Sasa hivi wizi mtaani ni kero kubwa na sio magari tu.Ukiwa na bustani ya ndizi na mapapai hapo nyumbani wanaiba,ukifunga pamp ya maji wanaiba,ukianika nguo nje wanaiba,
mmelala usiku wanaingia sebuleni wanasafisha kila kitu,ukiwa na vimifugo hapo home wanavizia.Yaani hakuna amani huku mtaani kabisa. Miaka ya nyuma kidogo hawa wezi kuna watu walikuwa wakiwawekea heshima ya kutowaibia, wanajeshi polisi na wana usalama wengine.Lakini sasa hivi hawachagui. Lingine hawa wezi wa mitaani au vibaka wanauzarau huu mfumo wa kuwakamata na kufikishwa polisi au mahakamani.Wanakuibia huku wakiamini hata nikipelekwa polisi au gerezani si chochote, nitatoka tu ama kwa pesa au kwa kumaliza kutumikia kifungo ambacho wanaona ni muda mfupi tu, kwa hiyo hawajali kabisa. Mimi maoni yangu wangerekebisha hiyo sheria ya adhabu iwe kali zaidi, tatizo lingepungua kwa kiasi kikubwa.Kama ni kifungo miaka iongezwe na ikiwa ni kulipa faini iwe kubwa. Naona kifungo cha muda mrefu kwa wanaofanya mapenzi na watoto au wanfunzi kimefanya matukio hayo kuwa machache sana tofauti na kabla yake.