Kuna wizi wa vifaa vya magari maeneo ya Goba, Mbezi na Temeke

Kuna wizi wa vifaa vya magari maeneo ya Goba, Mbezi na Temeke

Yaan matukio haya ndio yananifanya niongeze Germany Shepherd nyumbani acha niingie gharama za kuwalisha
Kuna jamaa alikuwa na mbwa watano ndani ya geti. Ukuta una waya za umeme na alarm. Sijui waliwafanya nini mbwa wakalewa wote. Alarm haikulia na nyaya za umeme hazikufanya kazi wakaruka ukuta wakaingia ndani. Bahati nzuri sana jamaa akwasikia walipokuwa wanafungua geti ili watoe magari
 
Ndio tatizo la kubana ajira kwa vijana. Weka mlinzi
Hili ndilo tatizo la watanzania. Kwenye jamii kuna ujinga mkubwa wa kutotaka ku-deal na matatizo ili yaondoke bali kila mtu anatafuta quick solution yake ambayo siyo endelevu. Halafu sisi wenyewe hatuna jitihada zozote bali tunataka kufanyiwa vitu. Mitaani huko tunaishi na hawa wezi. Mwizi hawezi kutoka sehemu za mbali kwenda kuiba mahali bila kuwa na connection ya mwenyeji. Kwa nini tusifikiria kuchukuwa hatua za pamoja kuliko kila mtu kufanya solution yake na kuzidi kuyafanya maisha yawe magumu?
 
Sio hivyo mkuu,wizi wa aina hii,wezi wanakuwa na gari au bodaboda,wanakufuatilia tokea mjini au sehemu yoyote ulipokutana nao bila ya wewe kujua mpaka nyumbani kwako,wakishapajua kwako sasa wanaanza kusoma ratiba zako bila ya wewe kujua,kwahiyo siku ya kuja kukupiga mara nyingi wanakuja na gari,vitu vyote wakishachomoa kwenye gari lako wanahamishia kwenye gari yao ambayo wanaipaki sio mbali na kwako,wakishatimiza lengo lao wanaondoka kiulaini,na wanaweza kwa usiku mmoja wakaiba hata nyumba tatu au nne....
Dawa ni kufuga ma ng’ang’a tu
 
Hili ndilo tatizo la watanzania. Kwenye jamii kuna ujinga mkubwa wa kutotaka ku-deal na matatizo ili yaondoke bali kila mtu anatafuta quick solution yake ambayo siyo endelevu. Halafu sisi wenyewe hatuna jitihada zozote bali tunataka kufanyiwa vitu. Mitaani huko tunaishi na hawa wezi. Mwizi hawezi kutoka sehemu za mbali kwenda kuiba mahali bila kuwa na connection ya mwenyeji. Kwa nini tusifikiria kuchukuwa hatua za pamoja kuliko kila mtu kufanya solution yake na kuzidi kuyafanya maisha yawe magumu?
Sisi kwetu kuna sungusungu ya kudumu!
 
dah! pole ya watu wote waliokutana na haya majanga...

nina amini kuwa wafanyayo haya wanajulikana ila watu wanakausha maana zama za kale ndio zinarudi rasmi!

hizi kazi zilikuwa zinaweka watu mjini.

ni hasara sana!
 
Hii ilitukuta kioo cha saiti mira ile kukikuta hadi namba zimeandikwa hapo wakaona isiwe tabu wakakiachia kikadondoka chini kikavunjika vunjika kisa tumemchenjia
Walikidondosha hivyo kupoteza ushahidi.
 
Ukanda kwa kuanzia Mbezi Msumi, Goba, Mbweni, Boko mpaka Bunju na Mabwepande kuna wizi sana wa vifaa vya magari.

Ukiwa na gari jitahidi ujenge na parking, jamaa wakiingia huwa wanaparura sio kidogo
 
Jerk zipo kubwa dakika 2 tu ushanyenyua gari nzma.
Nuts kuna zile mashine za kufungulia nut
Chuma inapigwa spana kama gari ya formula 1 ile! Dakika 5 watu wamemaliza shughuli! Taa ina namna ya kupigwa twaa inalegea wanachomoa waya na kusepa nazo chap!
 
Omba yasikukute braza

Sawa mkuu ila sehemu nayokaa mie ,majirani wenzangu wanaibiwa lakini mimi huwa sijawahi kuibiwa,labda wanajua kwamba sio mlalavi maana mimi nimewahi sana kulala saa nane usiku na kuamka nimechelewa sana saa kumi na mbili na nusu,kwahiyo wanahisi huyu mwamba ukigusa dirisha tu kashastuka ndio maana hawapotezi muda kuja kwangu.
 
Habari wana JF

Kuna wizi mpya wa vifaa vya magari naona umekithiri sana huko maeneo ya Goba, Mbezi, Temeke watu wanaibiwa sana vifaa naomba Ma RC , POLISI N.K walishugulikie hili swala wezi wanajulikana n wanaonunua hivo vifaa vya wizi wanajulikanaa.

View attachment 1759159View attachment 1759160View attachment 1759162View attachment 1759164View attachment 1759167
View attachment 1757830
Mimi ilishawahi kunikuta uchungu wake naujua, na hata ukija kupata pesa za kurudishia hivyo vilivyoibwa itakuchukua muda mrefu sana saikolojia yako kurudi normal,hutokuwa mwenye amani kabisa,itafikia mahali utaona kama kuwa na gari ni kujitakia matatizo,hutakaa umuamini mtu yeyote anaefuatilia gari lako au kulikaribia,ila muda utafika utasahau...
 
Back
Top Bottom