Kuna watu kwa enzi hizi bado wanasikiliza mpira kupitia redio?

Kuna watu kwa enzi hizi bado wanasikiliza mpira kupitia redio?

TBCtaifa wanatangaza mpira wa ligi kuu na ile ya championship.

Hivi kuna watu bado,wanasikiliza mpira kupitia redio wakati Tv zimetapakaa kila kona?
Nadhani na mimi nitashangaa kuwa hadi hivi leo bado kuna watu wajinga kama wewe wanaoshangaa mpira kutangazwa redioni!

1. Kuna wasioona hawaangalii TV
2. Kuna walio vijijini ambako hakuna umeme
3. Kuna walio ofisini wanaendelea na kazi hawawezi kuacha kazi kuangalia mpira kwenye TV au simu
4. Kuna walio safarini ni dereva lakini anapenda mpira hawezi kuangalia TV au simu huku anaendesha.

Ni hayo tu
 
Mh! Kwahiyo mtoto akiwa wa kishua mjini anashinda nyumbani kwenye TV anahisi kIla mtu anaweza kuifikia TV kwa muda anaoutaka?

Kuna Watanzania wanabanwa na ratiba mpaka wa wanashindwa kwenda kutazama mpira inabidi wasikilize kwenye redio ya simu! Mfano, walinzi wa magetini, madereva.
TBCtaifa wanatangaza mpira wa ligi kuu na ile ya championship.

Hivi kuna watu bado,wanasikiliza mpira kupitia redio wakati Tv zimetapakaa kila kona?
 
TBCtaifa wanatangaza mpira wa ligi kuu na ile ya championship.

Hivi kuna watu bado,wanasikiliza mpira kupitia redio wakati Tv zimetapakaa kila kona?
Yes..
Mimi it's my preference..nikitizma kwa TV nakereka, wanacheza hovyoo,marefa wa hovyo .. Bora redioni.
 
Nadhani na mimi nitashangaa kuwa hadi hivi leo bado kuna watu wajinga kama wewe wanaoshangaa mpira kutangazwa redioni!

1. Kuna wasioona hawaangalii TV
2. Kuna walio vijijini ambako hakuna umeme
3. Kuna walio ofisini wanaendelea na kazi hawawezi kuacha kazi kuangalia mpira kwenye TV au simu
4. Kuna walio safarini ni dereva lakini anapenda mpira hawezi kuangalia TV au simu huku anaendesha.

Ni hayo tu
Tena ni zaidi ya mjinga! Labda Kama hapandi daladala,Ila kwenye madaladala dar asilimia kubwa tunasikiliza mpira
 
Bado tupo wapenzi wa kusikiliza redio,

Mfano, nusu ya Mechi za kombe la Dunia la 2006 Germany, nimezisikiliza kupitia redio na Charles hirari Mtangazaji.

Hivi Sasa Huwa nipo na radio Maisha Kutoka Kenya, watangazaji Steve Mkangai(baba Nora man of tactics , Nyota wa kumemetuka uwanjani,na Hassan mwana wa Ali (Japo kahama redio)

Bila kusahau vituko vya Amope vya Hassan mwana wa Ali.

Mfano wa kituko Cha Amope,

"Amope amekaa Miaka sita analalama hana kazi, ghafla bin vu Amope anabadilika viatu bei ghali, nguo bei ghali, simu bei ghali, nyumba bei, usafiri bei ghali, wenzake wanamuuliza mwenzetu unafanya kazi gani,

Amope anasema njooni niwaonyeshe, wanapokaribia kwake anafungua simu yake anawaonyesha mtandaoo wa betting, anasema Hii ndioo ofisi yanguu, hahaha "

Watu tumeanza kusikiliza redio, Idhaa ya kiswahili, Dw, Voa, R na nk, tukiwa vidudu,

Mpaka tumekuwa kama wa raibu.

Siku haiwezi kutamatika bila kusikiliza idhaa ya kiswahili hata Moja na kupata mbili tatu taarifaa na changanuzi za ulimwengu na matukio yake.
 
Back
Top Bottom