Kuna wenye nyumba wana roho mbaya usiombe

Natumaini wote mu bukheri wa afya vijana kwa wazee wenzangu

Naja tena na ushuda wa niliyoyapitia kwenye upangaji

Mwaka 1984 mitaa ya uhuru mwanza nikapata nyumba ya kupanga kwa mzee x na mkewe.

Nami nikiwa na mama watoto classmate wangu na watoto wetu wawili nikiwa nafanya kazi ma mzee mmoja hivi nisingependa kumtaja jina tulikuwa tunafuata mizigo ya magendo kisumu wakati huo hapa nchini hali tete sabuni tu ilikuwa ni lulu.

Sasa basi kwa kuwa muda mwingi niliutumia kazini na miaka hiyo hamna hata simu kuna muda nilikuwa narudi usiku nakuta geti limefungwa so nagonga mama yeyo ananifungulia kumbe mwenye nyumba akawa kama hapendi kurudi usiku nafunguliwa sasa basi mama watoto akapigwa bit no kifungua na funguo za getini akachukua mwenye mjengo.

Mimi sawa tu nikawa kila nikirudi naruka ukuta nazama ndani.

Duh! Usiombe mwenye mjengo akajua naruka ukuta nikasafiri kama siku 8 kurudi ukuta unepandishwa kozi 3 kwenda juu nikawa sina ujanja tena wa kuruka nikapiga hesabu nikaona vipande vya tofali nikavipanga nikadandia ukuta japo kushuka ilikuwa ni shida ikawa ndiyo zangu akajua.

Yaani ni moto hakuchoka nikaenda tena safari zangu kurudi nakuta juu ya ukuta pamezungushiwa vipande vya chupa no kugusa ukuta komando nikaishiwa mbinu sasa kila nikija nimechelewa naenda kulala gesti baada ya kama miezi mitatu nikapata nyumba nyingine.

Cha ajabu sasa huyu mzee na mkewe kila nikitoka safari sabuni na mafuta sukari chumvi lazima niwape lakini nikiri walikuwa na rohombaya sana nyumba yenyewe ilikuwa ya madebe japo enzi hizo nayo ilikuwa ni nyumba lakini hapana
1984 mpaka leo hii, washafariki hao, my mind huwa inaniambia nyumba si lolote lile huwa nashangaa kweli mtu kujivunia nyumba au gari na kunyanyasa wengine, haya makitu tunayo kwa muda mfupi mno.
 
Ngoja nikipata muda mzuri nitaleta story za namna magendo toka kisumu yalivyokuwa yanafanyika enzi za kina clement mabina gitana masanja mawenge na kuna mhaya alishakuwa marehemu kuna jamaa alikuwa ndiyo msuka mipango kwa sasa ana kikampuni cha ujenzi
Hio nitaisubiri kwa hamu maana hawa miamba nlikua nikiwasikia tu kua ni wazee wa kazi, wanapiga michongo yao kenya. Clement Mabina alikua anabadili magari kama nguo..
 
Natumaini wote mu bukheri wa afya vijana kwa wazee wenzangu

Naja tena na ushuda wa niliyoyapitia kwenye upangaji

Mwaka 1984 mitaa ya uhuru mwanza nikapata nyumba ya kupanga kwa mzee x na mkewe.

Nami nikiwa na mama watoto classmate wangu na watoto wetu wawili nikiwa nafanya kazi ma mzee mmoja hivi nisingependa kumtaja jina tulikuwa tunafuata mizigo ya magendo kisumu wakati huo hapa nchini hali tete sabuni tu ilikuwa ni lulu.

Sasa basi kwa kuwa muda mwingi niliutumia kazini na miaka hiyo hamna hata simu kuna muda nilikuwa narudi usiku nakuta geti limefungwa so nagonga mama yeyo ananifungulia kumbe mwenye nyumba akawa kama hapendi kurudi usiku nafunguliwa sasa basi mama watoto akapigwa bit no kifungua na funguo za getini akachukua mwenye mjengo.

Mimi sawa tu nikawa kila nikirudi naruka ukuta nazama ndani.

Duh! Usiombe mwenye mjengo akajua naruka ukuta nikasafiri kama siku 8 kurudi ukuta unepandishwa kozi 3 kwenda juu nikawa sina ujanja tena wa kuruka nikapiga hesabu nikaona vipande vya tofali nikavipanga nikadandia ukuta japo kushuka ilikuwa ni shida ikawa ndiyo zangu akajua.

Yaani ni moto hakuchoka nikaenda tena safari zangu kurudi nakuta juu ya ukuta pamezungushiwa vipande vya chupa no kugusa ukuta komando nikaishiwa mbinu sasa kila nikija nimechelewa naenda kulala gesti baada ya kama miezi mitatu nikapata nyumba nyingine.

Cha ajabu sasa huyu mzee na mkewe kila nikitoka safari sabuni na mafuta sukari chumvi lazima niwape lakini nikiri walikuwa na rohombaya sana nyumba yenyewe ilikuwa ya madebe japo enzi hizo nayo ilikuwa ni nyumba lakini hapana

Wewe ndo una matatizo, sio huyo mzee, mambo mengine ni lujadili sio kuruka ukuta kama kibaka. 1. Mnauza vitu vya magendo, 2. Unaruka ukuta, ulishindwa kaa naye chini mkajadili?
 
Kuna mzee boya kweli,anakuja kudai kodi saa 8 usiku.hapo nishamkimbia kimbia.[emoji1787][emoji1787].natoka saa kumi usiku narudi saa 5 usiku
 
[emoji23] sasa unataka akudai kodi saangapi kama unarudi mida ya wanga?
 
Bro wakati wewe unahangaika na mwenye nyumba hapo Uhuru, mimi niko F3 Mwanza Sec aka Gorani ( hiyo Pamba Sec ikiwa primary school), nikitokea hapo Mirongo PS karibu na Community center na Lupondije na bhana bakwe akiwa tajiri hatari. Nikikaa Isamilo ya juu karibu na Susuma. Muvu Liberty na Tivoli. Now guess how old am I?
Utakua na hamsini plus
 
Heshima kwako Shem.
 
Hio nitaisubiri kwa hamu maana hawa miamba nlikua nikiwasikia tu kua ni wazee wa kazi, wanapiga michongo yao kenya. Clement Mabina alikua anabadili magari kama nguo..
Kuna mtu anaitwa matata huyu aliwahi kuwa meya wa manispaa ya ilemela sasa basi kama lilivyo jina lake matata na alikuwa mtata kweli
Aliwahi kuleta songombingo na watu wa serikali ilikuwa ni shida
 
Unayajua madebe lakini enzi hizo tena ilionekana nyumba ya maana hiyo mitaa ya uhuru rufiji unguja matofali yenyewe ni biskuti

Nayajua ndio maana nimekuuliza, unless kama jina la debe kwa Mwanza lilikuwa likijulikana tofauti na nijuavyo...

Debe ilikuwa ni container la bati la lita kama ishirini hivi lililokuwa likijazwa mafuta ya kula kama OKI, KORIE...

Kama ilivyokuwa kwa mapipa watu wengi vijijini waliyatumia kwenye kuezekea nyumba, kuzungushia nyumba uzio au wale watu wa mashineni waliyatumia kama kipimo cha nafaka, wauzaji mataputapu waliyatumia kuhifadhia ulabu n.k...
 
Wewe ndo una matatizo, sio huyo mzee, mambo mengine ni lujadili sio kuruka ukuta kama kibaka. 1. Mnauza vitu vya magendo, 2. Unaruka ukuta, ulishindwa kaa naye chini mkajadili?
Huyo father house alikuwa na akili mbovu sijawahi ona mimi nilikuwa namchukulia kama kaka yangu ila hakuwa muelewa hata kidogo
 
Back
Top Bottom