Kuna wengine hatujui tulipokosea

Kuna wengine hatujui tulipokosea

EP 13

Siku zinavyooenda ndo navyokumbushwa kuwa zimebaki siku kadhaa au niache kazi. Mimi siogopi nishasema litakalo kuwa na liwe haya ni Maisha yangu yeye ana Maisha yake tayari. Hivyo ilikuwa kawaida kila siku jioni kuulizwa Lisa zimebaki siku ngapi nami namjibu kama jana zilikuwa ishirini basi leo ni 19 yaani hivyo kila siku zinavyoonda na siku zangu za notes ndio zinavyopungua.

Zilivyobaki tu wiki mbili nikampigia simu auntie na kumweleza kila kitu akanambia usijali nitaongea na baba yako. Au unaweza kuja kuishi Morogoro nikamwambia untie sitaki kuja Morogoro nataka na mimi nijaribu kujitegemea ila nikishindwa tu nitakuja Morogoro. Akanambia usijali nitaongea na baba yako tutashughulikia. Yaani huyu mama alikuwa na upendo wa agape. Alikuwa akibeba majukumu yetu kama mama yetu mzazi tulikuwa tukimfurahia sana.

Ikabaki wiki moja baba akanitumia laki tano akasema hii itakutosha kuanzia ukikwama sehemu utasema. Na mimi nilikuwa na akiba yangu kama laki mbili hivi sababu alikuwa akinitumia hela ndogo kila mwezi na hii ilikuwa kazi ya auntie.

Niliwatafuta madalali wakanitafutia chumba mtaa mwingine mbali kidogo na kwa babamdogo nikalipia nikanunua godoro, nikanunua vitu vya muhimu vyombo kidogo na jiko la gas ninapeleka kwenye chumba changu pasipo kusema nyumbani. Nilimuomba bosi ruhusa ya kushughulikia alinipa siku mbili. Nyumbani naaga kama naenda kazini kumbe mimi naenda kuweka sawa geto langu.

Zimebaki siku tatu kila kitu kipo tayari bado mimi kubeba nguo zangu tu na kuenda kuanza Maisha. Siku hiyo nilimuwahi baba mdogo kabla hajaniuliza kuwa zimebaki siku ngapi. Nikamwambia kuwa nina maongezi kidogo na yeye. Akasema sawa

Nikaingia chumbani kwangu nikachukua mkataba wangu na kumpa huku nikisema. Asante kwa kunilea na kunitunza kwa siku zote nilizokaa hapa. Mimi ni binadamu popote pale nilipokosea kwa kujua hata kwa kutukujua naomba unisamehe. Naomba baraka zako huko ninapoenda kuanza Maisha ila kama nikishindwa naomba unipokee tena.

Baba yangu mdogo akanijibu huku akijichekesha chekesha sasa mwanangu Lisa mbona ghafla hivyo mimi ujue nilikuwa nakutania. Wewe mtoto siku zote tulizokuwa wote hapa hujanijua tu baba yako! Sasa wadogo zako, mimi na mama yako tutakuwa wapweke tulishakuzoea ilibidi ungetoka hapa unaenda kwako yaani kwa mume wako au kwenye nyumba yako mwenyewe kuliko kwenda kuhangaika na manyumba ya kupanga.

Nikamwambia usijali hizo changamoto ndio zitakazonipa nguvu ya kuendelea kupambana. Alinisihi sana nisiondoke nikakataa akasema basi subiri tuagize hata msichana wa kazi akija uache umemfundisha kazi unatuachaje mwanangu hivi. Nikamwambia usijali mtazoea tu. Akawaita mke wake na mtoto wao na kuwaeleza kila kitu wote walibaki wamepigwa na butwaa. Kesho yake asubuhi nimeamka nikatafuta bodaboda nikafungasha mizigo yangu na kuelekea kwangu siku hiyo hata vyombo sikuwaoshea hakuna alotoka nje japo kuniaga kinafiki. Nikaondoka zangu kuanza Maisha mapya ya kujitegemea. Baba yangu na auntie wote walinipa baraka zao pia walikuwa wakinisapoti kwa vitu vidogo vidogo Lisa nina amani sasa na nipo huru.

Mama yangu ananikana tena mara ya pili.

Siku zimeenda mama yangu amekuja Tanzania kafikia kwa mdogo wake. Kule kwa mume wake hawezi kwenda tena sababu alimtoroka mume wake tena kwa kumuibia na kumsababishia maradhi mpaka mauti. Nikatapata taarifa kuwa yupo lakini anaumwa amelazwa hosptili nimepigiwa simu na mdogo wake kuwa kunahitajika kiasi cha hela sh laki moja ili aweze kuruhusiwa kutoka hospitalini.

Siku hiyo bosi alikuwepo ofisini wakati napokea taarifa ya mgonjwa ikabidi nimwombe ruhusa kwenda hospitali kumouona mgonjwa. Bosi wangu hakuwa na shida ameniruhusu lakini akanambia nimpe namba ya mama ili akitulia ampigie amjulie hali. Sijawahi kumwambia bosi chochote kuhusu mama yangu. nimeenda nimenunua matunda ya na juice ya box ili niende kumuona mgonjwa naenda nyumbani kuchukua hela ili nilipe mgonjwa aruhusiwe. Nawapigia simu kuwauliza amelazwa hospitali gani wananipiga danadana wanasema kama kumuona mgonjwa tukutane kwa mdogo wake. Nitume tu hela ili waweze kuruhusiwa make muda unavyooenda muda wa kuruhusu wagonjwa utaisha na akiendelea kukaa hospitalini gharama zitaongezeka. Nikaamua kumpigia mdogo wangu Joy na kumuuliza kama ana taarifa za ugonjwa wa mama. Akanijibu hivi wewe Lisa hujawaji kumjua mama yako ni mtu wa aina gani? Ni kweli mama yetu yupo hapa lakini haumwi hata mafua wanataka kula tu hela yako. Na kama huna kazi na hiyo pesa nitumie nusu yake nikale hata chips kuku. Nilikasirika nikaamua kuwatumia hela waliyoitaka nilivyo hakikisha imeenda na nikaona jina la mdogo wake ndo lililotokea nikanyamaza kimya sikutaka hata kuwauliza kama wamepata au kuwambia naenda kwa mdogo wake nikaachana nao.

Kumbe nilivyoondoka kazini bosi wangu alimpigia mama ili kujua hali yake. Bosi alivyojitambulisha kuwa ni bosi wangu mama alinikana kuwa mimi sio mtoto wake yeye ni shangazi yangu na ahumwi chochote wala hajanipigia simu kuwa anaumwa labda kama nimeenda kwenye mambo yangu mengine lakini sina mgonjwa yeyote. Bosi alivyonipigia simu na kuniambia alivyoambiwa na mama niliumia sana. Nami nikaamua kumweleza Maisha ya mama juu alinionea huruma sana ila akanambia usijali hipo siku moja tu mama yenu atakiri kuwa wewe ni mtoto wake.

Kesho yake asubuhi nipo zangu kazini napokea simu kutoka kwa mama yangu anafokea kwanini namtangazia kwa watu yangu kuwa anaumwa kwanini nimetuma hela halafu nimekaa kimya siulizi hata kama wameiona. Nilimjibu nikamwambia shida yake ilikuwa hela na nilimtumia alichotaka na kama huitaki waweza rudisha. Hamuwezi amini mama yangu alirudi South pasipo kunitafuta wala kuniaga. Nilikuja kusikia ameshaondoka zake siku hizi aniumizi sana nimeshaamua kuishi navyoona sawa kwangu madam simkwazi yeyote wala sivunji sheria ila siishi kwa kumridhisha mtu huku mimi naumia.

Mchana mwema nikipata nafasi natamani leo nimalize nimechoka mwenzenu kutype si mchezo.
 
Kuna wazazi huwa wanaangalia kati ya watoto wao ni nani amezubaa zubaa sana ili wamuendeshe. Nahisi wewe una hiyo character ndio maana ulikuwa unaonewa sana. Yaani umegundua kabisa mtu anakudanganya alafu unamtumia??!! Mbaya zaidi yeye kipindi cha bata hajawahi hata kukukumbuka!!!
Huo moyo kama bado unao uache haraka iwezekanavyo, unattract umasikini na kudhulumiwa!
 
Ep 14

Muda umeenda safari zangu za kwenda Morogoro hazikatika kila mwezi naenda. Naondoka ijumaa jioni na kurudi jumapili jioni sababu nikiwa nyumbani kwa auntie na baba pia na mdogo wetu tunayekutana kwa baba amekuja anaishi pale na wao ni furaha. Ukifika nyumbani huna wazo la kuwaza mama yangu angekuwepo hapa sababu aunt anatupa kila namna ya kufurahi. Kila nikienda Morogoro lazima niende kwa kaka Dav kumsalimia na kwa mama yake Dav. Mama anannipenda sana yaaani furaha.

Kilikuwa kipindi cha Christmas nimepewa likizo ya wiki mbili nabaki dar kufanya nini. Geto langu nimelifunga huyo Morogoro nipo tu nyumbani namwona mama yake Kaka Dav anakuja nyumbani tena pasipo kupiga simu kumbe wanafahamiana na aunti. Tumemkaribisha amepiga stori za hapa na pale jioni inaingia namsindikiza mpaka kwenye kituo cha daladala sababu alipojenga baba yangu na stand ya daladala sio mbali. Nimerudi nyumbani namuuliza auntie imekuwaje umefahamiana na mama yake kaka Dav? Ananiambia kuwa Dav ndiye aliyewakutanisha hivyo wao ni marafiki.

Nimekaa Morogoro nimemaliza wiki napokea simu kwa kutoka kwa kaka Dav na kunambia kuwa kesho nijiandae jioni atakuja kunichukua tutoke out anataka anioneshe wifi yangu mpya. Yule wa mwanzo najua kuwa walisha achana kama miezi sita hivi imepita yaani changamoto za mahusiano yake nilikuwa nazijua. Nafurahi kwenda kukutana na wifi mpya.

Nimemwambia auntie ananiambia sawa hamna shida. Lakini simwelewi auntie anavyokazana kumwagia sifa kedekede Kaka Dav. Utasikia Dav kijana mzuri, ana adabu, mpole, msikivu na mcha Mungu.

Saa kumi jioni nimejiandaa nipo dukani kwa auntie (duka la dawa na vipodozi) Kaka Dav anakuja na gari lake mpaka dukani kwa auntie kunichukua anashuka anamsalimia auntie naona kama wanapeana ishara Fulani nikasema labda wameshazoeana. Auntie anamtania Kaka Dav arudi salama huyo. Kaka Dav anajibu usiwe na wasiwasi kabisa yupo mikono salama. Namuanga auntie na kulifuata gari lilipo nataka nifungue mlango wa nyuma Kaka Dav ananiwahi na kufungua mlango wa mbele na kunionesha kwa ishara nimepanda kwenye gari. Kaka Dav anazunguka gari anaingia upande wa dereva na kuwasha gari hao tunaondoka huku nikimpungia auntie nae akitusindikiza kwa macho.

Ndani ya gari namuuliza kaka Dav. Kaka wifi yupo wapi sasa akanijibu usijali tutakutana nae huko tunapoenda atakuja ana usafiri wake. Nikasema sawa njiani tunapiga stori tu za kawaida. Tumeenda mpaka Nashera hotel tumeenda upande wa bar Kaka Dav anachagua sehemu ya meza yenye viti viwili tu. Namuuliza mbona tunakaa wapi na wifi akija atakaa wapi akanambia kwani wewe wasiwasi wako ni nini akija tutahama sasa hajafika itabidi tukae hapa. Siku hiyo kaka Dav alivaa vizuri ananukia hatari

Tumekaa wahudumu wamefika ananiuliza utakunywa nini namjibu fanta orange akanambia Lisa fanta wanakunywa wagonjwa. Ngoja nikuagizie wini nikakataa sababu mimi situmii kilevi. Ikumbukwe kutokana na kash kash za Maisha sio mtu wa kutoka wala kunywa pombe yaani sijichanganyi kabisa hivo hayo mambo ya vinjwaji hata siyajui.

Kaka Dav akasema basi kama hutaki wine chagua kati ya Bavaria na gland malta chagua moja. Nikachagua gland malta yeye ameletewa wine hata sijui wine gani. Wahudumu wa jikoni nao wamefika tumeshatoa oda zetu tunakunywa na kula na stori za hapa na pale tu.

Tumeshamaliza kula mimi namwambia kaka umenambia kuwa nakuja kuonana na wifi yangu, tumekula tumemaliza hajatokea wala sioni ukimpigia simu sio vizuri kabisa.

Kaka Dav huku amenikazia macho, jicho jekundu kali nikajikuta siwezi kumtazama usoni. Hali ya hewa imebadilika ghafla ile kujihamini nilikokuwa nako sina tena. Nini hiki lisa Mungu wangu nawaza.

Kaka Dav akanambia Lisa kuna mwanamke nampenda sana, nilimpenda toka siku ya kwanza nimekutana nae, ni miaka minne sasa toka nimfahamu huyu mwanamke nimemuonesha dalili zote za kuwa nampenda kimapenzi lakini yeye hata hajali. Je Lisa utanisaidia kumwambia huyu mwanamke kuwa nampenda.? Huku ananiangalia usoni

Kaka Dav si ulisema tunakuja kukutana na wifi. Sasa inakuwaje unaanza kuniambia habari za mwanamke mwingine?

Lisa sina mwanamke wala hakuna mwanamke tulikuja kukutana naye hapa ningekwambia ukweli usingekubali kuja hapa.

Sasa huyo mwanamke unayetaka nikusaidie kumwambia mimi namjua sasa?

Ndio unamjua, Lisa utanisaidia kumwambia nateseka sana juu yake sipo tayari kumkosa hata siku moja.

Akili yangu ikanituma kwa rafiki yangu wa field Husna basi kama sio Husna rafiki yangu Linda. Linda ni rafiki yangu wa chuo. Kipindi Kaka Dav anakuja kunitembelea chuo alikuwa anatukuta wote. Nikamjibu ndio nitakusaidia sisi wanawake tunaelewana nitakusaidia kaka Dav kuwa na amani kabisa.

Nikataka kujiridhisha ni yupi kati ya Husna au Linda. Nikamuuliza swali la kimtego. Ndio nitakusaidia lakini nitampataje?

Nitakupa namba yake ya simu umpigie na umwambie kuwa nampenda sana yeye ndo kila kitu kwangu.

Nachukua simu yangu nakumwambia haya nitajie.

Anaanza kutaja 0765………… nashangaa mbona inatajwa namba yangu sasa. Namwambia kaka Dav ebu acha masihala taja vizuri namba mbona unataja namba yangu?

Aya nakutajia tena 0765……. Mbona unarudia makosa yale yale sasa huyo mtu nitampigiaje?

Kaka Dav akanisogolea na kunishika mikono yangu yote miwili na kuniambia maneno haya.

Lisa mwanamke mwenyewe ni wewe nakupenda sana. Nakupenda ulivyo mtulivu, mpole na msikivu tafadhali Lisa.

Kaka Dav mimi nakuheshimu kama Kaka yangu, umenisaidia kwa mengi nakuheshimu sana.

Kama kaka yako na siyo kaka yako. Ananisogolea na kunikumbatia Lisa tafadhali usinikatae.

Nime muda kwanza nitakujibu.

Nategemea jibu zuri kutoka kwako nakupenda Lisa sipo tayari kukupoteza.

Tumekubaliana kuwa anipe muda nijifikirie. Tunaondoka kwenye gari hakuna anayemwongelesha mwingine. Ananifikisha dukani kwa auntie na kuondoka zake.

Tukutane kesho.
 
Ep 14

Muda umeenda safari zangu za kwenda Morogoro hazikatika kila mwezi naenda. Naondoka ijumaa jioni na kurudi ijumaa jioni sababu nikiwa nyumbani kwa auntie na baba pia na mdogo wetu tunayekutana kwa baba amekuja anaishi pale na wao ni furaha. Ukifika nyumbani huna wazo la kuwaza mama yangu angekuwepo hapa sababu aunt anatupa kila namna ya kufurahi. Kila nikienda Morogoro lazima niende kwa kaka Dav kumsalimia na kwa mama yake Dav. Mama anannipenda sana yaaani furaha.

Bikra inaenda kutolewa na kaka Dev
 
Alisema kama wew ulivyosema,ingawaje mimi sjawah kabisa tongoza humu jf

Nipo mkoani na wengi humu wapo dar na mbunye za mbali sinaga hamu nazo
Achana naye wala usimind mimi na mdogo wangu ni watu wa masihara..!! 😹

Ila nimeona unapambana kwa Lisa ila ukikaza unang’oa chuma hiko, trust me bro 🤣😹
 
Kweli wew na mdogo wako mna masihara mabaya sana

Yaan mdogo wako asivyo na akili,mimi kumkosoa tu kuwa Lisa anaandika kisukuma akasema namtaka

Wakat niliona kwenye maandishi Lisa anaandika Maneno ya kisukuma kama nalala au naalikwa badala ya nikalala au nikaalikwa
 
Nakuona teacher wa kiswahili, ila sisi watu wazima tuna VAR tushaona refa unaforce ubingwa kwa Arsenal 😹😹
 
Back
Top Bottom