Kunani kati ya rais Samia na Kikwete tusichojua na tunapaswa kukijua? Je, hii ni haki?

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
11,099
Reaction score
13,709


Kuna ming'ono kuwa rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete ndiye anaongoza Tanzania kwa kutumia remote kwa sasa. Je, kama ni kweli, inakuwaje tunayamaza?

Inakuwaje anaendelea kulipwa haki za usataafu wakati hajastaafu na anashiriki siasa kila siku? Inakuwaje kila serikali inaposhambuliwa, yeye ndo anajigeuza kuwa msemaji wake?

Kwanini kama hakuna namna, serikali inanyamaza na kumruhusu Kikwete awe msemaji wake asiye rasmi? Nani anajua historia za uhusiano wa wawili hawa?

Kunani kati ya rais Samia na Kikwete tusichojua na tunapaswa kukijua? Je, hii ni haki? Je, kama jamii na taifa tufanye nini ili kujiondoa kwenye mtego huu wa watu binafsi na mambo yao? Kweli, tumeishiwa hivi? Baba yenu najiwazia kimyakimya tu.
 
Ni kikwete sasa maana kawashwa washwa mpaka kaonekana kila kona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…