Na nyie huwa mnachekesha muda mwingine. Mwanamke mmoja unakuta kwa siku anaombwa namba na wanaume hata kumi kwa hiyo awe anatoa tu kisa kuwaridhisha nyie? Akitoa namba kwa hao wote mnamuita malaya, akikataa utaskia kauli kama hiyo yako hapo juu.
Alafu kingine kinachonichekesha unakuta mwanaume anaelalamika hajapewa namba utamskia ooh usipoolewa usirudi kunitafuta kana kwamba ana sifa hata kidogo ya kuwa mume kumbe ni muhuni tu. Kuna muda muwe mnavaa viatu vyetu tunatongozwa na wengi hatuwezi gawa gawa namba kama njugu eboo nyie vipi???