PreGE2025 Kundi la “Wachokonozi” wamekamatwa na watu waliodai kuwa ni Askari Polisi katika eneo la Maji ya Chai, Arumeru, Arusha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
Kundi la Wachokonozi linaloundwa na Joseph Mrindoko na Jackson Kabalo wamekamatwa leo na watu waliodai kuwa ni askari polisi katika eneo la Maji ya Chai, wilayani Arumeru, Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo, watu hao waliovamia nyumba ya Joseph Mrindoko walikuwa wamevalia kiraia na kujitambulisha kama Askari Polisi kabla ya kuwaweka chini ya ulinzi wahusika hao wawili.

Taarifa zinaeleza kuwa vifaa vyote vya kazi vya kundi hilo, vikiwemo kamera, kompyuta na nyaraka mbalimbali, vilichukuliwa na watu hao bila kuwasilishwa hati yoyote ya upekuzi au maelezo rasmi ya sababu ya ukamataji huo.

Hadi sasa, haijafahamika rasmi ni kituo gani cha polisi kilichohusika na tukio hilo, wala sababu ya ukamataji wa wachokonozi hao ambao wamekuwa wakijulikana kwa kazi zao za ufuatiliaji wa masuala ya kijamii na kisiasa.

Credit: Martinmaranjamasese
 
Kwa Sasa ukikubali kukamatwa na watu ambao hawana viongozi wa mtaa et wanajiita Polisi umekwisha. Pambana kadri uwezavyo, Bora kufa ukimpambana kuliko kufa ukisulubiwa. Do It at your own risk
 
Kundi la Wachokonozi linaloundwa na Joseph Mrindoko na Jackson Kabalo wamekamatwa leo na watu waliodai kuwa ni askari polisi katika eneo la Maji ya Chai, wilayani Arumeru, Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo, watu hao waliovamia nyumba ya Joseph Mrindoko walikuwa wamevalia kiraia na kujitambulisha kama Askari Polisi kabla ya kuwaweka chini ya ulinzi wahusika hao wawili.

Taarifa zinaeleza kuwa vifaa vyote vya kazi vya kundi hilo, vikiwemo kamera, kompyuta na nyaraka mbalimbali, vilichukuliwa na watu hao bila kuwasilishwa hati yoyote ya upekuzi au maelezo rasmi ya sababu ya ukamataji huo.

Hadi sasa, haijafahamika rasmi ni kituo gani cha polisi kilichohusika na tukio hilo, wala sababu ya ukamataji wa wachokonozi hao ambao wamekuwa wakijulikana kwa kazi zao za ufuatiliaji wa masuala ya kijamii na kisiasa.

Credit: Martinmaranjamasese
Yaani bado na nyie wengine mnaruhusu tu watu waliovaa kiraia na kusema wao ni polisi wafanye mambo haya? Piga, ua! Itajulikana mortuary baadae kama kweli ni polisi.
 
Mkuu watu wanakuja na miguu ya kuku sisi tuna korodani tu. Ulitegemea tuwafanye nn?
Unajua kitu wasijojua watu ni kwamba, watu kama hao hata wakiwa na miguu ya kuku sio rahisi kuitumia kwenye kundi la watu.Wanajua wakiua mtu ndio hukumu yao ya kifo, na wakiwa watatu nyie mko kumi, hawawezi kuua watu wote kabla hawajadhibitiwa. Na wanajua kuna uwezekano wao kupona ikiwa hawatatumia silaha, kuliko wakitumia

Kwa hiyo inahitaji ujasiri tu katika kuwakabili kama kundi.
 
Unajua kitu wasijojua watu ni kwamba, watu kama hao hata wakiwa na miguu ya kuku sio rahisi kiutumia kwenye kundi la watu.Wanajua wakiua mtu ndio hukumu yao ya kifo, na wakiwa watatu nyie mko kumi, hawawezi kuua watu wote kabla hawajadhibitiwa. Na wanajua kuna uwezekano wao kupona ikiwa hawatatumia silaha, kuliko wakitumia

Nadhani elimu inahitajika mkuu. Unajua kwa tulio wengi bunduki ni mashikolo mageni.
 
Unajua kitu wasijojua watu ni kwamba, watu kama hao hata wakiwa na miguu ya kuku sio rahisi kiutumia kwenye kundi la watu.Wanajua wakiua mtu ndio hukumu yao ya kifo, na wakiwa watatu nyie mko kumi, hawawezi kuua watu wote kabla hawajadhibitiwa. Na wanajua kuna uwezekano wao kupona ikiwa hawatatumia silaha, kuliko wakitumia

Kwa hiyo inahitaji ujasiri tu katika kuwakabili kama kundi.
Shida haijulikani risasi itaanza kwa nani kati ya hao 10
 
Back
Top Bottom