Kuna watu kwa enzi hizi bado wanasikiliza mpira kupitia redio?

Kuna watu kwa enzi hizi bado wanasikiliza mpira kupitia redio?

Una uhakika tv zimesambaa kila kona?

Ww kuwa na tv ya inch 16 uliyobandika ukutani haina maana wote wana tv mana n gharama kuzidi radio huko vijijini
Unajua mimi kazi ilikuwa kutembea nchi nzima,na kwa miaka 12 nimetembea kila mkoa tena nikarudia kutembea kwa zaidi ya mara tano hivyo nimeona vijijini watu wakiangalia mpira kwa tv
 
Ukiwa dasilamu unaonaga nchi imeendelea sana , wengine wanasahau vijijini kwao wana share maji ya kunywa na punda kwenye ki dimbwi🤔🤔
Watu huko wanatembea km 30 kufuata maji/shule ndo aje aweze kumiliki tv na kisumbuzi chake, haiwezekani aisee.

Unajua mimi kazi ilikuwa kutembea nchi nzima,na kwa miaka 12 nimetembea kila mkoa tena nikarudia kutembea kwa zaidi ya mara tano hivyo nimeona vijijini watu wakiangalia mpira kwa tv
Kwahy hujakuta radio kabisa, mbona hata huko mjini Daslamu watu wakiwa kwenye shughuli zao wanatumia radio.
 
Ukiwa dasilamu unaonaga nchi imeendelea sana , wengine wanasahau vijijini kwao wana share maji ya kunywa na punda kwenye ki dimbwi🤔🤔
japo mimi sikai dar najua kuwa kuna vijiji bado havijaendelea lakini kuna maendele makubwa watu wana tv,zipo wamenunua wao,zipo wamenunuliwa na watoto wao lakini,hivyo vinavyoitwa vibanda umiza vipo vingi,na kuna watu wa mjini wamechukua hiyo fursa ya kutembea vijijini na tv na genereta kuonesha mpira
 
Mkuu kuna vijiji hamna umeme wala solar,kama unasema umetembe nchi nzima na wengi wana TV nadiriki kusema bado hujatembea umeishia tu kutembea mijini,mpenda soka kama hana tv lazima asikilize hata radio ili kujua matokeo na msimamo,mfano mdogo wewe hapo mjini umeme ukikatika,huna jenereta wala solar na mechi ya derby inachezwa je usingesikiliza radio?
 
Radio bado zinasikilizwa sana hata Benjamin Mkapa utakuta mechi inaendelea uku jukwaani mtu anasikiliza radio kwaajili ya kupata uchambuzi nk, kwangu nikiwa natazama mechi za kwenye TV uwa sikosi Radio kwa sababu ya ujinga wa TANESCO
 
Back
Top Bottom