarufu kama NM halafu anamdhalilisha Kwa kiwango kile. Daaah,hatari kubwa kwenye jamii .
 
Hivi yule aliyesema, "MWANAMKE AKIPEWA SAUTI, MAMLAKA...BASI MAMBO YAMEHARIBIKA...JAMII AU FAMILIA INAYOMPA UONGOZI MWANAMKE JAMII HIYO HAITOFANIKIWA KAMWE."

Hivi mnadhani yake yalidondoka bure...?
Kwani ni uongo !!

Wajanja Wachache wanatumia Mwanya huo kufanikiwa lakini jamii au familia Kwa Ujumla wake inaelekea kubaya. Si ulisikia kuwa ukiona Mwanaume anakusumbua achana Naye. Kauli ya wakubwa hua inasikilizwa sana. Na kauli ya wakubwa Ina ulinzi na Sheria ndani yake!.

Tutegemee Mengi sana kwenye nyakati Hizi za muNGU Wa mchongo Mwanamke baba Zumaridi.
 
Nimeona video mtandaoni mwanamke mmoja kwenye party ya wanawake wenzake anajigamba kwamba ametoka nyumbani kwake hajaaga ila kampa mumewe taarifa tu kwa vile tu yupo financial stable.

Imagine mke wako anajitapa hivi mtandaoni uko ndani hali ikoje mkeo anatoka kwako bila taarifa how, si anaweza hata kulala nje ya nyumbani bila taarifa kuna ndoa kweli hapo.

Wanawake wa hivi wengi ni onjeshaonjesha
 
Mnapaswa kujua huyo mama yupo hapo kumuwakilisha shetani.

Siku hizi hao wamama hawana hofu hata na Mungu, wanakwambia mambo ya kuolewa yamepitwa na wakati kila mtu anaamua mwenyewe aolewe au aoe mwanamme (kula kulala or kiben ten).

Ndoa kwao siyo muhimu, wanaendesha maisha eti kwa sababu wana uwezo kifedha so pesa inaweza kuwapa chochote wakitakacho hata watoto.

Wanakwambia mume/NDOA ilikuwa zamani, sasa hivi maigizo.

Hapo kwenye hiyo event pale mbele angalia kuna mwanamme pale anajichekesha kwa kujilazimisha, hadi anajigeuza kama anafurahi but imemuumiza anajua siyo sawa ila kwa sababu kazungukwa na mashangingi hao hawezi sema kitu sababu atazomewa!.

[emoji419] Teundelee kujifunza tabia ya mwanadamu.
Ni Kweli lakini wanaume nao wamezidi ubinafsi na ujinga. Kila anachokilazimisha Mwanamke kina madhara Kwa Mwanaume awe KIJANA au Mzee. Wabaume hawashtuki tu na kuamua kuunda umoja wao imara na kutengeneza Hata Clubs mbalimbali za michezo na kuinjoi maisha Badala ya ulevi tu na kuibiana wake na kudhalilishana matokeo yake ndo zikivunjika watoto wanaegemea upande Wa mama na mwishowe baba anapoishiwa nguvu anakosa Msaada Mwisho anakufa Kwa msongo Wa Mawazo.

Wanaume wanapaswa kuamka na kuwakataa wanawake magumegume wanaojifanya wanapesa au wasomi Wa digrii au Ajira za Chupi!!
 
Wajanja Wachache wanatumia Mwanya huo kufanikiwa lakini jamii au familia Kwa Ujumla wake inaelekea kubaya
Mtu wa namna hiyo unaweza kuona asubuhi amegongwa Bonyokwa, mchana Tabata, Ubungo, Tangibovu, jioni anamalizia Mbezi akifika nyumbani hoi, mume akiomba unyumba ananyimwa na hawezi kusema kitu asikilizwe
 
Huyu anaamini kuwa free kipesa ndo kumdharau mme wako?Binafsi ukiwa free kipesa ni kusaidiana katika majukumu. Na si kumdharau mwenzako. Sema wanawake wenye ndoa za kikristo wengi wanadharau,wanajua mme hawezi ongenza mke mwingine.
Imekuja kubainika kuwa kile kilichoitwa Ukristo wa mchongo Ilikua ni mbinu za Shetani kuliangamiza Ulimwengu.
Haiwezekani karibu asilimia 90 ya taratibu za makanisa Yote hautokani na Biblia . Yaani Kila utaratibu ndani ya makanisa umewekwa na wazungu tu hiko ULAYA na Marekani(Kwa wapentekoste).
Matokeo yake taratibu za mchongo zinafeli na kuacha Ukristo usio na Wakristo waaminifu na watiifu kama alivoelekeza Yesu Kristo.
 
Back
Top Bottom