Kuna watu kwa enzi hizi bado wanasikiliza mpira kupitia redio?

Kuna watu kwa enzi hizi bado wanasikiliza mpira kupitia redio?

Tbctaifa wanatangaza mpira wa ligi kuu na ile ya championship,hivi kuna watu bado,wanasikiliza mpira kupitia redio wakati Tv zimetapakaa kila kona?
Mzee kuna wengine hatupati mda wa kucheki kwenye tv,wengi wanakuwa maeneo yao ya kazi so kufungulia redio na kusikiliza ni option yetu
 
Tbctaifa wanatangaza mpira wa ligi kuu na ile ya championship,hivi kuna watu bado,wanasikiliza mpira kupitia redio wakati Tv zimetapakaa kila kona?
Anakwendaaa....lunyamilaaa...hatareee hatareee....gooooo..gooooo...namnagani hapa mpira una gonga mtambaa panya na kurudi ndani kila anadaka kwa utulivu mkubwa sana 😊😊☺️☺️
 
Una uhakika tv zimesambaa kila kona?

Ww kuwa na tv ya inch 16 uliyobandika ukutani haina maana wote wana tv mana n gharama kuzidi radio huko vijijini
Tv inches 16 inatakiwa aiweke kitandani kama tablet😅
 
wapo wengi sana na tena sio tu vijijini hata mjini pia, last time nimeskiliza mpira kwenye radio nikiwa town kabisa kwa sababu nilikosa access ya TV…so it’s easy!
 
Tatizo hujatembea Nchi nzima Hadi ndanindani huko vijijini.ukienda vijijino huko redio ndiyo sehemu pekee ya kupata habari.
Sio vijijini mkuu hata mijini watu wanasikiliza mpira kwa redio, sio wote wana muda wa kupoteza kideoni.
Mfano madereva na makonda wa daladala, makuli masokoni, wauza maduka wengi muda wa kukaa kucheki mechi hawana hivyo huwa wanasikiliza.
 
Tbctaifa wanatangaza mpira wa ligi kuu na ile ya championship,hivi kuna watu bado,wanasikiliza mpira kupitia redio wakati Tv zimetapakaa kila kona?
Tatizo sio TV tatizo makampuni kama vile AZAM, DSTV, ZUKU, N.K unaweza kuwa nayo ila shda iko kwa makampuni
 
Wako wengi sana nikiwemo mimi, nina kiredio changu cha elfu kumi huwa nasafiri nacho kusikiliza mpira
 
Back
Top Bottom