Kuna wizi wa vifaa vya magari maeneo ya Goba, Mbezi na Temeke

Yaan matukio haya ndio yananifanya niongeze Germany Shepherd nyumbani acha niingie gharama za kuwalisha
Kuna jamaa alikuwa na mbwa watano ndani ya geti. Ukuta una waya za umeme na alarm. Sijui waliwafanya nini mbwa wakalewa wote. Alarm haikulia na nyaya za umeme hazikufanya kazi wakaruka ukuta wakaingia ndani. Bahati nzuri sana jamaa akwasikia walipokuwa wanafungua geti ili watoe magari
 
Ndio tatizo la kubana ajira kwa vijana. Weka mlinzi
Hili ndilo tatizo la watanzania. Kwenye jamii kuna ujinga mkubwa wa kutotaka ku-deal na matatizo ili yaondoke bali kila mtu anatafuta quick solution yake ambayo siyo endelevu. Halafu sisi wenyewe hatuna jitihada zozote bali tunataka kufanyiwa vitu. Mitaani huko tunaishi na hawa wezi. Mwizi hawezi kutoka sehemu za mbali kwenda kuiba mahali bila kuwa na connection ya mwenyeji. Kwa nini tusifikiria kuchukuwa hatua za pamoja kuliko kila mtu kufanya solution yake na kuzidi kuyafanya maisha yawe magumu?
 
Dawa ni kufuga ma ng’ang’a tu
 
Sisi kwetu kuna sungusungu ya kudumu!
 
dah! pole ya watu wote waliokutana na haya majanga...

nina amini kuwa wafanyayo haya wanajulikana ila watu wanakausha maana zama za kale ndio zinarudi rasmi!

hizi kazi zilikuwa zinaweka watu mjini.

ni hasara sana!
 
Hii ilitukuta kioo cha saiti mira ile kukikuta hadi namba zimeandikwa hapo wakaona isiwe tabu wakakiachia kikadondoka chini kikavunjika vunjika kisa tumemchenjia
Walikidondosha hivyo kupoteza ushahidi.
 
Ukanda kwa kuanzia Mbezi Msumi, Goba, Mbweni, Boko mpaka Bunju na Mabwepande kuna wizi sana wa vifaa vya magari.

Ukiwa na gari jitahidi ujenge na parking, jamaa wakiingia huwa wanaparura sio kidogo
 
Jerk zipo kubwa dakika 2 tu ushanyenyua gari nzma.
Nuts kuna zile mashine za kufungulia nut
Chuma inapigwa spana kama gari ya formula 1 ile! Dakika 5 watu wamemaliza shughuli! Taa ina namna ya kupigwa twaa inalegea wanachomoa waya na kusepa nazo chap!
 
Omba yasikukute braza

Sawa mkuu ila sehemu nayokaa mie ,majirani wenzangu wanaibiwa lakini mimi huwa sijawahi kuibiwa,labda wanajua kwamba sio mlalavi maana mimi nimewahi sana kulala saa nane usiku na kuamka nimechelewa sana saa kumi na mbili na nusu,kwahiyo wanahisi huyu mwamba ukigusa dirisha tu kashastuka ndio maana hawapotezi muda kuja kwangu.
 
Mimi ilishawahi kunikuta uchungu wake naujua, na hata ukija kupata pesa za kurudishia hivyo vilivyoibwa itakuchukua muda mrefu sana saikolojia yako kurudi normal,hutokuwa mwenye amani kabisa,itafikia mahali utaona kama kuwa na gari ni kujitakia matatizo,hutakaa umuamini mtu yeyote anaefuatilia gari lako au kulikaribia,ila muda utafika utasahau...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…