Kuna watu wanabaraka sana ukiwasaidia mambo yako lazima yanyooke kwa kasi ya ajabu

Kuna watu wanabaraka sana ukiwasaidia mambo yako lazima yanyooke kwa kasi ya ajabu

Ni ngumu Ila epuka kutoa misaada hovyo hovyo na mbele za macho ya watu
Ni muhimu sana kuzungumza na Mungu wako ama kuisikiliza sauti ya rohoni unapotaka kutoa msaada wowote..! Roho ikisita acha mara moja


Inanitokeaga hiyo na nikisita nakukimbia kupokea simu.. Kumbe!!!!

Nitazidi kuwa makini, Amina.

Shukurani Kaka
 
Huwa kuna mdogo wangu ambaye tumezaliwa mama mmoja baba tofauti .

Huyu mtoto yupo bright Sana na very humble.

Huwa nikitoa hela za shule na mahitaji kumpatia , basi huwa nafanya madili mengi yanatiki Sana na Kwa haraka.


Nilivyogundua hili jambo nimekuwa nahakikisha namsaidia sana.

Nilichogundua watu wenye Nyota wapo .

Juzi nilimpa buku tano tu Ila Jana nimepiga mshindo mkubwa hatari na hii ni kawaida kila nikimpa hela lazima nipige mshindo.
Chai
 
Ni kweli,mfano mimi nikija kununua kitu kwako siku hiyo utauza sana
 
Yaani mtu anapiga kazi kwa bidii ili apate pesa, akizipata hajishukuru kwa bidii aliyoiweka anakimbilia kusema ni baraka.
 
Kwenye Biashara yangu. Alikuja mama mmoja anahitajika nimuuzie bidhaa lakini alikuwa na pesa ambayo kama nitauza itakuwa imekula kwangu. Basi mama akalalamika sana kuwa nimuuzie kwa bei hiyo.

Akaniambia nikimuuzia huenda mungu ataleta faida yangu kupitia wateja wengine na madua mengine kadha wa kadha.

Basi dah nikakubali kumuachia bidhaa.

Ile anatoka tu...walifululiza wateja kuingia sio kawaida na kila mteja bei ninayomtajia hazungushi kabisa.

Nilipiga sana pesa siku ile.

Naamini hilo mkuu.
 
Back
Top Bottom