Mufti kuku The Infinity
JF-Expert Member
- Sep 21, 2019
- 6,053
- 10,032
- Thread starter
- #461
Mkuu, hii series sio poaDah,
Umenikumbusha aisee.
Kwenye jumong bana umenikumbusha Prince Taesso na na Prince Youngpo. Jamaa walikua hawampendi Jumong wakamfanyia kila aina ya vitimbi vya kutosha tu ila mwishoni aliwadhibiti.
Wapi chawa wa Jumong Oi, Mari na Hyoppo. Vibaka wa mtaani waliokuja kugeuka kua mawaziri kwe serikali ya Jumong.
Na mwisho ni swahiba wangu na rafiki yangu wa damu kabisa Cha Pombe Mo Palmo, mtaalam wa kutengeneza Silaha. Huyu loyalty yake kwa Jumong ni undoubted.
Hii series pamoja na kua na episodes za kutosha lakini niliiangalia kwa kuirudia zaidi ya mara tatu. Mwanzoni nilikubali mateso ya ITV niwe nakaa macho mpaka saa tano za usiku ilivyotoka.
Ila baadae alosto yake ilivyozidi nikaja kuzikuta zinauzwa kariakoo unanunua DVD moja ina episodes kama 10 hivi nikairudia.
Mi zipo kwenye PC, ni kuangalia tu muda wote 🙌🙌