PreGE2025 Kundi la “Wachokonozi” wamekamatwa na watu waliodai kuwa ni Askari Polisi katika eneo la Maji ya Chai, Arumeru, Arusha

PreGE2025 Kundi la “Wachokonozi” wamekamatwa na watu waliodai kuwa ni Askari Polisi katika eneo la Maji ya Chai, Arumeru, Arusha

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wanajua yote hayo, ndiyo maana wamechagua kutokaa kimya, pia wanaheshimu maoni na uchaguzi wa wengine ndiyo maana huyo mmoja anamwambia mwenzake hao watakao tiki it'a okay.
Sasa hao watu wenu watakao wabaka inakuwaje hawaheshimu uchaguzibwa wengine? Kwani nini mtake wote wafanane na nyie kimisimamo? Kwanini muine kubaka ndiyo njia sahihi, kwanini kama misimamo yao ni jinai msiwachukulie hatua za kisheria badala yake mtishie kuwabaka?
Bro usinihusishe na ccm kabisa , mimi kitu naongelea hapo ni swala la kulinda uhai wako ni jukumu lako , hata kama nikupiga kimya ili kulinda uhai ni bora upige tu
 
Vijana hapa kati wamejichanganya vibaya sana , tatizo mliwapa kichwa wakajikita wanayakoroga wangebaki huko huko kwenye dini wanapopakosoa , alaf wao wakikosolewa wanatukana
Walipagawa zaidi Mange alivyo wapost na kuwasifu basi ikawa kila siku wana mkejeli Rais na serikali yake.

Wenzao wana kosoa wapo nje ya nchi wao wana kosoa wapo Tanzania.

Hawakutumia busara.

Mungu awasaidie watoke salama.

Ila wakitoka waachane na mambo ya siasa.
 
Kundi la Wachokonozi linaloundwa na Joseph Mrindoko na Jackson Kabalo wamekamatwa leo na watu waliodai kuwa ni askari polisi katika eneo la Maji ya Chai, wilayani Arumeru, Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo, watu hao waliovamia nyumba ya Joseph Mrindoko walikuwa wamevalia kiraia na kujitambulisha kama Askari Polisi kabla ya kuwaweka chini ya ulinzi wahusika hao wawili.

Taarifa zinaeleza kuwa vifaa vyote vya kazi vya kundi hilo, vikiwemo kamera, kompyuta na nyaraka mbalimbali, vilichukuliwa na watu hao bila kuwasilishwa hati yoyote ya upekuzi au maelezo rasmi ya sababu ya ukamataji huo.

Hadi sasa, haijafahamika rasmi ni kituo gani cha polisi kilichohusika na tukio hilo, wala sababu ya ukamataji wa wachokonozi hao ambao wamekuwa wakijulikana kwa kazi zao za ufuatiliaji wa masuala ya kijamii na kisiasa.

Credit: Martinmaranjamasese
Mimi nawakubali Kwa sababu za kuwaamsha watu kuhusu utapeli wa dini.

Sema Sasa Huwa wanaita dini za watu upumbavu na wapumbavu labda hapo ndipo wanaingia kwenye matatizo na mamlaka hata hivyo haikufaa kuwakamata Kwa staili hiyo.
 
Vijana hapa kati wamejichanganya vibaya sana , tatizo mliwapa kichwa wakajikita wanayakoroga wangebaki huko huko kwenye dini wanapopakosoa , alaf wao wakikosolewa wanatukana
Umeandika nini?
 
Vijana hapa kati wamejichanganya vibaya sana , tatizo mliwapa kichwa wakajikita wanayakoroga wangebaki huko huko kwenye dini wanapopakosoa , alaf wao wakikosolewa wanatukana
Tatizo wimbi la vijana huku mtandaoni kila mtu ni expert kweny siasa yani mtu akiwez kuleta kahoja tofauti unaonekana genious afu ubaya wengi wao wala hawajui chochote kuhus maswala kisiasa, uongozi Na hata maswal ya kiserikali yanavyoenda upinzani wameshawaingiza kweny mfumo kuwa kuchukia serikali yako ndio usmart huo na hamna kitu chochote cha maana utakachoona serikali inafanya na serikali haiko kwa ajili yako
 
Unajua kitu wasijojua watu ni kwamba, watu kama hao hata wakiwa na miguu ya kuku sio rahisi kiutumia kwenye kundi la watu.Wanajua wakiua mtu ndio hukumu yao ya kifo, na wakiwa watatu nyie mko kumi, hawawezi kuua watu wote kabla hawajadhibitiwa. Na wanajua kuna uwezekano wao kupona ikiwa hawatatumia silaha, kuliko wakitumia

Kwa hiyo inahitaji ujasiri tu katika kuwakabili kama kundi.
Sasa mkuu umevamiwa nyumbani utawezaje kufanya hivyo, na ukionesha ukaidi ndio yanakua yale yale ya mdude pigwa kichwani damu zinavuja.

Inshort hiki unachokisema chafaa kiwe akilini kwa Kila mwananchi kwa namna ile ile ambayo huwa wanapeana taarifa za wizi iwe hivyo hivyo kupeana taarifa kwa upande huo.
 
Vijana wawili Joseph Mrindoko na Jackson Kabalo wanaounda kundi la "Wachokonozi" wamevamiwa na watu wenye silaha waliojitambulisha kuwa ni Askari Polisi wakiwa nyumbani kwao maeneo ya Maji ya Chai, wilayani Arumeru mkoani Arusha.
View attachment 3376994
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, watu hao walikuja na gari aina ya Landcruzer wakiwa wamevalia kiraia na wamebeba silaha za moto. Walipoingia ndani waliwaweka vijana hao chini ya ulinzi lakini walipoambiwa watoe vitambulisho kuthibitisha kama wao ni Polisi kweli walikataa.

Walifanya upekuzi kwenye nyumba hiyo bila kufuata taratibu. Walipoambiwa waitiwe mjumbe wa serikali ya mtaa ili awe shahidi walikataa, na kusema wasifundishwe kazi. Katika upekuzi huo wamechukua vifaa mbalimbali ikiwemo camera, computer, microphones, tape revorder, na nyaraka mbalimbali zilizokuwemo, kisha kuwafunga pingu "Wachokonozi" na kuondoka nao.
View attachment 3376994
Majirani walipouliza wanawapeleka kituo gani cha Polisi, watu hao hawakujibu bali waliondoa gari kwa mwendo mkali. Ndugu wameenda kituo cha Polisi Maji ya Chai lakini hawajawakuta. Hadi sasa, haijafahamika wamepelekwa kituo gani lakini ndugu wanaendelea kufuatilia.

Familia za "Wachokonozi" zinaomba tuwasaidie kupaza sauti ili ndugu zao wapatikane wakiwa hai. Wanaomba waliowakamata wasiwaue wala kuwapoteza bali kama wanatuhumiwa kwa makosa yoyote basi wawapeleke mahakamani kwa hatua za sheria.

Credit: Malisa GJ
Hakuna kituo cha polisi Maji ya Chai. Kuna post King'ori na kuna makao makuu ya polisi wilaya pale Usa River ambapo ndio karibu zaidi na Maji ya Chai.

Ila nilisema, vijana tucheze na vyote ila sio michezo inayoigusa amani ya hili taifa. Gharama yake sio poa.
 
Wanaweza kupewa kesi ya kukashifu Imani za watu kinyume na Sheria ya Makosa ya Jinai ya Tanzania. Na ushahidi upo kwenye videos zao kibao.

Wakristu na waislamu watasema hilo ni pigo wamepigwa na Mungu
 
Kundi la Wachokonozi linaloundwa na Joseph Mrindoko na Jackson Kabalo wamekamatwa leo na watu waliodai kuwa ni askari polisi katika eneo la Maji ya Chai, wilayani Arumeru, Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo, watu hao waliovamia nyumba ya Joseph Mrindoko walikuwa wamevalia kiraia na kujitambulisha kama Askari Polisi kabla ya kuwaweka chini ya ulinzi wahusika hao wawili.

Taarifa zinaeleza kuwa vifaa vyote vya kazi vya kundi hilo, vikiwemo kamera, kompyuta na nyaraka mbalimbali, vilichukuliwa na watu hao bila kuwasilishwa hati yoyote ya upekuzi au maelezo rasmi ya sababu ya ukamataji huo.

Hadi sasa, haijafahamika rasmi ni kituo gani cha polisi kilichohusika na tukio hilo, wala sababu ya ukamataji wa wachokonozi hao ambao wamekuwa wakijulikana kwa kazi zao za ufuatiliaji wa masuala ya kijamii na kisiasa.

Credit: Martinmaranjamasese
In fact kuna kikundi cha wahuni kinatumia jina la polisi. Inabidi raia tuwe na silaha wakija wakikosa kitambulisho unawaua
 
Tatizo wimbi la vijana huku mtandaoni kila mtu ni expert kweny siasa yani mtu akiwez kuleta kahoja tofauti unaonekana genious afu ubaya wengi wao wala hawajui chochote kuhus maswala kisiasa, uongozi Na hata maswal ya kiserikali yanavyoenda upinzani wameshawaingiza kweny mfumo kuwa kuchukia serikali yako ndio usmart huo na hamna kitu chochote cha maana utakachoona serikali inafanya na serikali haiko kwa ajili yako
Kweli, vijana wengi wameingia kwenye harakati za kisiasa wakiww na upeo mdogo sana wa namna mifumo inavyofanya kazi na ipi ni mipaka yao. Vijana wanaropoka mambo mazito sana kiuwepesi wepesi.

Hawataki kiheshimu mamlaka na wala hawaijui sanaa ya siasa wao ni kuwa radical tu wakidhani ndio sifa bora kumbe hakuna serikali yoyote inayotaka watu radical na conservative.
 
Back
Top Bottom