Kuna wenye nyumba wana roho mbaya usiombe

Kuna wenye nyumba wana roho mbaya usiombe

Toka 1984hadi Leo Bado unaogopa kumtaja!?ungemtaja tu ili akifa afe kwa amani,hata mashirika ya kijasusi Huwa sometime yanaachia Siri ambazo zimepitwa mda wake,auu kama amekufa atapumzika Sasa maana utakuwa umetoa ya rohoni😆😆😆😆😆
 
Wengi wao wana vielement vya kichawi huwa siyo bure
Ni kweli kabisa mkuu, jamaa ana roho ngumu/kishetani. Ila kwa jamaa huyu nimeshamchoka kiukweli. Nataka kwa mwakani nitafute eneo ninunue nami niweke fremu zangu, nimechoka kunyanyasika.
 
Toka 1984hadi Leo Bado unaogopa kumtaja!?ungemtaja tu ili akifa afe kwa amani,hata mashirika ya kijasusi Huwa sometime yanaachia Siri ambazo zimepitwa mda wake,auu kama amekufa atapumzika Sasa maana utakuwa umetoa ya rohoni😆😆😆😆😆
Alishakufa amebaki mke wake
 
62 kijana
Bro wakati wewe unahangaika na mwenye nyumba hapo Uhuru, mimi niko F3 Mwanza Sec aka Gorani ( hiyo Pamba Sec ikiwa primary school), nikitokea hapo Mirongo PS karibu na Community center na Lupondije na bhana bakwe akiwa tajiri hatari. Nikikaa Isamilo ya juu karibu na Susuma. Muvu Liberty na Tivoli. Now guess how old am I?
 
Hahahahaha lupondije
 
Natumaini wote mu bukheri wa afya vijana kwa wazee wenzangu

Naja tena na ushuda wa niliyoyapitia kwenye upangaji

Mwaka 1984 mitaa ya uhuru mwanza nikapata nyumba ya kupanga kwa mzee x na mkewe.

Nami nikiwa na mama watoto classmate wangu na watoto wetu wawili nikiwa nafanya kazi ma mzee mmoja hivi nisingependa kumtaja jina tulikuwa tunafuata mizigo ya magendo kisumu wakati huo hapa nchini hali tete sabuni tu ilikuwa ni lulu.

Sasa basi kwa kuwa muda mwingi niliutumia kazini na miaka hiyo hamna hata simu kuna muda nilikuwa narudi usiku nakuta geti limefungwa so nagonga mama yeyo ananifungulia kumbe mwenye nyumba akawa kama hapendi kurudi usiku nafunguliwa sasa basi mama watoto akapigwa bit no kifungua na funguo za getini akachukua mwenye mjengo.

Mimi sawa tu nikawa kila nikirudi naruka ukuta nazama ndani.

Duh! Usiombe mwenye mjengo akajua naruka ukuta nikasafiri kama siku 8 kurudi ukuta unepandishwa kozi 3 kwenda juu nikawa sina ujanja tena wa kuruka nikapiga hesabu nikaona vipande vya tofali nikavipanga nikadandia ukuta japo kushuka ilikuwa ni shida ikawa ndiyo zangu akajua.

Yaani ni moto hakuchoka nikaenda tena safari zangu kurudi nakuta juu ya ukuta pamezungushiwa vipande vya chupa no kugusa ukuta komando nikaishiwa mbinu sasa kila nikija nimechelewa naenda kulala gesti baada ya kama miezi mitatu nikapata nyumba nyingine.

Cha ajabu sasa huyu mzee na mkewe kila nikitoka safari sabuni na mafuta sukari chumvi lazima niwape lakini nikiri walikuwa na rohombaya sana nyumba yenyewe ilikuwa ya madebe japo enzi hizo nayo ilikuwa ni nyumba lakini hapana
...Unawapea nini Sasa ??? [emoji848]...

Sent from my TECNO BD4j using JamiiForums mobile app
 
Tulikuwa tunaena kuokota Jojo mabasi yakifika toka Kisumu na Musoma.
Ngoja nikipata muda mzuri nitaleta story za namna magendo toka kisumu yalivyokuwa yanafanyika enzi za kina clement mabina gitana masanja mawenge na kuna mhaya alishakuwa marehemu kuna jamaa alikuwa ndiyo msuka mipango kwa sasa ana kikampuni cha ujenzi
 
Naisubiri kwa hamu bro.
 
Mkuu kuna mengi ya kujifunza kwako..
Tunasubiri hiyo simulizi kwa hamu.
 
Pole sana, mwenye nyumba wangu simjui, napigiwa simu mara moja kila baada ya miezi sita ukimtumia chake ni baada ya miezi sita tena
 
Back
Top Bottom