Umechelewa sn kulitambuwa hilo mkuu,
Sio kusaidia mtu Kwa kutoa pesa pekee kunaleta riziki bali hata kuishi na watu tofauti tofauti nyumbani kwako,
Kuna watu wanakula jasho na kutumia nyota za wengine bila kujijuwa,
Na siku utakayowaondoa hao unaoishi nao nyumbani kwako ndy hapo utaanza kuona ugumu wa maisha.
Rejea Kwa wazee wetu wa zamani walikuwa wanapenda kulea watoto wa ndugu na watu baki na Wala hawakuwa na kipato kubwa,
lakini waliweza kusomesha watoto wa ndugu na kumudu maisha Kwa wepesi kabisa.
Leo maisha tunayaona magumu kwasababu ya ubinafsi wetu na choyo kwa Kila mtu kuishi na family yake pekee na sio kusaidia wengine.