Kuna wenye nyumba wana roho mbaya usiombe

Kuna wenye nyumba wana roho mbaya usiombe

U
Nayajua ndio maana nimekuuliza, unless kama jina la debe kwa Mwanza lilikuwa likijulikana tofauti na nijuavyo...

Debe ilikuwa ni container la bati la lita kama ishirini hivi lililokuwa likijazwa mafuta ya kula kama OKI, KORIE...

Kama ilivyokuwa kwa mapipa watu wengi vijijini waliyatumia kwenye kuezekea nyumba, kuzungushia nyumba uzio au wale watu wa mashineni waliyatumia kama kipimo cha nafaka, wauzaji mataputapu waliyatumia kuhifadhia
Umenena vyema nyumba ilikuwa imeezekwa kwa hayo madebe na ilikuwa imezingushiwa ukuta wa tofali za tope
 
Natumaini wote mu bukheri wa afya vijana kwa wazee wenzangu

Naja tena na ushuda wa niliyoyapitia kwenye upangaji

Mwaka 1984 mitaa ya uhuru mwanza nikapata nyumba ya kupanga kwa mzee x na mkewe.

Nami nikiwa na mama watoto classmate wangu na watoto wetu wawili nikiwa nafanya kazi ma mzee mmoja hivi nisingependa kumtaja jina tulikuwa tunafuata mizigo ya magendo kisumu wakati huo hapa nchini hali tete sabuni tu ilikuwa ni lulu.

Sasa basi kwa kuwa muda mwingi niliutumia kazini na miaka hiyo hamna hata simu kuna muda nilikuwa narudi usiku nakuta geti limefungwa so nagonga mama yeyo ananifungulia kumbe mwenye nyumba akawa kama hapendi kurudi usiku nafunguliwa sasa basi mama watoto akapigwa bit no kifungua na funguo za getini akachukua mwenye mjengo.

Mimi sawa tu nikawa kila nikirudi naruka ukuta nazama ndani.

Duh! Usiombe mwenye mjengo akajua naruka ukuta nikasafiri kama siku 8 kurudi ukuta unepandishwa kozi 3 kwenda juu nikawa sina ujanja tena wa kuruka nikapiga hesabu nikaona vipande vya tofali nikavipanga nikadandia ukuta japo kushuka ilikuwa ni shida ikawa ndiyo zangu akajua.

Yaani ni moto hakuchoka nikaenda tena safari zangu kurudi nakuta juu ya ukuta pamezungushiwa vipande vya chupa no kugusa ukuta komando nikaishiwa mbinu sasa kila nikija nimechelewa naenda kulala gesti baada ya kama miezi mitatu nikapata nyumba nyingine.

Cha ajabu sasa huyu mzee na mkewe kila nikitoka safari sabuni na mafuta sukari chumvi lazima niwape lakini nikiri walikuwa na rohombaya sana nyumba yenyewe ilikuwa ya madebe japo enzi hizo nayo ilikuwa ni nyumba lakini hapana
Shule inafunguliwa lini.
 
Yaani vijana ukizeeka umekuwa kama zombie vile......wanataka uishi kama uko zama za mawe.......wanaona uzee kama ni upungufu wa akili......Kila ukifanya jambo la kisasa wanakushangaa utasema kichekesho......

Yaani kama ni amri yao wazee wote wakamatwe wakawekwe jumba la makumbusho ya taifa......
 
Yaani vijana ukizeeka umekuwa kama zombie vile......wanataka uishi kama uko zama za mawe.......wanaona uzee kama ni upungufu wa akili......Kila ukifanya jambo la kisasa wanakushangaa utasema kichekesho......

Yaani kama ni amri yao wazee wote wakamatwe wakawekwe jumba la makumbusho ya taifa......
Wapuuzi sana hawa vijana mkuu
 
Back
Top Bottom