The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Kuna ming'ono kuwa rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete ndiye anaongoza Tanzania kwa kutumia remote kwa sasa. Je, kama ni kweli, inakuwaje tunayamaza?
Inakuwaje anaendelea kulipwa haki za usataafu wakati hajastaafu na anashiriki siasa kila siku? Inakuwaje kila serikali inaposhambuliwa, yeye ndo anajigeuza kuwa msemaji wake?
Kwanini kama hakuna namna, serikali inanyamaza na kumruhusu Kikwete awe msemaji wake asiye rasmi? Nani anajua historia za uhusiano wa wawili hawa?
Kunani kati ya rais Samia na Kikwete tusichojua na tunapaswa kukijua? Je, hii ni haki? Je, kama jamii na taifa tufanye nini ili kujiondoa kwenye mtego huu wa watu binafsi na mambo yao? Kweli, tumeishiwa hivi? Baba yenu najiwazia kimyakimya tu.