Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
Ndiyo maana Kafulila aliamua kumwita mtu Mwizi hivi hivi, unaonesha ww ni mwizi wa mali ya umma, ndiyo maaana unawatetea sana wezi wenzako
Hongera kwa kukamilisha ule mpangoMwakaboko the great man, umezidiwa kalale upate mawazo mapya umezidi kucopy na kupaste!
hiyo katiba unayo itetea mipe ni ibara ipi inampa mwananchi madaraka ya kumwajibisha kiongozi aliye mchagua kama hakutimiza wajibu wake?
usiwe mvivu kusoma kama ulivyokawa kule ordinary level, kasome ibara ya 28-31 vikiwemo na vifungu vyake vyote, majibu ya swali lako hapo juu utayapata tena mazuri tuu.
unawaza kujenga ghorofa angani wewe,nafasi za uteuzi zitafutwe kiushindani unafikiri serikali ni kampuni???? Kachukue fomu mwaka huu ugombee urais tuone kama utayafanya hayo na mawazo yako ya kutawala familia yako,tena unaonekana wewe ni dikteta.
jamani kumbe hutambui serikali kuwa ni kampuni?
Mkiungana watu kumi mkaweka mitaji yenu pamoja kutafuta faida chombo chenu kinatwa kampuni.
Hebu niambie watu milioni 40 na kitu walioweka rasilimali zao pamoja na wakaunda chombo cha kusimamia rasilimali hizi kwa maana kinazitumia rasilimali kutengeneza mapato na wakaweka utaratibu wa mapato badala ya kugawana watumie kujenga miundo mbinu chombo hicho kinatwaje?
Kimsingi kwa maana ya kampuni serikali ni kampuni na wamiriki wa kampuni hii ni wananchi.
Yaani wewe nakushakushangaa kwa maana unaamini shirika linaloanzishwa kwa kodi na mapato ya watanzania wote mtu mmoja ateue rafiki yake, au mshirika wake ndio inafaa tena ambaye hana sifa ndio sahihi kuliko kusema shirika hili washindanie watanzania wote na mwenye sifa zaidi ndiye achaguliwe kuliendesha na akishindwa anafukuzwa mara moja.
Lakini akileta faida anaongezewa mkataba
UFO asante kwa kumueekeza pale sura ya kusoma,
Na mie huwa napata utata naomba nisaidie, kiongozi wa UMMA ni yupi? kuna sehemu wameainishwa watumishi/viongozi wa umma? naomba msaada. nipe ibara na mie
bwana ego, serikali sio kampuni kuwa muelewa bhana, mambo mengine hayahitaji elimu kubwa wajameni
Kumbuka maneno yako ya awali ulokasema kuhusu serikali ni kampuni, waswahili husema ukiwa mwongo jitahidi uwe na kumbukumbu lkn wewe sahv unaanza kutugeuka unakataa maneno yako ulokatoa awali tukueleweje hapo?tatizo lenu mnaangalia kampuni kwa kuangalia majina na serikali kwa kuangalia majina.
nenda katika maana ya kampuni ni kitu gani na urudi katika maana ya serikali ni kitu gani utagundua kuwa serikali ni kampuni inayomulikiwa na wananchi wote kwa pamoja ambapo wamiliki wa kampuni hii ni wananchi wenyewe.
lakini kampuni ya kumilikiwa na wananchi wote tayari imepewa special name kwa maana ya kuitwa serikali.
lakini ukichukua kampuni ni kitu gani na kinaundwa vipi si kwa maana ya sheria zilizopo bali kama una kampuni inayomilikiwa na watu wengi utaratibu wao ni ule ule wa kuweka katiba ya kuwaongoza inayoweka utaratibu wa kila kitu.
wananchi hawa wanachagua bodi ya kusimamia kampuni hii ambayo ni bunge
wananchi hawa wanamchagua mkurugenzi mtendaji ambaye ni raisi.
sasa sielewi ni kitu gani kinachowafanya kidai serikali si kampuni?
nitawashangaa pale mtakapokaa watu watano na kuamua kuweka mitaji yenu pamoja na kuunda chombo cha kusimaia mitaji hiyo na kuitumia kuwaletea faida na chombo hicho mkakiita kampuni lakini pale watu milioni arobaini na kitu wanapoweka mitaji yao pamoja na kuunda chombo cha kusimamia mitaji hiyo kuwaletea faida ambayo wameamua itumike si kwa kugawana fedha bali kujenga miundo mbinu ya jamii basi mnasema hii si kampuni?
ni kampuni lakini jina lake ni serikali kama ambavyo kila kampuni ina jina lake linaloitofautisha na makampuni mengine.
Kumbuka maneno yako ya awali ulokasema kuhusu serikali ni kampuni, waswahili husema ukiwa mwongo jitahidi uwe na kumbukumbu lkn wewe sahv unaanza kutugeuka unakataa maneno yako ulokatoa awali tukueleweje hapo?
tatizo wewe hauelewi nimekuambia tatizo wewe unaangalia majina na unatofautisha herufi mimi nalinganisha maana na katika hilo maelezo yangu tangu mwanzo bado niko pale pale.
Letatizo lako wewe unadhani nikisema inaitwa serikali nimeitoa katika orodha ya makampuni.
Kusema inaitwa serikali ni sawa na kusema makampuni yenye mmiliki mmoja mmoja yanaitwa hivi au yenye wamiriki wengi yanaitwa hivi.
Maelezo yangu yote niliyokutajia yanaeleza ni vitu gani vinaifanya serikali yeyote kuwa ni kampuni lakini nikahitimisha kwa kueleza kuwa makampuni yanayomilikiwa na wananchi wote yenye kusimamia rasilimali zao huitwa special name kuwa ni serikali.
Au kwa kifupi serikali ni kampuni ya wananchi inayomilikiwa na wananchi wote katika nchi husika ambayo mtaji wake ni rasilimali za nchi na inayotakiwa kutumia rasilimali za jamii kusimamia shughuli zote zinazofanyika katika jamii na kuwaletea wananchi maendeleo.
Sasa kwa nini wewe unayesema serikali sio kampuni usiseme ni kitu gani katika maana ya kampuni kinachokosekana katika serikali kinachoinyima sifa ya kuwa kampuni.
unataka nisemeje wakati hilo linafahamika kuwa serikali sio kampuni??? Lol
nakuwa na mashaka hata kama unaelewa kampuni ni nini?
unataka nisemeje wakati hilo linafahamika kuwa serikali sio kampuni??? Lol
ningekujibu kwa lugha uliyotumia lakini nitakuwa najishusha, kwangu mimi naamini kundi kutajwa katika katiba ni useless kama hakuna mfumo wa kulinda haki hiyo iliyotajwa.
mimi sisomi katiba kwa kuangalia ibara fulani inasema nini bali naenda mbali zaidi kuangalia baada ya katiba kusema nini kinafuata na ni nani atatekeleza na je yule anayetakiwa kutekeleza nani atahoji au mhusika ataenda wapi na kuna mfumo unaofanya haki itendeke.
katiba haisomwi kwa kifungu kimoja kwani huwezi kupata kitu chochote katika maisha kwa kutumia kifungu kimoja tu cha katiba na hilo ndilo tatizo la wengi.
Hao vichomi wa lumumba wamewekwa hapa kwa ajili ya kupinga au kuharibu mada yoyote kuhusu katiba mpya, wameandikishwa wiki moja na hawachangii mada nyingine yoyote.
Ndugu ngoja usaidiwe hapo, nakushauri ukasome Ibara ya 231 utapata mwanga wa hiko ulichomuomba huyo jamaa hapo. Lakini pia kasome ile SURA YA NNE IBARA YA 28-31 Utapata kujua hayo pia.
We haika naona unaona raha tu kubishana bishana, sasa nakushauri kama unayo hiyo katiba ni vema ukaisoma yote kipengele hadi kipengele usipende usomewe na watu coz ukisomewa afu ukaja kuambiwa kuna hiki kuna kile bado utaanza kuuliza tena kuna kitu flani? Usiwe kama mwanafunzinwa chekechea na epuka uvivu wa kusoma. Na huyo jamaa alokupa hizo sehemu alitakiwa alupe darasa kama hili piaMajukumu ya Tume 231.-(1) Majukumu ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma yatakuwa ni kufuatilia na kuchunguza tabia na mwenendo wa viongozi wa umma kwa madhumuni ya kusimamia na kuhakikisha kuwa maadili na miiko ya uongozi wa umma inazingatiwa, inalindwa na kuheshimiwa katika utumishi wa Serikali, Bunge, Mahakama, taasisi na idara nyingine zote za umma. (2) Bila kuathiri masharti ya jumla ya ibara ndogo ya (1), majukumu mahsusi ya Tume yatakuwa ni: (a) kusimamia maadili katika utumishi wa umma; (b) kuchunguza tabia na mwenendo wa kiongozi wa umma na kuchukua hatua pale inapostahili; na (c) kusimamia sheria kuhusu maadili ya viongozi wa umma. (3) Bunge litatunga sheria kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Ibara hii.
Kwa kusoma majukumu ya tume. Tunawezaje kumjua kiongozi au mtumishi wa umma ni yupi?
Mie ninaomba sehemu ambayo hawa watu wamekuwa defined kwenye katiba