Dadakidoti
JF-Expert Member
- Jul 26, 2024
- 399
- 1,409
- Thread starter
- #241
EP 13
Siku zinavyooenda ndo navyokumbushwa kuwa zimebaki siku kadhaa au niache kazi. Mimi siogopi nishasema litakalo kuwa na liwe haya ni Maisha yangu yeye ana Maisha yake tayari. Hivyo ilikuwa kawaida kila siku jioni kuulizwa Lisa zimebaki siku ngapi nami namjibu kama jana zilikuwa ishirini basi leo ni 19 yaani hivyo kila siku zinavyoonda na siku zangu za notes ndio zinavyopungua.
Zilivyobaki tu wiki mbili nikampigia simu auntie na kumweleza kila kitu akanambia usijali nitaongea na baba yako. Au unaweza kuja kuishi Morogoro nikamwambia untie sitaki kuja Morogoro nataka na mimi nijaribu kujitegemea ila nikishindwa tu nitakuja Morogoro. Akanambia usijali nitaongea na baba yako tutashughulikia. Yaani huyu mama alikuwa na upendo wa agape. Alikuwa akibeba majukumu yetu kama mama yetu mzazi tulikuwa tukimfurahia sana.
Ikabaki wiki moja baba akanitumia laki tano akasema hii itakutosha kuanzia ukikwama sehemu utasema. Na mimi nilikuwa na akiba yangu kama laki mbili hivi sababu alikuwa akinitumia hela ndogo kila mwezi na hii ilikuwa kazi ya auntie.
Niliwatafuta madalali wakanitafutia chumba mtaa mwingine mbali kidogo na kwa babamdogo nikalipia nikanunua godoro, nikanunua vitu vya muhimu vyombo kidogo na jiko la gas ninapeleka kwenye chumba changu pasipo kusema nyumbani. Nilimuomba bosi ruhusa ya kushughulikia alinipa siku mbili. Nyumbani naaga kama naenda kazini kumbe mimi naenda kuweka sawa geto langu.
Zimebaki siku tatu kila kitu kipo tayari bado mimi kubeba nguo zangu tu na kuenda kuanza Maisha. Siku hiyo nilimuwahi baba mdogo kabla hajaniuliza kuwa zimebaki siku ngapi. Nikamwambia kuwa nina maongezi kidogo na yeye. Akasema sawa
Nikaingia chumbani kwangu nikachukua mkataba wangu na kumpa huku nikisema. Asante kwa kunilea na kunitunza kwa siku zote nilizokaa hapa. Mimi ni binadamu popote pale nilipokosea kwa kujua hata kwa kutukujua naomba unisamehe. Naomba baraka zako huko ninapoenda kuanza Maisha ila kama nikishindwa naomba unipokee tena.
Baba yangu mdogo akanijibu huku akijichekesha chekesha sasa mwanangu Lisa mbona ghafla hivyo mimi ujue nilikuwa nakutania. Wewe mtoto siku zote tulizokuwa wote hapa hujanijua tu baba yako! Sasa wadogo zako, mimi na mama yako tutakuwa wapweke tulishakuzoea ilibidi ungetoka hapa unaenda kwako yaani kwa mume wako au kwenye nyumba yako mwenyewe kuliko kwenda kuhangaika na manyumba ya kupanga.
Nikamwambia usijali hizo changamoto ndio zitakazonipa nguvu ya kuendelea kupambana. Alinisihi sana nisiondoke nikakataa akasema basi subiri tuagize hata msichana wa kazi akija uache umemfundisha kazi unatuachaje mwanangu hivi. Nikamwambia usijali mtazoea tu. Akawaita mke wake na mtoto wao na kuwaeleza kila kitu wote walibaki wamepigwa na butwaa. Kesho yake asubuhi nimeamka nikatafuta bodaboda nikafungasha mizigo yangu na kuelekea kwangu siku hiyo hata vyombo sikuwaoshea hakuna alotoka nje japo kuniaga kinafiki. Nikaondoka zangu kuanza Maisha mapya ya kujitegemea. Baba yangu na auntie wote walinipa baraka zao pia walikuwa wakinisapoti kwa vitu vidogo vidogo Lisa nina amani sasa na nipo huru.
Mama yangu ananikana tena mara ya pili.
Siku zimeenda mama yangu amekuja Tanzania kafikia kwa mdogo wake. Kule kwa mume wake hawezi kwenda tena sababu alimtoroka mume wake tena kwa kumuibia na kumsababishia maradhi mpaka mauti. Nikatapata taarifa kuwa yupo lakini anaumwa amelazwa hosptili nimepigiwa simu na mdogo wake kuwa kunahitajika kiasi cha hela sh laki moja ili aweze kuruhusiwa kutoka hospitalini.
Siku hiyo bosi alikuwepo ofisini wakati napokea taarifa ya mgonjwa ikabidi nimwombe ruhusa kwenda hospitali kumouona mgonjwa. Bosi wangu hakuwa na shida ameniruhusu lakini akanambia nimpe namba ya mama ili akitulia ampigie amjulie hali. Sijawahi kumwambia bosi chochote kuhusu mama yangu. nimeenda nimenunua matunda ya na juice ya box ili niende kumuona mgonjwa naenda nyumbani kuchukua hela ili nilipe mgonjwa aruhusiwe. Nawapigia simu kuwauliza amelazwa hospitali gani wananipiga danadana wanasema kama kumuona mgonjwa tukutane kwa mdogo wake. Nitume tu hela ili waweze kuruhusiwa make muda unavyooenda muda wa kuruhusu wagonjwa utaisha na akiendelea kukaa hospitalini gharama zitaongezeka. Nikaamua kumpigia mdogo wangu Joy na kumuuliza kama ana taarifa za ugonjwa wa mama. Akanijibu hivi wewe Lisa hujawaji kumjua mama yako ni mtu wa aina gani? Ni kweli mama yetu yupo hapa lakini haumwi hata mafua wanataka kula tu hela yako. Na kama huna kazi na hiyo pesa nitumie nusu yake nikale hata chips kuku. Nilikasirika nikaamua kuwatumia hela waliyoitaka nilivyo hakikisha imeenda na nikaona jina la mdogo wake ndo lililotokea nikanyamaza kimya sikutaka hata kuwauliza kama wamepata au kuwambia naenda kwa mdogo wake nikaachana nao.
Kumbe nilivyoondoka kazini bosi wangu alimpigia mama ili kujua hali yake. Bosi alivyojitambulisha kuwa ni bosi wangu mama alinikana kuwa mimi sio mtoto wake yeye ni shangazi yangu na ahumwi chochote wala hajanipigia simu kuwa anaumwa labda kama nimeenda kwenye mambo yangu mengine lakini sina mgonjwa yeyote. Bosi alivyonipigia simu na kuniambia alivyoambiwa na mama niliumia sana. Nami nikaamua kumweleza Maisha ya mama juu alinionea huruma sana ila akanambia usijali hipo siku moja tu mama yenu atakiri kuwa wewe ni mtoto wake.
Kesho yake asubuhi nipo zangu kazini napokea simu kutoka kwa mama yangu anafokea kwanini namtangazia kwa watu yangu kuwa anaumwa kwanini nimetuma hela halafu nimekaa kimya siulizi hata kama wameiona. Nilimjibu nikamwambia shida yake ilikuwa hela na nilimtumia alichotaka na kama huitaki waweza rudisha. Hamuwezi amini mama yangu alirudi South pasipo kunitafuta wala kuniaga. Nilikuja kusikia ameshaondoka zake siku hizi aniumizi sana nimeshaamua kuishi navyoona sawa kwangu madam simkwazi yeyote wala sivunji sheria ila siishi kwa kumridhisha mtu huku mimi naumia.
Mchana mwema nikipata nafasi natamani leo nimalize nimechoka mwenzenu kutype si mchezo.