Kuna wenye nyumba wana roho mbaya usiombe

Kuna wenye nyumba wana roho mbaya usiombe

Natumaini wote mu bukheri wa afya vijana kwa wazee wenzangu

Naja tena na ushuda wa niliyoyapitia kwenye upangaji

Mwaka 1984 mitaa ya uhuru mwanza nikapata nyumba ya kupanga kwa mzee x na mkewe.

Nami nikiwa na mama watoto classmate wangu na watoto wetu wawili nikiwa nafanya kazi ma mzee mmoja hivi nisingependa kumtaja jina tulikuwa tunafuata mizigo ya magendo kisumu wakati huo hapa nchini hali tete sabuni tu ilikuwa ni lulu.

Sasa basi kwa kuwa muda mwingi niliutumia kazini na miaka hiyo hamna hata simu kuna muda nilikuwa narudi usiku nakuta geti limefungwa so nagonga mama yeyo ananifungulia kumbe mwenye nyumba akawa kama hapendi kurudi usiku nafunguliwa sasa basi mama watoto akapigwa bit no kifungua na funguo za getini akachukua mwenye mjengo.

Mimi sawa tu nikawa kila nikirudi naruka ukuta nazama ndani.

Duh! Usiombe mwenye mjengo akajua naruka ukuta nikasafiri kama siku 8 kurudi ukuta unepandishwa kozi 3 kwenda juu nikawa sina ujanja tena wa kuruka nikapiga hesabu nikaona vipande vya tofali nikavipanga nikadandia ukuta japo kushuka ilikuwa ni shida ikawa ndiyo zangu akajua.

Yaani ni moto hakuchoka nikaenda tena safari zangu kurudi nakuta juu ya ukuta pamezungushiwa vipande vya chupa no kugusa ukuta komando nikaishiwa mbinu sasa kila nikija nimechelewa naenda kulala gesti baada ya kama miezi mitatu nikapata nyumba nyingine.

Cha ajabu sasa huyu mzee na mkewe kila nikitoka safari sabuni na mafuta sukari chumvi lazima niwape lakini nikiri walikuwa na rohombaya sana nyumba yenyewe ilikuwa ya madebe japo enzi hizo nayo ilikuwa ni nyumba lakini hapana
Misuko suko ya aina hii inapelekea kumiliki nyumba yako.
 
Mkuu au alikuwa anakuhisi kuwa ni kibaka flani?Yani Kodi Nampa na visabuni vya rushwa anapata halafu aniletee hizo?Mm nisingemsumbua hata mke wangu ningemgongea dirisha lake afungue yeye la sivyo anipe funguo yangu ya geti.Yani Nimekasirika utadhani hii sio chai
Wewe wasema
 
Bora huyo wa kwako mkuu. Kwenye moja ya biashara zangu, kuna fremu nimepanga lakini mwenye nyumba mjinga sijawahi ona.

Kama alikuwa anakudai hata elfu 10 na akaona wateja wamejaa kwako anakufata kuja kukuomba pesa yake ili watu wajue kuwa unadaiwa.

Na wakati mwingine biashara yako ikienda vizuri, ghafla atakuambia chumba chako anampango wa kukitumia, na hata kodi ikiisha anaomba uendelee.
 
Wengi wao wana vielement vya kichawi huwa siyo bure
 
Bora huyo wa kwako mkuu. Kwenye moja ya biashara zangu, kuna fremu nimepanga lakini mwenye nyumba mjinga sijawahi ona.

Kama alikuwa anakudai hata elfu 10 na akaona wateja wamejaa kwako anakufata kuja kukuomba pesa yake ili watu wajue kuwa unadaiwa.

Na wakati mwingine biashara yako ikienda vizuri, ghafla atakuambia chumba chako anampango wa kukitumia, na hata kodi ikiisha anaomba uendelee.
Huyo wako ana wazimu[emoji23],
 
Hapo mwaka ni 84 au 94 faza na bado unasema ulikua una machalii wawili...
Nimemaliza shule 1978 ilunda primary school mwaka 1981 nikaozeshwa mwaka 1982 tukajaliwa kupata watoto mapacha hao wawili mwaka 1983 nikapata mchongo kwenye magari ya chama cha ushirika nyanza nikapiga kazi miezi kama 9 hivi nikakutana na jamaa mfanyabishara enzi hizo akanichukua tukaanza kazi ya kwenda kuchukua bidhaa kisumu na hapo ndiyo nikapata kupanga mitaa ya uhuru
Nikakutana na hayo masaibu ya baba mwenye mjengo
 
Daah wewe ni Uncle angu umri wa wajomba zangu huo...mwaka 1978 nina miaka miwili nafungwa nepi tuu.
 
Back
Top Bottom